Tabia ya wafanyabiashara kukaa na simu zinazotumika kufanya miamala mbali na eneo la biashara inakera

Daydream

Member
Oct 26, 2023
58
328
Kuna hii tabia imezuka ya wamiliki wa biashara kuweka huduma za kifedha za mitandao ya simu mbalimbali lakini simu wanakaa nazo wenyewe mbali na ofisi zao na kwenye biashara zao wanaweka vijana ambao ukitoa pesa au kuweka lazima awasiliane na bosi wake ili akupe au kukuwekea.

Hii tabia kiukweli inakera sana hasa pale inapotokea mtu una haraka lakini huwezi pokea pesa zako au kuwekewa kwa wakati mpaka kijana aliewekwa dukani awasiliane na bosi wake ndio uwekewe au ukabidhiwe pesa baada ya kutoa kitu ambacho kinaweza chukua hata dakika 20 kama bosi hayupo very responsive.

Kama vijana mnaowaweka dukani hamuwaamini basi hakuna sababu ya kuweka huduma za kifedha mana zile huduma ni za haraka na mtu hutegemea ndani ya dakila 3 mpaka 5 awe amepata huduma na kuondoka zake, kumuweka mteja zaidi ya dakika 20 kwenye ofisi yako ni kumpotezea muda

Jitahidini kubadirika.
 
Kwa kweli inakera sana ila nadhan sababu ni kuogopa kuibiwa wengi wa vijana wanaowekwa madukani ni kutoka njee ya mji hivyo janja janja wakija ni rahisi kuibiwa kuna mteja wangu wa mayai aliibiwa 1.46ml dukani aliweka kijana na elimu ya hapa na pale alishampa,
 
Back
Top Bottom