Nimekutana na mzee mmoja mstaafu katika kuongea nae nikagundua ana mipangilio ya miaka mingi mbele.
Mosi: Ana eneo ekari 5-6 Kongowe ya Mbagala hapa ana ndoto ya kujenga shule.
Pili: Ana eneo ekari moja Mabwepande hapa ana mpango wa kujenga nyumba za kupangisha.
Tatu: Ana eneo ekari moja na nusu Fukayosi, hapa ana mpango wa kulima mananasi.
Nimeangalia mipango yake na umri wake kwa akili yangu imegoma hasa hapo kwenye shule na ukizingatia ni miaka 13 sasa tangia astaafu. Naamini jamii forum kuna watu wenye umri tofauti na uzoefu tofauti.
Je, mstaafu wa JWTZ anaweza kutekeleza hayo? Kuuza eneo hataki kusikia kabisa tena ukimshauri mnaweza kugombana.