Ukitaka kufanikiwa 2017 katika maisha achana na tabia hizi

Hiyo inamaanisha aliyefaulu maisha amuepuke ambaye amefeli maisha. Na mwanadamu ni mnyama anahitaji kuwa atakapoona hapa ninakubalika hivyo aliyeshindwa maisha atajikuta anarudi alipotoka na aliyefaulu kwenda kwa wenzie.
hapav nilikuwa nina maana usipende kukaa watu ambao wanaweza kukukatisha tamaa katika maisha
 
Tafuta Kwanza Baraka za BWANA, Anza kwenda kwa wazazi ili upewe baraka huko, kama umeoa tunza familia ili ikubariki, kama unamwamini BWANA toa zaka na sadaka, acha uzinzi na namna zake zote, Acha tabia ya kwenda kazini kwa mazoea bali jifunze kwenda kujituma kazini, tunza akiba ktk pesa au vitu ama ktk vyote.
 
very true 6,7 na 8 zimeniathiri sana hasa mawaka jana, pia kuna binamu yangu nilimkopesha laki 3 na nusu tangu mwaka 2014 mpaka leo naona hana mpango wa kurudisha, inagawa kiukweli hali yake kiuchumi si nzuri ni mwanachuo diploma hana stable financial supporters ila inaniuma sana hela yangu hasa kwa usawa huu sasa hivi wa uncle magu kila nikifulia naikumbuka.
Msamehe broo
 
Achana na Imani za kishirikina badala yake fanya kazi kwa nguvu zako zote pasipokuwa na aibu ya kazi yako unayoifanya " milion values one shiling"
 
Namba 9&4. Najitahidi Ku delete completely nisije aibika na Mungu atanisaidia amen!
 
kama wewe ni kijana na ungependa kuona mwaka huu ukipata mafanikio katika maisha basi achana na hizi tabia .

1.tabia ya kufatilia maisha ya watu na familia zao.

2.tabia ya kujilinganisha uwezo wako kimaisha na wengine .

3.tabia ya kutaka kuonekana kwa watu unajua kila kitu.

4.kumpenda mtu asiyekupenda

5.usipende kuwa na urafiki na watu walioshidwa maisha.

6.usipende kuwa na tabia za kukopesha watu pesa

7.usipende kuwa na moyo wa kusaidia watu ili uonekane mtu mwema mtu akikuomba kama huna mwambie sina.

8.achana na tabia ya kufanya mambo kwa ndugu au marafiki upate sifa uonekana uwe una pesa.

9.achana na tabia ya kuhonga ovyo

10.tabia za ubishi usiokuwa na maana achana naoo.

haya jamani kama una mengine hebu ongezea iwe kama somo
epuka kupoteza muda mwingi kwenye mitandao: whatsAPP, fb, int, jf, twitter, ect
 
Mkuu tabia nyingine nzuri ni kufanya mazoezi hii inasaidia sana kuwa na displine na kutokuwa na stress za kijinga...kufocus kwenye mambo ya marndeleo na kuepuka magonjwa ya kijingakijinga.Hii ndio ari yangu ya mwaka huu wa 2017.Bila kusahau kula ovyoovyo ...eat healthy.Lingine jifunze kujipa raha mwenyewe kabla ya mtu mwingine.....life is all about you.Jiridhishe mwenyewe kabla ya mtu mwingine.Cheers and happy new year guys
 
Back
Top Bottom