Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,117
- 4,764
Takriban kila kona, wafuasi wa vyama vya upinzani wamepokea kwa furaha kubwa kauli ya Nape kuwa "hakuna CCM imara bila upinzani."
Kauli hiyo inamfanya Nape kuonekana shujaa machoni mwa wafuasi hao wa upinzani. Sio shujaa kwa sababu yupo sahihi au amejitoa mhanga bali tu kwa vile amesema kitu ambacho wafuasi hao wa upinzani wanataka kusikia.
Kuna siku niliona picha inasambaa huko Twitter ya Fatma Karume na Kigwangallah, na watu wakamwaga pongezi lukuki kuwa huo ni ushuhuda kwamba "siasa si uadui."
Back to Nape: mtu akijisumbua kidogo tu ku-Google "Nape Chadema" au "Nape Upinzani/Wapinzani" atakumbana na kauli hatari kabisa kutoka kwa mwanasiasa huyo, ambaye pamoja na mwenzie Mwigulu Nchemba walisimama kidete huko nyuma kujenga hoja kuwa "Chadema ni chama cha kigaidi."
Nape asema CHADEMA ni chama cha Kigaidi - JamiiForums
Hiyo kauli yenyewe ya "hakuna CCM imara... " tu ina walakini. Kwamba la muhimu si uwepo wa Upinzani kwa maslahi ya Watanzania bali uimara wa CCM.
Ofkoz, kila mtu ana haki na uhuru kuamini hadaa lakini ni vema kukumbuka busara za Baba wa Taifa kuwa "Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu, ukalikubali atakudharau" (01/05/1995)
[Na credit where due, Nape anastahili pongezi kwani tangu atumbuliwe na Jiwe ametokea kuwa kipenzi wa wafuasi wa upinzani kwa kuwalisha sweet political rhetoric zinazopokelewa kwa shangwe na kumfanya aonekane shujaa of sort...]
Sent using Jamii Forums mobile app