Muungano wa Tanganyika na Zanzibar; Una Faida gani na kwa manufaa ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar; Una Faida gani na kwa manufaa ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Apr 14, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Imekuwa ni jadi na utamaduni kufurahia sikukuu hii na kuwaenzi waasisi wa Muungano wetu Mwalimu Nyerere na Mzee Abeid Karume kwa matamasha, gwaride na shangwe kebekebe.

  Lakini imekuwa ni dhambi, tena yenye sumu kali kwa mtu yeyote kuhoji au kutaka kuuchambua Muungano huu.

  Lengo lango si kuuliza historia au kudadisi uhalali wa Muungano wa Tanzania bali ni faida zake na manufaa yake kutokana na mfumo wa Muungano kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, mamlaka zilizoko kama vile Mahakama, Bunge, Baraza la Wawakilishi na ni vitu gani ambavyo ni kwa ajili ya Muungano na vipi si kwa ajili ya Muungano.

  Je, kwa nini tuliweka vipengele fulani viwe masuala ya muungano na vingine visiwe?

  Je, Muungano huu una maana gani ikiwa vipengele ilivyoko vinakingana na azma kuu ya kuunda Taifa lenye nguvu na umoja?

  Je, Wananchi wa Tanzania, wananufaika vipi na Muungano huu na wanaathirika vipi kutokana na Muungano huu na mfumo wake?

  Je, kuna haja ya kuupitia Muungano na ama kupengua vipengele fulani au kuunganisha kila kitu na kuwa na sura moja bila kutofautisha ya hili la Watanganyika au Watanzania Bara na lile ni la Wazanzibari?
   
 2. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  MI NAONA YALIKUWA YA KALE NA SASA HATUNA FAIDA KABISAAAAAAAAAAAAAA!

  Tuliambiwa kuwa Tz ina mikoa 25 yaani 20 bara na mitano visiwani. hili jambo siku hizi halisikiki, nadhani mkoa wa Manyara ulisha ongezeka. Labda tukumbushane kwa sasa Tz ina mikoa mingapi. Ila nachojua mambo ya mikoa kwa Zz sio deal make
  • Wana wimbo wa taifa
  • Wana bendera yao
  • Wana Jeshi
  Nashindwa kujua, kwanini tunaendelea kudanganyika wakati mambo yamebadilika bila kutuhusisha sisi wadau?
  Ninachojua wameamua kufaidi mambo ya muungano wakati ya kwao wanakula wenyewe. Subiri baada ya uchaguzi ndo utasikia Mbunge wa ... ameshinda kwa kura 36 kati ya kura 40 zilizo pigwa. kwanini uwakilishi usiwe sawia na ule wa Tz bara?
  Kweli twaliwa kwa muungano. Mie siu-mind kabisa.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nyange,

  Unaposema
  je unamaanisha nani?
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Muungano una faida zake na nyingi zimekwishapatikana na kuonekana

  Muungano una matatizo yake mengine yanajulikana na yanawezekana kumalizwa

  Muungano upelekwa kwa wenye nchi, mkataba uchunguzwe upya kwa maslahi ya pande mbili

  wakati ni huu,
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Tunahitaji kutafakari sana kwa hili, Mzee wetu aliwahi kusema kuwa muungano umesaidia usalama kwa bara.
  Kwa sasa jama hawa mamwinyi wana kila kitu chao kuanzia bendera, wimbo, rais, na mambo mengine mengi. In Short if we were to vote today then i would vote for a big NO. na sitabadili huu msimamo. Tuachane nao tu manake maandamano kibao hasa ule ugonvi wa deposits za mafuta yalogunduliwa. Katika bajeti ya taifa nadhani wanapata mgao mara mbili kutoka muunganoni na mapinduzini!
   
 6. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Wanashindwa kutafakari huu muungano, waulize huo wa EAC itakuwaje? Nchi hii inaongozwa na vilaza yaani hawafahamu 1+1=2 or more.
   
 7. T

  Tall JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  faida za muungano zipo nyingi sana kuliko hasara.siku zote umoja ni nguvu. Lakini hatuwezi kuona faida kubwa za muungano hadi kwa bahati mbaya tutengane, wajerumani ukiwauliza leo watakwambia faida nyingi sana za muungano .sikatai kuna baadhi ya viongozi wetu hawasimamii ipasavyo mambo ya muungano na baadhi ya vipengele vya muungano vyahitaji kurekebishwa.haya ni mawazo yangu binafsi.
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jamii Forums,

  Inaukuwaje mnakuwa na majibu kama Amos Makala au John Chiligati kama si William Lukuvi? Majibu yasiyo na hoja wala kujenga hoja, bali ni majibu alimradi umejibu?

  Kama kuna Faida, zitaje hizo faida kwa kina si kusema kuna faida nyingi sana, maana kama kuna faida nyingi sana, kwa nini mpaka leo hii kuna kero za muungano na hakuna mwenye kuthubutu kuzifanyia kazi?
   
 9. T

  Tom JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Muungano umejengwa asilimia mia moja kwa msingi wa serikali MBILI ZA CCM, lakini toka lini CCM ikawa na ufanisi wa mambo ya wananchi. CCM yenyewe imejengwa ktk misingi ya ubinafsi, ufisadi na ubabaishaji. Muungano haiwekani ukawa mzuri chini CCM, labda ondoa hiyo kitu CCM. Hata ukaunganisha ikawa nchi moja na serikali moja badala ya ilivyo sasa nchi moja na serikali mbili, bado choko choko toka wanaCCM wa mkoa wa UNGUJA NA PEMBA hazitakoma.
   
 10. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Baada ya Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri yetu kutamka bayana katika Bunge kuwa Zanzibar sio nchi, kulikuwa na mjadala mkali kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu usahihi wa kauli yake hiyo.

  Wako watu wengi walioona kuwa kauli ya Mheshimiwa wetu huyu aliyoitamka mbele ya kadamnasi ya waheshimiwa wenzake ni sahihi kwa misingi ya katiba zetu. Aidha kumekuwa na watu wengine, wakiwamo baadhi ya Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, waliyoyatizama mambo kwa upande wa pili wa sarafu. Kwao wao hawa, Zanzibar ni nchi kamili na kamwe haiwezi kusemwa vyenginevyo. Kila moja ya makundi haya limekuwa na sababu zake ambazo baadhi zimetolewa kwa hoja zenye mashiko na nyengine zimekuwa ni hoja za kibubusa ambazo hazina mashiko yoyote ya kielimu zaidi ya kutolewa kwa misingi ya ushabiki au jazba. Kwa maoni ya Wazanzibari waliowengi, hata Rais Kikwete hakuongeza jipya lolote pale alipolihutubia bunge na kuzungumzia kadhia hii zaidi ya kuongeza petroli katika moto unaowaka au kupigilia msumari katika kidonda kibichi kinachovuja damu!

  Vyovyote iwavyo, Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatamka bayana kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, Katiba hii haikutamka hili kwa bahati mbaya au kwa kukosewa kama baadhi ya watu wanavyoamini. Katiba hii imetungwa; na walioiandika walijua lengo lao tangu mwanzo wa uandishi wao na walihakikisha wanalikamilisha. Ikitathminiwa tangu awali inaweza kubainika wazi kuwa hakukuwa na nia njema kutoka upande wa Tanganyika katika kuunda na kuuendeleza Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar.

  Mwalimu Nyerere mwenyewe katika miaka ya mwisho wa 1950 aliwahi kunukuliwa akisema kuwa lau angeweza kuvisukuma nje ya bahari ya hindi visiwa vya Zanzibar basi angefanya hivyo kwa jinsi vinavyomkera na asivyopenda kuviona vinastawi na kunawiri (Smith, William E. 1973 uk 121). Kwa vile ni dhahiri kuwa asingeweza kutekeleza kusudio lake hilo, ndipo alipotafuta kila mbinu ili angalau basi Zanzibar isiwe nchi huru yenye mamlaka yake inayojitegemea. Katika kukamilisha azma yake hiyo, ndipo alipobuni mpango wa kuifanya Zanzibar kuwa ni sehemu ya Tanganyika chini ya kitambaa cha Muungano. Kwa bahati mbaya sana Mzee Karume kwa wakati ule hakuweza kung'amua haraka nia mbaya hii ya Tanganyika na viongozi wake kwa Zanzibar na hivyo akajikuta anacheza ngoma asiyoitambua kwa kuiweka rehani Zanzibar na maslahi yake .

  Watu wanaweza kushangaa ni kwa vipi Mwalimu Nyerere, kiongozi anayeonekana 'mtakatifu' mbele ya macho ya baadhi ya watanganyika asemwe kuwa hakuwa na nia njema na Zanzibar hasa pale suala la muungano linapohusika. Ukweli huu unadhihirika wazi iwapo itatathminiwa ushiriki wa Nyerere tangu mwanzo wa harakati za muungano hadi pale alipofariki. Historia inajionyesha wazi kuwa kabla ya Muungano Zanzibar ilikuwa ni nchi inayojitegemea na yenye mamlaka yake kamili ' independent and sovereign state'.

  Makubaliano ya Muungano ‘Articles of Union' yaliyosainiwa mwaka 1964 ni mkataba wa kimataifa ‘international treaty' unaotambuliwa na Vienna Convention on the Law of Treaties. Makubaliano hayo ya Muungano yalikuwa juu ya mambo kumi na moja tu ambayo ndiyo yaliyokubaliwa kuwa mambo ya muungano. Mihimili ya utendaji na kutunga sheria ya Zanzibar (Zanzibar Executive and Legislature) ilikosa mamlaka ya kisheria juu ya mambo hayo kumi na moja tu. Nje ya mambo yale kumi na moja Zanzibar ilikuwa na mamlaka yake kamili ya kusimamia na kushughulikia mambo yote mengineyo. Hii ndiyo sababu Makubaliano ya Muungano yalibakisha separate executive and legislature kwa Zanzibar zilizotakiwa kuundwa kwa mujibu wa sheria za Zanzibar na ambazo zina mamlaka ya kusimamia na kushughulikia mambo yote ambayo si ya muungano kwa Zanzibar. Mambo haya yanamaanisha kuwa Makubaliano ya Muungano yamebakisha kiwango fulani cha utaifa ‘sovereignty' kwa Zanzibar juu ya mambo yake yote yasiyo ya muungano.

  Mashaka yote katika Muungano huu unaoweza kufananishwa na muungano wa paka na panya yameanzia katika Sheria ya Muungano yaani 'Acts of Union, No. 22 of 1964'. Ikilenga kuridhia na kurasimisha Makubaliano ya Muungano, Sheria hiyo ya Muungano ilitoa mwanya wa kuvurugwa Muungano na kuonewa aliye dhaifu na mdogo. Kwa hakika Sheria hii imeweka jiwe la msingi kwa mipasuko yote ya kikatiba iliyofuatia katika muungano wetu. Ni sheria hii ndiyo iliyodhihirisha bayana nia mbaya ya Tanganyika na viongozi wake kwa mustakabali wa Zanzibar. Sikusudii kuonyesha kila jambo lililokwenda kinyume na spiriti ya Makubaliano ya Muungano katika sheria hii.

  Bali kwa mukhtasari, kifungu cha 8 cha sheria hii kwa mfano kilimpa mamlaka Rais wa Jamhuri ya Muungano kupitisha na kutoa ‘Decrees'. Ijapokuwa ni kweli kuwa Ibara (III) ya Makubaliano ya Muungano inaelezea kuwa wakati wa kipindi cha mpito Jamhuri ya Muungano ingeongozwa kwa Katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ili kukidhi matakwa ya Makubaliano ya Muungano lakini kwa vyovyote vile Ibara hii haikumpa madaraka yoyote Rais kupitisha na kutoa Decrees. Rais alikuwa na madaraka kwa mujibu wa Ibara (V) (b) ya Makubaliano ya Muungano kutoa ‘oder' ya kuifanya itumike hadi Zanzibar sheria yoyote iliyohusu jambo la muungano. Haikubaliki kulitafsiri neno ‘order' lililotumika katika Ibara (V)(b) ya Mapatano ya Muungano kumaanisha ‘Decree' hasa kwa vile Decree zilizotolewa na Rais zilikuwa na hadhi ya kikatiba wakati presidential order zingekuwa na hadhi ya azimio la kiutendaji yaani 'executive declaration' tu.

  Kufuatia kifungu 8, Rais wa Jamhuri wa wakati ule (Nyerere) alipitisha Decrees chungu nzima ambazo hazikuwiva pamoja wala kwenda sambamba na makubaliano ya Muungano. Kwa mfano, katika G.N. 245 ya 1964 Nyerere alitoa Decree iliyoitwa Transitional Provisions Decree ambayo iliibatiza Serikali yote ya Tanganyika na kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Athari ya kwanza ya ‘Decree' hii ni kuviza muundo wa shirikisho uliotazamiwa na kukusudiwa na Makubaliano ya Muungano. Lakini pia, kuichanganya Serikali ya Tanganyika ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kumeyachanganya mambo yasiyo ya Muungano ya Tanganyika ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano na, hivyo, kuifanya Tanganyika na Jamhuri ya Muungano kuwa ni pande mbili za sarafu moja!

  Mhimili wa utoaji haki (mahkama) mathalan kamwe haukuingizwa wala kufanywa kuwa ni jambo la muungano (haumo kwenye Makubaliano ya Muungano) na hivyo kuufanya kila upande wa Muungano uwe na mfumo wake wa sheria na mahkama yake iliyo huru kutoka nyenziwe. Bali kutokana na kuchanganywa mambo kimakosa kile kilichopaswa kuwa Mahkama kuu ya Tanganyika sasa kinaitwa Mahkama kuu ya Jamhuri ya Muungano. Hili ni koseo kubwa hasa kwa kuwa kila inapotajwa Mahkama ya Jamhuri ya Muungano katika sheria mbalimbali imekuwa ikitafsiriwa kuwa ni Mahkama ya Tanzania Bara na kwamba Mahkama za Zanzibar hazina mamlaka mlingano au 'concurrent jurisdiction' kushughulikia jambo hilo.

  Mfano uliowazi upo katika kesi ya Jina Khatib Haji v Juma Sleiman Nungu [1986] L.R.C ambapo ilielezwa na Mahkama kuwa kwa vile sheria ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano imeipa mamlaka Mahkama kuu ya Jamhuri ya Muungano kusikiliza petition za uchaguzi hivyo Mahkama kuu ya Zanzibar haina mamlaka ya kusikiliza kesi hizo hata kama itahusu uchaguzi wa wabunge katika majimbo ya Zanzibar!

  Kama kwamba haitoshi, Transitional Provisions Decree pia imeeleza kuwa kila mtu aliyekuwa anashikilia Afisi katika ajira ya Jamhuri ya Tanganyika atahesabika kuwa anashikilia Afisi inayofanana na hiyo katika Jamhuri ya Muungano. Athari ya hili ni kuwa watumishi wote wa Serikali ya Tanganyika wakawa ni watumishi wa Jamhuri ya Muungano hata kama Afisi zao hazihusu mambo ya Muungano. Hata sheria zilizosimamia mambo ya ajira na utumishi serikalini ambazo awali hazikuwa za muungano nazo kinyemela zikawa ni sheria za muungano kwa kuwa utumishi katika serikali ya Jamhuri ya Muungano sasa limepewa hadhi ya kuwa jambo la Muungano.

  Hata Wizara ambazo si za mambo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika nazo sasa zaitwa kuwa Wizara za Jamhuri ya Muungano. Jambo hili limewapa madaraka kwa mlango wa nyuma Mawaziri wanaosimamia Wizara zisizo za Muungano kwa Tanganyika kushughulikia baadhi ya mambo ambayo si ya Muungano hadi Zanzibar! Kwa Mfano Waziri anayeongoza Wizara ambayo si ya Muungano kwa upande wa Tanganyika anapokwenda katika mikutano ya kimataifa kuiwakilisha Tanzania hivi huwa anaiwakilisha Tanganyika au Tanzania nzima ikiwemo Zanzibar. Maana wawapo kule ughaibuni hujinasibu kuwa wao ni Mawaziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa mfano Mimi ni Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Jamhuri ya Muungano wakati mambo hayo siyo katika mambo ya Muungano.

  Halkadhalika, kuosekana kwa Mfuko Mkuu tofauti kwa mambo yasiyo ya muungano kwa Tanganyika nalo limekuwa ni tatizo jengine. Kwa msingi huu, hata tanganyika inapotaka kutumia fedha kwa idara na taasisi zake zisizo za muungano basi fedha hizo hutolewa kutoka katika hazina na Mfuko Mkuu wa Muungano. Jambo hili linaipa Zanzibar unfair advantage kwa kuwa yenyewe hairuhusiwi kutumia fedha kutoka mfuko huu kwa mambo yasiyo ya muungano kwa Zanzibar. Kwa bahati mbaya, fedha zote za ruzuku na misaada zinazokuja kwa jina la Tanzania kutoka nje huhifadhiwa katika mfuko huu ambao Zanzibar hainufaiki nawo na badala yake tanganyika kwa kujifanya wajanja wanazitafuna mara mbili.


  Itaendelea………
   

  Attached Files:

 11. sexologist

  sexologist JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 2,296
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 135
  Waheshimiwa JF..

  Nimekuwa nikifuatilia sana masuala ya muungano.. Nilichogundua ni kwamba viongozi wa Bara ndio wanaong'ang'ania huu Muunguno uendelee kuwepo, pasipo kuwa na faida yoyote kwa wakaz wa bara! Sijaona mznz hata mmoja anayeutaka huu muungano.. Kwa kuthbitisha hlo angalia matukio ya kuchoma maeneo ya biashara wa watu wa bara hko znz..

  Ukiangalia JK amewaweke waznz weng mno kwenye serikali yake (sisemi kwa ubaya) ili kuuridhsha upande wa pili..

  Swali, waznz wanaonyesha vp kwamba wanauhtaji muungano huu?? Je matukio ya kuchoma bar za wabara, serkal imechukua hatua gani?? Je muungano una umuhmu gani, au ni kuendeleza urafiki wa Nyerere na Karume?
   
 12. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF tukiwa kama wananchi wanaohitaji kuchangia hoja nzito na zenye maslahi kwa nchi yetu, tunao wajibu wa kufahamu kwa undani jambo hili kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Kwangu mimi naona Muungano huu ni mzuri kwa malengo yaliyotafsiriwa na waasisi, LAKINI pia ni kiini macho kwa Watanganyika. Kwa sababu:

  1. Zanzibar inatambulikana kimataifa kimichezo kama nchi.
  2. Zanzibar ina Rais, na anaheshimika ndani na nje ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  3. Zanzibar ina Bendera ya Taifa.
  4. Zanzibar ina Wimbo wa Taifa.
  5. Wazanzibar wanavitambulisho kama Wazanzibar na siyo Watanzania.
  6. N.k

  Je, Nchi yetu Watanganyika iko wapi? Haki zetu za uraia kama watanganyika ziko wapi? Nini kifanyike hasa katika mchakato wa Katiba Mpya???

  Je Muungano huu si Kiini macho kwa watanganyika?? Kwanini??
  JE,
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,554
  Trophy Points: 280
  Hata ukiwa na sifa zote hizo ulizozitaja, lakini kama hauna vyombo vya dola vya ulinzi na usalama, wewe sio dola!.
   
 14. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pasco, nakubaliana na wewe lakini hoja yangu inasimamia pale muonekano na mwendelezo wa Wazanzibar katika kujaribu kujenga Taifa lao upya. Karibia haya yote niliyoyataja hapo juu, yamefanywa na Rais mstaafu wa Zanzibar Abeid Aman Karume. Kwa nini tusitarajie mengine kufanywa na hilo " ulinzi na usalama" likiwemo??

  Unakumbuka wakati Karume alisusia kuhudhuria sherehe za Muungano eti kwa kisingizo cha mvua?? Unakumbuka kuwa Mwafaka wa Zanzibar uliaasisiwa na Wazanzibar chini ya Rais wao wakati huo Karume kwa kukaa meza moja na upinzani kwa mazungumzo ya ... kwa nini kugombana huku sote wazanzibar?? Tuungane tutawale pamoja nchi ni yetu sote.... Wamefanikiwa. Kwa nini usifikiri na mengine kujitokeza? Ikiwa hivyo sisi Watanganyika tutabaki tunaitwaje??

  Maana Katiba yao haitutaji!!
   
 15. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu aliwahi kusema wananchi wa Tanzania Bara ni Wadanganyika!! Ukitafakari sana utaona maana iliyojificha. Tatizo tulilo nalo watanzania, hatutaki kuumiza vichwa kufikiri na kubaini kitakachotokea mbeleni kwa kutumia historia za wakati uliopo na uliopita. Hii ni hatari sana.

  Tutaishia kutatua mambo ambayo yasingetufika kama tungeyabaini mapema. Tabia hii ndiyo inatufanya hata sisi wanaJF tusichangie mada kama hizi. Tafadhali njooni tuchangie post hii na pengine mniodolee dukuduku nilizonazo kwa hatma ya Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Watanganyika na Wazanzibar.
   
 16. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Faida ya Muungano ni Wazanzibari kuishi Tanganyika na kumiliki ardhi bila Bughdha
  Kujibebesha mzigo usio wa lazima.
  Muungano ufe hata kesho maisha yataendelea tu.
   
 17. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nijuavyo mimi, Muungano ukifa, Katiba yetu inabadilishwa. Jina la nchi na Muundo wa Serikali lazima vibadilishwe. Kwa maana nyingine, tunabadili usajili wa Jina la Taifa letu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa. Au si hivyo??!!
   
 18. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaona sasa wanadai Baraza lao la Mitihani. Kwani Wizara yao ya Elimu inafanya kazi gani???
   
 19. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,182
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  Mwanangu wee ulie tu!
  zenj sasa ni dola na kiujanja wamekodi vyombo vya dola toka tg kuisimamisha dola kwa gharama ya watg
  Huku wanetu wanakalia mawe na viroba darasani na mkifa kwa kukosa dawa mnazikwa makaburi ya pamoja!
  Jiulize mashujaa wetu kina Mirambo,Kinjeketile,Sina,.....vifo vyao hawakuiba kuku bali waliipigania Tg dhidi ya dhulma ya kutawaliwa.
  Leo kuna mzenj anatutawala kinyemela Bila aibu tunaona sawa tu kweli wadanganyika!
  Haya yanayotokea ni laana na tusipo jitambua mapema tutavuna tunachokipanda
  IDUMU TANGANYIKA!
   
 20. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  naipenda tanzania lakini naikumbuka Tanganyika imenyongwa na kuuwawa! Nadhani serikali 3 ni muhimu saaana!
   
Tags:
Loading...