April26
JF-Expert Member
- Jul 14, 2020
- 1,403
- 2,119
Habari wana MMU.
Bila shaka sitakuwa nje ya content ya jukwaa nikisema mahusiano yangu na baba mzazi wangu wakati niko teen's ages yalinifanya niishi kwa wasiwasi sana nikijuwa nanyimwa haki na sipendwi na mzazi wangu hasa wa kiume.
Nakumbuka nilikuwa nishamaliza darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 15 siku moja nikaenda disco vumbi, kama kawaida kule kijijini kabla ya siku ya harusi huwa kuna siku kadhaa za burudani, hivo nikaamua kwa mara ya kwanza kushiriki na mimi hili kwanja nililokuwa nasimuliwa tu na wenzangu maana mimi mzee alikuwa hataki kabisa niende pamoja na matukio alioona yeye kama.mzazi sio size yangu.
Nikaondoka usiku huo bhana, ile narudi mida ya saa 6 usiku nanyata ile bila kishindo, nikashika kitochi (kurunzi) changu namlika hadi kitandani naona hakuna godoro...duuuh.
Akili ikaruka,,,nikawaza nimeibiwa au !!! Kwa kuwa nilikuwa na wadogo zangu rooms nyingine nikawaamsha kuuliza nao wakashangaa!!
Kama ndani ya dakika 3 hivi mzee akaingia ndani,,,mbona nasikia kelele? Hamjalala tu? Mara akatupa jicho chumbani kwangu na akauliza godoro liko wapi. April26 kidogo mkojo upite maana mzee alikuwa mkoloni mweuzi kwa kichapo. Nikajuwa hapa lazima nilambe dadekii.
Nikajifanya namdanganya, baba nimetoka nje kujisaidia narudi nakuta godoro hamna, akauliza ,,,umetumia masaa mangapi kujisaidia,,,?? Mimi kimya.... Kumbe bhana keshaandaa na fimbo mbili kali hatari palepale nikaanza kukichezea kichapo!!
Kula stick kula fimbo kula ukuni hadi nikawa hoi.....aiseee.....mzee akasema ole wako siku nyingine urudie uone.
Kumbe bhana alikuja ndani hajanikuta akaamua kubeba na kupeleka ndani kwake na akawapiga bit madogo nikiuliza wajifanye hawajui....!!! Alisoma chezo tangu naondoka aliniona akanipotezea tu.
Baadae akanambia nenda fata godoro pale ,,,pumbavu wewe na iwe mwisho
Wakuu nilikaa kwa muda kama miezi 3 nikiwa kama mgonjwa wa akili,,,si unajuwa age hizo ndo za ku-question sheria,,,, why nipigwe mbona baba wa fulani hawapigi wanae na wengine nawazidi umri lakini wanaenda disco???
Basi bhana sikuwa na jinsi ikabidi nifate sheria. Nashukuru malezi yake yamenisaidia sana hadi sasa najibunia. Mzee wangu baba April26 nakutakia kila la kheri mzee wangu, msalimie na mama yangu. Amina.
EBU SEMA NA WEWE JAMBO GANI UNAAMINI KWA SASA HAPO ZAMANI ULIKUWA WRONG LAKINI ULIVOADHIBIWA ULIMIND SANA MZAZI WAKO.