Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Kwa sisi ambao tumetoa tongotongo za macho.naweza kusema sehemu ya KIGAMBONI ilitakiwa iwe ni sehemu ambayo yenye mvuto mkubwa wa kuishi watu na siajabu ndio ingekuwa sehemu ghali kuishi lkn bahati mbaya kwenye miti hakuna wajenzi.

Tazama hiyo attached pic hapo angalia kwa umakini kisha analyse the location wisely .View attachment 1822546
Kigamboni ukishuka Panton tu unakutana na maeneo skwata ta kufa mtu.

Eneo Kama kigamboni ingebidi iwe Kama Masaki au ostabay ila kwasababu sisi watanzania hatuwezi kupanga Basi ni balaa tupu.
 
Hv kwa mji wa dar ni maeneo gan yaliyo salama kuishi?/ Ambayo hayana vibaka vibaka na wezi? Ukiachilia mbali oSterbay,Upanga,Mbezi,Masaki, na mitaa ya kishua kama hyo. Nazungumzia mitaa ya watu wa kipato cha kati tuh!
Kaishi Magogoni karibu na Ikulu
 
Ukitaka mwisho wako wa Kutembea kutokana na Vibaka na Majambazi kuwa wengi na Kula Kwako Bata ( Kustarehe ) kuwe ni Saa 12 Jioni, basi kaishi Kigamboni.
Afande khamisi kawamaliza sana mkuu kapiga shaba mno majambazi
 
Mimi nimekaa sehemu mbalimbali dar,but kigamboni is the best place hakuna foleni, nyumba zimekaa kwa nafasi Hali nzuri ya hewa n.k nimepanga but next month naanza ujenzi kwenye kiwanja changu kisarawe 2 mwasonga
 
Kigamboni hakuna tofauti na Mbagala, hakuna tofauti na Temeke, hakuna tofauti na Yombo, hakuna tofauti na kiwalani, hakuna tofauti na kongowe.
maeneo hayo yote yanafanana sana
kwa sababu kwa asilimia kubwa yanakaliwa na wakaazi wa mikoa ya kusini.
 
Kinacho nikera Kigamboni ni kuwa kushoto sana na maeneo yote ya Dar.. yani mfano umepata safari ya mkoani inayokubidi ukapande basi Mbezi stand hapo utalazimika kukimbia kimbia asubuhi kama kichaa kuliwahi hilo basi.

Pili kigamboni mambo ya kuvuka maji unalipia, kuvuka daraja unalipia huu ukoloni ni wa kipuuzi sana kwa watu wa kigamboni , sijui watu wa huko wamelikosea nini hili taifa? yani kutoka kwake asubuhi akatafte hela ni lazma atoe hela kuvuka, bado wakati wa kurudi kukitafuta kitanda kuegesha mbavu mtu alipie kwenda kwake,, maana ake ukiwa na gari basi elfu 90 hadi 120 kwa mwezi za kuvukia ni lazima uwe nazo.... stupid
 
Kigamboni (sasa ni wilaya) ni sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo tofauti na maeneo mengine ilichelewa kuendelezwa kimiundombinu mpaka kufika miaka ya 90. Watu walichelea kuishi huko kutokana na kupaona ni maporini palipostahili kuishi wanyama.

Hivi leo, mambo ni tofauti sana, mji unakua kwa kasi ya ajabu, barabara zinajengwa kutangulia makazi ya watu, ni sehemu pekee katika jiji la Dar es Salaam ambako ukiingia unasahau kuhusu foleni za barabarani, hali ya hewa ni nzuri kutokana kutokuwepo kwa ujenzi holela wa nyumba, ni karibu sana na city centre na kuna fursa nyingi za kuanzisha biashara.

Binafsi nilifika kwa mara ya kwanza na kuhamia Kigamboni mwaka 2015 kutoka Survey maeneo ya karibu na Mlimani city nilipoishi kwa takribani miaka minne ila mpaka kufikia leo sijawahi kujutia kuishi huku wala kuwaza kuhamia mahali pengine katika mji huu kutokana na sifa nilizozitaja hapo juu na kwa bahati nzuri Mungu amenijaalia kujenga kakibanda huku huku.

Kwa ambao hawajawahi kufika huku hudhani kwamba Kigamboni ni kisiwa na kwamba usafiri pekee wa kufika huku ni wa kuvuka maji kwa pantoni, la hasha! Kigamboni si kisiwa bali imetenganishwa na sehemu nyingine ya jiji kwa sehemu ya bahari iliyoingia nchi kavu (ghuba) ambayo ni bandari ya Dar es Salaam na Kwa sasa ukiachilia usafiri wa wa pantoni kuna daraja na barabara mbili ambazo unaweza kupita bila hata kuiona hiyo bahari.

Karibuni sana Kigamboni.
Bei ya kiwanja shingapi
 
Sawa mkuu...

Anonymous haina jinsia.


Oyaaaaaaa Tangaaaazooooooooooo....!!

Wale wa Kigamboniinooooo mkooo taaayaaariiiiiii.......!!!

Kasie The Foodie anakuja kuwafundisha namna ya kula utumbo wa samaki, mbata za madafu na mazagazaga ya sea food....

Andaeni ndimu na pilipili, tangawizi nakuja nazo....

Kibali kishatoka hapa fulu TBS.....


Kiiigaaamboooniiinoooooo hoooooyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Wuuuuhuuuuuuuuuuuu....!!

Team Kg mko juuuuuuuuuuui........

Shurti niwaandalie KG Bash full of sea food hadi wenye allegies watakula bila kuathirika.

Hapana chezea Kasie The Foodie .

.
"kula utumbo wa samaki"


 
Kigamboni hakuna tofauti na Mbagala, hakuna tofauti na Temeke, hakuna tofauti na Yombo, hakuna tofauti na kiwalani, hakuna tofauti na kongowe.
maeneo hayo yote yanafanana sana
kwa sababu kwa asilimia kubwa yanakaliwa na wakaazi wa mikoa ya kusini.
Umeshafika Kibada? kama ungefika Kibada huwezi kuropoka haya.

Kibada kuna mashindano ya kujenga nyumba za ghorofa ukiwa na nyumba ya chini utatamani kuuza uhame.
 
Kigamboni ukishuka Panton tu unakutana na maeneo skwata ta kufa mtu.

Eneo Kama kigamboni ingebidi iwe Kama Masaki au ostabay ila kwasababu sisi watanzania hatuwezi kupanga Basi ni balaa tupu.
Mikwambe na Chekechea ni sehemu nzuri sana. Tuna wakaribisha, viwanja hakuna chini ya nusu ekari
 
Back
Top Bottom