Ukiwa in teen ages tukio gani mzazi alikufanyia ukaona umeonewa na ukamchukia?

April26

JF-Expert Member
Jul 14, 2020
1,403
2,117
Habari wana MMU.

Bila shaka sitakuwa nje ya content ya jukwaa nikisema mahusiano yangu na baba mzazi wangu wakati niko teen's ages yalinifanya niishi kwa wasiwasi sana nikijuwa nanyimwa haki na sipendwi na mzazi wangu hasa wa kiume.

Nakumbuka nilikuwa nishamaliza darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 15 siku moja nikaenda disco vumbi, kama kawaida kule kijijini kabla ya siku ya harusi huwa kuna siku kadhaa za burudani, hivo nikaamua kwa mara ya kwanza kushiriki na mimi hili kwanja nililokuwa nasimuliwa tu na wenzangu maana mimi mzee alikuwa hataki kabisa niende pamoja na matukio alioona yeye kama.mzazi sio size yangu.

Nikaondoka usiku huo bhana, ile narudi mida ya saa 6 usiku nanyata ile bila kishindo, nikashika kitochi (kurunzi) changu namlika hadi kitandani naona hakuna godoro...duuuh.

Akili ikaruka,,,nikawaza nimeibiwa au !!! Kwa kuwa nilikuwa na wadogo zangu rooms nyingine nikawaamsha kuuliza nao wakashangaa!!

Kama ndani ya dakika 3 hivi mzee akaingia ndani,,,mbona nasikia kelele? Hamjalala tu? Mara akatupa jicho chumbani kwangu na akauliza godoro liko wapi. April26 kidogo mkojo upite maana mzee alikuwa mkoloni mweuzi kwa kichapo. Nikajuwa hapa lazima nilambe dadekii.

Nikajifanya namdanganya, baba nimetoka nje kujisaidia narudi nakuta godoro hamna, akauliza ,,,umetumia masaa mangapi kujisaidia,,,?? Mimi kimya.... Kumbe bhana keshaandaa na fimbo mbili kali hatari palepale nikaanza kukichezea kichapo!!

Kula stick kula fimbo kula ukuni hadi nikawa hoi.....aiseee.....mzee akasema ole wako siku nyingine urudie uone.

Kumbe bhana alikuja ndani hajanikuta akaamua kubeba na kupeleka ndani kwake na akawapiga bit madogo nikiuliza wajifanye hawajui....!!! Alisoma chezo tangu naondoka aliniona akanipotezea tu.

Baadae akanambia nenda fata godoro pale ,,,pumbavu wewe na iwe mwisho

Wakuu nilikaa kwa muda kama miezi 3 nikiwa kama mgonjwa wa akili,,,si unajuwa age hizo ndo za ku-question sheria,,,, why nipigwe mbona baba wa fulani hawapigi wanae na wengine nawazidi umri lakini wanaenda disco???

Basi bhana sikuwa na jinsi ikabidi nifate sheria. Nashukuru malezi yake yamenisaidia sana hadi sasa najibunia. Mzee wangu baba April26 nakutakia kila la kheri mzee wangu, msalimie na mama yangu. Amina.

EBU SEMA NA WEWE JAMBO GANI UNAAMINI KWA SASA HAPO ZAMANI ULIKUWA WRONG LAKINI ULIVOADHIBIWA ULIMIND SANA MZAZI WAKO.
 
Dahh tamu kitambo, aisee mm kuingia geto, nikiwa naanza kidato cha kwanza, shule ya day, mzee kakaza kindakindaki, halaf huwa napitia kwa mama had ujumbe umfikie nouma sana, kuchezea vichapo ukikutana nanvyo n kama nyampala, ila sahv n kama washkaji
 
dahh tamu kitambo, aisee mm kuingia geto, nikiwa naanza kidato cha kwanza, shule ya day, mzee kakaza kindakindaki, halaf huwa napitia kwa mama had ujumbe umfikie nouma sana, kuchezea vichapo ukikutana nanvyo n kama nyampala, ila sahv n kama washkaji
Daah ila unaonaje kwa sasa alikuwa sahihi au kuna mahala alikosea mzee japo wazee hawakosei.
 
Hongera sana na wazazi wako wabarikiwe.

Amen mkuu unajua kuna ile age kila mzazi anachofanya kwako kwa faida yako unaona kama kero. Mama alikuwa akiniambia ukweli utakutana nao pale mbele kwenye kona hakuna haja ya kuharakia mambo japo kuna mengine bado niliyaforce kwa siri na yakawa lakin baadae nilikuja kujua kuwa hayakuwa na faida yeyote kwangu.
 
Amen mkuu unajua kuna ile age kila mzazi anachofanya kwako kwa faida yako unaona kama kero. Mama alikuwa akiniambia ukweli utakutana nao pale mbele kwenye kona hakuna haja ya kuharakia mambo japo kuna mengine bado niliyaforce kwa siri na yakawa lakin baadae nilikuja kujua kuwa hayakuwa na faida yeyote kwangu.
Kweli kabisa, kuhusu kisa changu nilicho andika niliumia sana ila baadae nilizoea tu kuwa sio lazima niende disco. Hii imenijenga hata sasa sishobokei sana issue za mitoko isiyokuwa na faida.
 
alikuwa yupo sahihi, koz hata nikijiangalia, ndo niliongeza juhudi, kuliko ile ya primary
Fresh kabisa. Teens inachangamoto sana.

Sema pia kutofanya baadhi ya mambo utotoni (unfullfilled activities) husababisha mtu aje kuyafanya ukubwani na sana huwa na madhara (we call it libido).

Mfano kama hukunyonya vizuri ziwa au ulikatishwa kunyonya unaweza jikuta ukubwani ndo wale wa kung'ata kalamu.

So far tunapolea watoto wetu pia tuangalie na yaliyo size yao tuwaruhusu kwa tahadhari.
 
Alinizuia kujifunza mchezo wa ngumi (Boxing) yaani kipindi hiko ilikuwa ni trending kwa teenagers waliokulia mitaa ya Mburahati na Magomeni.

Kuna siku nilitoroka asubuhi alfajiri kwenda kupasha pasha uwanja wa KIFA aisee nilivyo rudi kile kipigo nilichopigwa sitasahau ilibidi majirani waingilie.
 
Kweli kabisa, kuhusu kisa changu nilicho andika niliumia sana ila baadae nilizoea tu kuwa sio lazima niende disco. Hii imenijenga hata sasa sishobokei sana issue za mitoko isiyokuwa na faida.

Mimi nakumbuka simu ilikuwa vita kubwa sana uzuri hela ilikuwepo nikinyang’anywa leo kesho nna nyingine mpya, ilifikia stage siwezi kusoma bila simu pembeni(inanikeep active kwa kuchat) vinginevyo nusu saa nying sana nakua nshasinzia mda . Kwa mwenendo huo muda wa kuchat na kudeal na simu unakuwa mwingi zaid ya kusoma.

Hapo bado sijagusia nayoyachat ndio ujinga mtupu imagine unasoma ukiitwa unashindwa kwenda on time kisa mnara unasoma 4G. Hapo hakuna kusoma ni kujidanganya na kuigiza kama unasoma.
 
Alinizuia kujifunza mchezo wa ngumi (Boxing) yaani kipindi hiko ilikuwa ni trending kwa teenagers waliokulia mitaa ya Mburahati na Magomeni.

Kuna siku nilitoroka asubuhi alfajiri kwenda kupasha pasha uwanja wa KIFA aisee nilivyo rudi kile kipigo nilichopigwa sitasahau ilibidi majirani waingilie.
Duuh pole mkuu sasa ndoto yako inaishi au ilikufa kabisa.
 
Mimi nakumbuka simu ilikuwa vita kubwa sana uzuri hela ilikuwepo nikinyang’anywa leo kesho nna nyingine mpya, ilifikia stage siwezi kusoma bila simu pembeni(inanikeep active kwa kuchat) vinginevyo nusu saa nying sana nakua nshasinzia mda . Kwa mwenendo huo muda wa kuchat na kudeal na simu unakuwa mwingi zaid ya kusoma. Hapo bado sijagusia nayoyachat ndio ujinga mtupu imagine unasoma ukiitwa unashindwa kwenda on time kisa mnara unasoma 4G. Hapo hakuna kusoma ni kujidanganya na kuigiza kama unasoma.
Hahahha aisee hatari sana.
 
Kunipiga saaanaaa kila nikiongozana na wanafunzi wenzangu wa kiume, na kila mwanafunzi wa kiume atayejaribu kuongozana nami ikitokea ameonwa na mzazi wangu au kaka yangu nae anapigwa.

Kupigwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa, ilifika sehemu nikawa wakiongea nawasikiliza wanipige wamalize.

Ila walinisababishia niingie kwenye mahusiano mapema as niwe na sehemu ya kujifariji.
 
Back
Top Bottom