Ukitaka kuwaghilibu Watanzania, ongea wanachotaka kusikia

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,764
Takriban kila kona, wafuasi wa vyama vya upinzani wamepokea kwa furaha kubwa kauli ya Nape kuwa "hakuna CCM imara bila upinzani."

Kauli hiyo inamfanya Nape kuonekana shujaa machoni mwa wafuasi hao wa upinzani. Sio shujaa kwa sababu yupo sahihi au amejitoa mhanga bali tu kwa vile amesema kitu ambacho wafuasi hao wa upinzani wanataka kusikia.

Kuna siku niliona picha inasambaa huko Twitter ya Fatma Karume na Kigwangallah, na watu wakamwaga pongezi lukuki kuwa huo ni ushuhuda kwamba "siasa si uadui."



Back to Nape: mtu akijisumbua kidogo tu ku-Google "Nape Chadema" au "Nape Upinzani/Wapinzani" atakumbana na kauli hatari kabisa kutoka kwa mwanasiasa huyo, ambaye pamoja na mwenzie Mwigulu Nchemba walisimama kidete huko nyuma kujenga hoja kuwa "Chadema ni chama cha kigaidi."

Nape asema CHADEMA ni chama cha Kigaidi - JamiiForums

Hiyo kauli yenyewe ya "hakuna CCM imara... " tu ina walakini. Kwamba la muhimu si uwepo wa Upinzani kwa maslahi ya Watanzania bali uimara wa CCM.

Ofkoz, kila mtu ana haki na uhuru kuamini hadaa lakini ni vema kukumbuka busara za Baba wa Taifa kuwa "Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu, ukalikubali atakudharau" (01/05/1995)

[Na credit where due, Nape anastahili pongezi kwani tangu atumbuliwe na Jiwe ametokea kuwa kipenzi wa wafuasi wa upinzani kwa kuwalisha sweet political rhetoric zinazopokelewa kwa shangwe na kumfanya aonekane shujaa of sort...]

Screenshot_20190219-132739_Facebook.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
We ni mamluki huna kipya.
Kauli ya Nape sio ya kipumbavu hata kidogo.
 
Nape sio mtu wa kumuamini na wapinzani hatutakiwi kumuona ni mwenzetu.

Anayoyaongea sasa ni matokeo ya "kutoswa" kwake

Swali angekuwa hajatoswa angeongea hayo? Au kwa mfano ateuliwe tena na "jiwe" mnazani atakuwa upande wa nani?
 
Nape sio mtu wa kumuamini na wapinzani hatutakiwi kumuona ni mwenzetu.

Anayoyaongea sasa ni matokeo ya "kutoswa" kwake

Swali angekuwa hajatoswa angeongea hayo? Au kwa mfano ateuliwe tena na "jiwe" mnazani atakuwa upande wa nani?
Huyu si wa kuamini hata kidogo.
 
Inaonekana unabeba maneno ya baadhi ya wachangiaji humu jukwaani kisha unafanya ndio msimamo wa upinzani. Huyo Nape sio mara moja au anaambiwa amebadilika na kujifanya mtakatifu baada ya kukosa madaraka. Ni kweli haongei kauli za kuwakwaza wapinzani kama zamani, lakini haimaanishi ndio anakubalika na wapinzani.
 
Inaonekana unabeba maneno ya baadhi ya wachangiaji humu jukwaani kisha unafanya ndio msimamo wa upinzani. Huyo Nape sio mara moja au anaambiwa amebadilika na kujifanya mtakatifu baada ya kukosa madaraka. Ni kweli haongei kauli za kuwakwaza wapinzani kama zamani, lakini haimaanishi ndio anakubalika na wapinzani.
Asante Tindo...angalia post#6
 
Liko wapi tamko rasmi la upinzani likiunga mkono kauli ya Nape?

Tangu lini Nape akawa mtu wa kuaminika?

Nataka nikuambie kitu kimoja watanzania siyo wajinga kiasi hicho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli na ni Dhahiri TUFANI Ya lisu yaja

Hofu imetanda kutokana na mengi

-Ufisadi 1.5 Trillion
- Mafao ya wastaasfu kuporwa

-Kufyweka Fao la kujitoa

- Wakulima kunyanyaswa - 2016 Suala la Sukari, ikapanda kutoka 1600 hadi 2400-- ilikuwa katazo kuuza Mahindi nje, mwaka 2017...Ikaja Mbaazi..2018 na sasa ni Korosho

- Hakuna ajira mpya tangu mwaka 2015...Kilio kipo kila nyumba.wengine wanalala sebuleni kwa Shemeji, mjomba n.k

- Wafanyakazi hawajaongezewa mishahara wala madaraja

-Uchumi kuporomoka --shs dorooo

- Bomoa boma

Kodi ya kichwa/machinga

Kuvamia bureau de change na jeshi

Wao wanapamba kwa sifa za kijinga za SGR, Stiglers na Bombadier
 
Back
Top Bottom