Ukitaka Kujua ni Jinsi Gani na Kiasi Gani WaZanzibari Wanautaka na Kuufaidi Muungano

Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
7,663
8,809
Leo hii waletee habari ya kuuvunja huo Muungano.

Akina Jussa wanajirusharusha huko pembeni wakicheza sinema chovu, lakini husikii wakihimiza Muungano uvunjwe.

Kama paliwahi kutokea fursa nzuri ya kuuvunja huu Muungano, , hapajawahi kuwa kama ilivyo sasa, wakati ambapo mZanzibari yupo madarakani kama rais wa nchi, na huko ndani ya Chama Cha CCM kukiwa hakuna mtu yeyote mwenye ushawishi wa hoja juu ya kuuendeleza Muungano uliopo.

Leo hii Zanzibar wakisema hawataki Muungano, hakuna atakayepinga uamzi huo tokea huu upande wa Tanganyika.

Kwa hiyo, muungano huu upo na utaendelea kuwepo kwa vile waZanzibari hawaupingi tena; kwa sababu umekwishaonyesha kuwa una manufaa makubwa kwao.

Kwa sababu nisizoweza kuzielezea hapa, Tanganyika hawawezi kuuvunja Muungano. Wanacholilia wao ni kuipata Tanganyika tu iliyomezwa ndani ya Muungano, basi!
 
hakuna faida ya muungano
Usiseme hivyo mkuu, kama wewe hufaidiki nao, kuna watu wanafaidika sana kwa kuwepo Muungano. Kwa sasa hivi, hata wale waliokuwa wanapiga kelele sana huko siku za nyuma kuhusu Muungano, tokea Zanzibar, nao kwa sasa hivi ni wanufaika wakubwa sana wa Muungano huo.
 
Dk90 zimekwisha, zimeingezwa 5
3 zimekwenda bado dk 2 tu
Tanganyika 0 - 3 Zanzibar
Hapa una maana kwamba, ili Tanganyika, angalau asawazishe, inambidi afunge goli kila baada ya sekunde 40!

Hii hujaruhusu mpira kuokotwa toka golini na kuufikisha katikati mchezo uanze tena!.

Kwa hakika Tanganyika shalazwa, hakuna njia tena.
 
Ila sasa kuna HASARA ya "Muungano" kwa Tanganyika.

Kiukweli hasara ni kubwa sana kwa Tanganyika kuliko faida.

Nafikiri nia ya SSH ni kuuvunja kwa style yake hii. Kuuza kila assets za Tanganyika, kupendelea Zanzibar katika pesa, teuzi,mikopo, nafasi mbalimbali, kuigawa na kuivuruga Tanganyika kidini, kikanda nk halafu ataondoka zake kwenda huko kwa wajomba zake baadaye muungano ukishavunjika anarudi nyumbani Zanzibar.
 
Huu Muungano ukivunjika, na ccm nayo kwishney!
hahahahaaaaa....

Hebu tueleze, Muungano unaisaidiaje CCM kubaki madarakani ?

Kwa mawazo yangu mimi, Muungano ukifa CCM ita revert back to TANU na kupata nafasi ya kuji rebrand kama chama cha ukombozi, chama cha masikini wa colonial Tanganyika... potentially a powerful vote getter.

A penny for your thoughts.
 
Hao jamaa wamejaa unafiki tu,kama vipi waitishe kura ya maoni.

Top politicians wa huko wana makazi au uwekezaji kama si Dar basi ni Tanga wengine hadi Dodoma.
 
Huu Muungano ukivunjika, na ccm nayo kwishney!
Kama usemavyo ndivyo, basi tuna safari ndefu sana, kwa sababu tuliowategemea wauvunje Muungano, sasa ndio wasiotaka kabisa kusikia hiyo habari.
Kwa maana yako ni kwamba tutakuwa nao CCM kwa muda mrefu sana.

Matumaini tuliyokwishayaweka kwa CHADEMA na yenyewe yanazidi kuwa hafifu sana. Hatujui Mbowe alirogwa na Samia kwa uchawi toka wapi, maanake hatujapata kuuona ukitumika ndani ya nchi hii tokea tuwe nchi huru.

Mbowe anajiapiza ataendelea na majadiliano ya Maridhiano, sijui wanaridhiana juu ya jambo gani tena!

Kwa hiyo CCM ipo palepale, haiendi popote.
 
hakuna faida ya muungano
Umasema Muungano hauna faida!! Mwulize Mbarawa kama amewahi kufanya biashara yoyote ile ikampa faida kubwa kama hii ya kuuza bandari za Tanganyika. Bila.Muungano, angepata wapi uwezo wa kuuza bandari za Tanganyika?
 
Yakhe wataka muungano uvunjike kwa nini Yakhe?
Hapana, sijataka hivyo; ninachosema tu ni kuwa waZanzibari hawataki tena Muungano uvunjike.
Kuna wakati, hasa lile kundi la akina Jussa na OMO, ilikuwa siku haipiti bila kusikia wakiimba wimbo wa kuuvunja Muungano.
Sasa hivi huwasikii tena wakiimba wimbo huo. Bila shaka Samia kawapa dawa ya kuuponya ule uhayawani uliokuwa umewaingia hao watu.
 
Muungano wa kipuuzi kabisa kuwahi kutokea duniani.yaani zanzibar inakuwa na eneo lake ndani ya Tanganyika(razaba) halafu watu wanachekelea upuuzi mtupu.
 
Muungano wa kipuuzi kabisa kuwahi kutokea duniani.yaani zanzibar inakuwa na eneo lake ndani ya Tanganyika(razaba) halafu watu wanachekelea upuuzi mtupu.
Hilo la "watu kuchekelea" hata mimi linanishangaza na kunitatiza sana.

Paliwahi kuwepo kundi la wabunge Bungeni, nadhani lilifahamika kwa jina la G55 (?), sikumbuki vizuri.

Hilo kundi la akina Njeru Kasaka lingeibuka leo hii, sijui hali ingekuwaje?

Badala yake, leo hii tunao akina Msukuma. Maajabu makubwa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom