Ukitaka kufanikiwa 2017 katika maisha achana na tabia hizi

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,683
kama wewe ni kijana na ungependa kuona mwaka huu ukipata mafanikio katika maisha basi achana na hizi tabia .

1.tabia ya kufatilia maisha ya watu na familia zao.

2.tabia ya kujilinganisha uwezo wako kimaisha na wengine .

3.tabia ya kutaka kuonekana kwa watu unajua kila kitu.

4.kumpenda mtu asiyekupenda

5.usipende kuwa na urafiki na watu walioshidwa maisha.

6.usipende kuwa na tabia za kukopesha watu pesa

7.usipende kuwa na moyo wa kusaidia watu ili uonekane mtu mwema mtu akikuomba kama huna mwambie sina.

8.achana na tabia ya kufanya mambo kwa ndugu au marafiki upate sifa uonekana uwe una pesa.

9.achana na tabia ya kuhonga ovyo

10.tabia za ubishi usiokuwa na maana achana naoo.

haya jamani kama una mengine hebu ongezea iwe kama somo
 
very true 6,7 na 8 zimeniathiri sana hasa mawaka jana, pia kuna binamu yangu nilimkopesha laki 3 na nusu tangu mwaka 2014 mpaka leo naona hana mpango wa kurudisha, inagawa kiukweli hali yake kiuchumi si nzuri ni mwanachuo diploma hana stable financial supporters ila inaniuma sana hela yangu hasa kwa usawa huu sasa hivi wa uncle magu kila nikifulia naikumbuka.
 
The giving hand is the receiving hand......hii inakwenda against na no.7 yako.

No.9 its OK.

Ila umenishangaza kwa hili mkuu, umeandika yote ila hujatuambia kua tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu ktk kazi zetu. Mimi sijawahi Ona mtu kafanikiwa bila kufanya kazi.

Hayo mengine yote uliyoandika ukiacha na kazi hufanyi bado hutofanikiwa tu
 
pole sana hiyo mbona imewakuta watu wengi tuu swala la kumkopesha mtu pesa wee lisikie tuu
 
kama wewe ni kijana na ungependa kuona mwaka huu ukipata mafanikio katika maisha basi achana na hizi tabia .

1.tabia ya kufatilia maisha ya watu na familia zao.

2.tabia ya kujilinganisha uwezo wako kimaisha na wengine .

3.tabia ya kutaka kuonekana kwa watu unajua kila kitu.

4.kumpenda mtu asiyekupenda

5.usipende kuwa na urafiki na watu walioshidwa maisha.

6.usipende kuwa na tabia za kukopesha watu pesa

7.usipende kuwa na moyo wa kusaidia watu ili uonekane mtu mwema mtu akikuomba kama huna mwambie sina.

8.achana na tabia ya kufanya mambo kwa ndugu au marafiki upate sifa uonekana uwe una pesa.

9.achana na tabia ya kuhonga ovyo

10.tabia za ubishi usiokuwa na maana achana naoo.

haya jamani kama una mengine hebu ongezea iwe kama somo
Kwa hio ukiacha vtu hivi unafanikiwa Kimaisha?

Sent from my HUAWEI Y300-0100 using JamiiForums mobile app
 
The giving hand is the receiving hand......hii inakwenda against na no.7 yako.

No.9 its OK.

Ila umenishangaza kwa hili mkuu, umeandika yote ila hujatuambia kua tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu ktk kazi zetu. Mimi sijawahi Ona mtu kafanikiwa bila kufanya kazi.

Hayo mengine yote uliyoandika ukiacha na kazi hufanyi bado hutofanikiwa tu
uko sawa kabisa mkuu ndo maana nikaongezea tujiongeze kidogo
 
Hilo linaitwa Wazo Pevu,sio vijana tu kwa watu wote ukishakopesha hesabu umetoa msaada kurudi ni Bahati!
 
5.usipende kuwa na urafiki na watu walioshidwa maisha

Hiyo inamaanisha aliyefaulu maisha amuepuke ambaye amefeli maisha. Na mwanadamu ni mnyama anahitaji kuwa atakapoona hapa ninakubalika hivyo aliyeshindwa maisha atajikuta anarudi alipotoka na aliyefaulu kwenda kwa wenzie.
 
6.usipende kuwa na tabia za kukopesha watu pesa

7.usipende kuwa na moyo wa kusaidia watu ili uonekane mtu mwema mtu akikuomba kama huna mwambie sina.

Unapoishi kwa hizi kanuni na wenzako wakiishi kwa hizi kanuni, natumaini utamuelewa akikwambia "Pesa ninayo ila siwezi kukupa C Programming alitoa kanuni za kufanikiwa, moja wapo ni sitakiwi kukukopesha, fack that kwanza sitakiwi hata kuwa na moyo wa kusaidia."
 
14. Acha kabisa kuwa mwana Ccm, itakugharimu 2017... Maana wamaweza kukuingiza na ww kumtafuta Faru John
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom