Ukiwa kwenye daladala achana na simu dada, hutaolewa!

Ukiwa kwenye daladala achana na simu dada, hutaolewa!

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
27,699
Reaction score
65,338
Umekaa kwenye siti au umesimama ndani ya daladala jirani kabisa na mkaka lakini muda wote upo bize kuhama toka social network moja kwenda nyingine mpaka mwisho wa safari. Hata salamu hujatoa na hata mkaka kukupa salamu kashindwa kwa jinsi ulivyo bize.

Vidole vinatabasamu lakini sura inazidi kukunjamana kwasababu ya kufuatilia maandishi kwenye screen ya simu.

Unatoka mwanzo wa safari mpaka unafika huinui uso wako wala kufungua kinywa chako ukaonekana ili mkaka akutathmini kama unafaa kwa sura ama maneno yako. Upo kimya kama mhamiaji haramu toka Ethiopia.

Ukifika unapoenda, unaendeleza ubize kwenye simu.

Unatoka na marafiki zako wa kike kwenda maeneo ya starehe ukifika huko badala ya kuizungusha sura yako ionekane na wakaka, ama ukarusha kicheko na kuonesha meno yako upo bize tu na simu.

Unaenda harusini, ama kwenye send off party ukifika ukumbini uso unauelekeza kwenye simu.

Kufumba na kufumbua umri unagonga 35 na unaanza kupewa majina ya ajabu ajabu kama kiporo, makombo n.k.

Hapo sasa ndiyo unaanza kustuka na kuamua kuoa badala ya kuolewa. Unamganda mwanaume akuoe mpaka unajilipia mahari mwenyewe.

Hivyo wito wangu kwenu mashosti zangu tupunguze matumizi ya simu. Simu itumie ukiwa peke yako nyumbani kwako. Ili wenye kukuona wakuone.

Tabasamu na kila mtu.
 
Alikwambia anataka kutathmiwa? Ukute anaemueka mjini ndo anamkeep buzy na hiyo simu... Sio kila mwanamke anataka kutongozwa...
 
Back
Top Bottom