Ukitaka Kuiharibu Jamii Yoyote, Shambulia Maeneo Haya 3

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
1,195
1,661
Kama jamii imetulizana ina maadili , usitumie mizinga ya atomic au masafa marefu . Shambulia maeneo 3 tu ambayo ni Ndoa na familia, Kioo cha jamii na Mfumo wa kielimu.Kwa leo tuone eneo moja.

1. Ndoa na Familia
Ukitaka mtotoo aje awe katili au jambazi , mlelee bila wazazi wawili (alelewe na mtaa), ukitaka mtoto wa awe haheshimu wanawake , mlelee bila baba yake halisi ,(akikua atalipiza mama yake alivyonyanyaswa na wanaume ). Ukitaka mtoto wa kike awe hana heshima kwa wanaume ,mlelee na mzazi mmoja.

Na hili wafanyabiashara wasio na maadili kama wauza midoli ya kupigia punyeto kwa wanaume na wanawake, wanajua cha kufanya ili kuongeza soko, chochea na kuza ugomvi wa wanandoa. Kosa ambalo mtu analivumilia kwa ndugu zake, analivumilia kwa rafiki zake, analivumilia kwa boss wake ,kosa kama hilo alione kuubwa mno akifanyiwa na mwanandoa mwenzie. Kinachofuata utengano ,hii inamaanisha madoli yatauzwa. Pombe zitauzwa za kutosha,watu walewe kwa jina la kuondoa stress. Kikubwa Zaidi, kuna mitoto inaenda kunuliwa kwenye ukahaba au ushoga.

Utaona hata humu mitandaoni wengi huomba hushauri wa ndoa , bila kujua wanaomjibu wana background zipi na zipi. Ulifungishwa ndoa humu mtandaoni?

Kama utamuuliza mtu, jana saa na dakika kama hii ya leo ulikuwa unaongea sentensi au neno lipi. Utakuwa umempa mtihani mkubwa sana , kwani uwezo wa akili ya mwanadamu una mwisho wa kufikiri.

Na kutokana na ukomo huo, utakuta kanuni alizojitungia mwanadamu, zinaenda zinabadilika . Mfano nchi za Ulaya , Mashariki ya mbali (China, Japan,Korea) na America ziliamua ili kuimarisha uchumi, mwanamke azae idadi maalum ya watoto tena kwa mpangilio maalum ilia pate muda mwingi wa kufanya kazi , program ilojulikana kama mapinduzi ya viwanda (Industrial revolution).

Miaka imeenda, uzazi mpango umejibu, tahamaki jamii hizo zina population yenye wazee wengi kuliko vijana. KWa lugha nyingine ,nguvu kazi ya wazalishaji (Vijana) ambayo ni kidogo , inahudumia wasiojiweza kuzalisha wengi (Wazee na watoto).

Nchi zote zimeupitia mpya mpango wa uzazi wa mpango kwa kuanza kuomba wanawake wafungue milango ,bali wameenda mbali,sasa kuna zawadi kwa kila mwanamke anayekubali kubeba ujauzito.

Ama kwa hakika, akili hii ndipo Muumba aliweka sheria ili kuichunga akili hii isifanye uharibifu. Makala ijayo tutaaangalia eneo la pili na la tatu la kushambulia ili kuimaliza jamii.

Inahitaji busara ya wazazi wako walokulea wakiwa wawili pamoja, na inahitaji upumbavu wako, kumlea mwanao kwa upweke usio wa lazima.

china 3 children policy.PNG
europe allowance.PNG
kim un.PNG
 
Kuna wale wanakuja kuomba wanaume wa kuwaoa wanasema wamechoka kuishi single huku wakiwa tayari wamezaa watoto bila baba wanayeishi pamoja. Wanajibiwa vibaya na wahuni
 
Kuna wale wanakuja kuomba wanaume wa kuwaoa wanasema wamechoka kuishi single huku wakiwa tayari wamezaa watoto bila baba wanayeishi pamoja. Wanajibiwa vibaya na wahuni
Kila mwanadau hukosea.Kama unaweza muoe, lea wanae .Mbona tunalea yatima wengi tu.
 
Back
Top Bottom