Ukiwa kiongozi usiwe mbea, umbea utakuondolea heshima na uaminifu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Uongozi ni dhamana inayokwenda na uaminifu wa pesa, na utu wa una waongoza. Watu wanapofikwa na majanga watakutaarifu ili uchukue hatua mbadala majukumu yasiyumbe na kazi kuharibika.

Kuna watakao kueleza shida zao za kifedha, Kuna watakaoomba msaada wa siku kadhaa bila majukumu Kwa Sababu za kifamilia na kwa kusisitiza umuhimu wa tatizo ataweka picha halisi mezani.

Kunawale kichwapazi akishakunywa bia mbili anaongelea yale aliyoambiwa kutokana na majukumu yake ya uongozi. Wengine hupeleka habari kwa mahasimu wa wale waliowaamini.

Ni kheri upoteze pesa kuliko kupoteza heshima katika jamii. Heshima hainunuliwi dukani bali hutunukwa kutokana na matendo.
 
Back
Top Bottom