Ukitaja Viongozi Wanafiki waliowahi kuihadaa Zanzibar Ukimtaja Maalimu Seif usimsahau na Dr.Bilal


Dr. Bilal kazi ya awali baada ya kuapishwa ilikuwa ni kutalii Mbuga za Serengeti kuumiza walipa kodi, maana alikuwa na wake zake watatu na kundi kubwa la wana Usalama yote hiyo ni ponda kodi; Dr. Bilal alijenga matumaini makubwa juu yake na watu walitegemea kuona changes akipata nafasi kubwa Serikalini yupo wapi ana lala wapi leo nafasi kapata, kama hawataki tusimwite Mnafki na mtu wa hila basi wamuamshe tuone yale makeke yake.
 

Hii ni Post ya kwanza tokea kujiunga JF Hoingera sana na karibu; ebu twambie wewe unajuwa nini juu ya Dr. Bilal mara zote akilazimisha kugombea Urais wa Zanzibar, mara zingine akifanya kinyume na taratibu za CCM hata pale ambapo ilitemewa kwa taratibu za CCM kuwa hakuta kuwepo Mgombea wa Kumpinga Karume ndani ya CCM.

Dr. Bilal alijitokeza kama alivyofanya Shibuda kwa Kikwete lakini kumbuka kuwa Shibuda yeye alitangaza nia tu! Ila Dr. Bilal yeye alikuwa anachukuwa hadi form
 
Wakati wazanzibari wanaendelea kukejeliwa wanapotaka kujitenga....wabara wako bize na kusapoti mambo haya


Nani anakejeli? Kikwete kawapa nafasi wote wawili kwa makusudi kabisa, Maalimu Seif wa CUF na Dr. Bilal kijana wa Komandoo sasa mbona hamna kitu, kama siyo uchu wa madaraka na njaa ya tumbo, Dr. Bilal aliaminika kama ndie atakaye weza kutete kuleta mfumo wa Muungano ambao Wazanzibari wanautaka kwa upofu wao, leo kawa kimia kabisa ameshajuwa kuwa sasa atakula pesa ya walipa kodi wa Tanganyika hadi afe atautete huu Muungano hadi afe!

Kama ni uongo time will tell.
 

Makene wewe unamjuwa sana Dr. Bilal na umekuwa ukizunguka naye sana katika ziara zake na hata Serengeti ulikuwa naye; Twambie Dr. Bilal tokea mwaka 2000 matumaini makubwa ambayo Wazanzibari walijenga juu yake ilikuwa ni ya nini? waitegemea nini kutoka kwake kama ikiwa akipata nafasi ya uongozi kama huu aliopewa sasa?
 

Makene mbona unanichekesha sasa! yaani alienda kutafuta ukweli juu ya barabara ya Serengeti?! Kweli wewe kiboko

Ebu angalia hapa kama kweli huyu siyo Mtalalii
H@ki Ngowi: Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal Akiwa Katika Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti

View attachment 33648

View attachment 33649


 
wa jina, Makamu alienda serengeti kula bata baada ya uchaguzi siyo uzushi, tena alienda na wake zake wote wawili. Ngoja nizitafute zile picha nikubandikie.
 
Mkuu, Arafat, tuko pamoja mwana, Haki unayo ifunua Inawauwa sasa wazenj kwisa tambua. Janja ya nyani kula hindi bichi, hao ni kigingi kwa manufaa ya wazanzibar. Waguse penye ulaji uone.
 

Hawa watu kwa muda mrefu sana wamekuwa tayari kwa lolote ilimradi waingie Madarakani; Wazanzibar wajidanganya juu yao hata kuwa tayari kwa lolote kwasababu ya hawa jamaa wawili lakini hawakujuwa kuwa hawa jamaa walikuwa na tamaa tu ya madaraka na uchu binafsi leo ndio watajuwa sasa Huwezi kumsikia Seif tena na zile kelele za kila siku ziko wako wapi? utafikiria kafungiwa Mtungini kwisha habari yake.
 
Umedandia hoja na kuongea yasiyomo. Nani kakwambia tunahubiri Uzanzibari hapa? Usikurupuke kuchangia jambo kama hulielewi mantiki yake.

Huyo hayupo nasi hapa, au hajatuelewa kabisa.
 
Sikuwahi kufikiri kama huyu ndugu Bilal anatabia kama za bwana Seif.

Wanafanana kila kitu hawana tofauti hata kidogo!

Wakati wote aking'ang'ania madaraka na kuwaadahaa Wazanzibari alijifanya sana kuwa yeye anampango wakubadili aina ya Muungano na kuiunganisha Zanzibar na OIC, na kwa kuwa huo ndio upofu wa Wazanzibar basi wanasiasa wanaotaka kura za chee huko utumia hila hizo na kupata kile kinachoitwa 'Cheap popularity' ambacho ndio Dr. Bilal alijizolea huko Zanzibar waliweka matumaini makubwa sana juu yake na kwa upofu wao waliamini kuwa akipata nafasi kuna lolote hawakujuwa kuwa ni kama wana-CCM wote walivyo wakati wakampeni ahadi lukuki baada ya hapo mtawaona tena uchaguzi ukiwadiwa.

Leo kaonja kodi ya Watanganyika hutamsikia tena wakiilaani Muungano watautetea hadi tone lao la mwisho, shida yao ilikuwa vyeo na ndicho walichokuwa na uchungu nao.

Hawa jamaa wawili nawafananisha na Zitto Kabwe wa CDM.
 

Kaka Makene yupo kazini anamjuwa Dr. Bilal fika na anazunguka naye kila siku, husidhani hayo unayomwambia hayajui anayajuwa lakini Bilal nadhani anamlipa kwa ajili ya kumsifia, namjuwa sana Makene ni Rafiki yangu ila kanunuliwa na RA kwahiyo hapo fedha zinamfanya kipofu.
 
Mkuu wangu siku zote nimekuwa nikiwaambia kwamba hawa viongozi wote ni wanafiki lakini hamkunielewa mkidhani sipendi maendeleo ya Wazanzibar. Hakuna kiongozi hata mmoja Zanzibar asiyekuwa mnafiki hilo ndilo nilojifunza isipokuwa wale waliokimbia toka wakati wa Karume. Na ktk swala hili wala usimseme Bilal peke yake kwa sababu anajulikana kuwa tapeli, majisifa, mroho na asiyetosheka na utajiri bali pia kisiasa lazima pia umwongezee Karume ambaye alichukua madaraka ya uongozi wa Zanzibar kwa kufuata maagizo ya CCM bara ili Zanzibar isijiunge na OIC. Na sii hivyo tu hata kukawepo na uadui wa kiana usiohusiana kabisa na maslahi ya Wazanzibar bali nani atashika madaraka gani na nani kakosa! Mbali na yote hayo angalia jinsi walivyojilimbikiza mali na yasemekana karibu kila hotel za kitalii beach wana 10%!...

Yaani Linchi letu lote limeoza kwa UNAFIKI ambao nadhani yawezekana inaingia ktk Uasili wa tamaduni zetu kwani haiwezekani unafiki huu wa kuuzana uwe wa bahati mbaya (coincidence) Upo ushahidi wa kihistoria unaoturudisha toka enzi za Utumwa kwamba sisi wenyewe tuliwauza ndugu zetu kwa kubadilishana na shanga!..Mambo mengi yanajirudia toka kuuzwa kwa nchi, mikataba na kadhalika yote haya yana historia ya Uasilia wa Mtanzania kwa Unafiki.. ndugu marafiki tunazikana kila siku yaani kwa Mbogo usikosee ukamwamini atakuweka mjini!
Kisha tunajiuliza ati sisi tumemkosea nini Mungu!
 
wa jina, Makamu alienda serengeti kula bata baada ya uchaguzi siyo uzushi, tena alienda na wake zake wote wawili. Ngoja nizitafute zile picha nikubandikie.

Makene anajuwa zaidi yako na alikuwa naye huko kwa taarifa yako.
 

Mkandara! GOOD there you are;

Niliwai kusema kuwa unaweza kukuta hata hawa tunaowapa matumaini makubwa sana leo kesho wakaturudi, huwa nasema na sita ogopa kusema hadi kifo changu kwa CDM hadi leo ninayemwamini ni Dr. Slaa tu! Nina wasiwasi mkubwa sana na Zitto kabwe na Mbowe! Sijui kwanini imani yangu inawakataa kwa kweli siwa amini hata kidogo wanatumia ujinga wetu kutu adahaa na amini hivyo na nitaendelea kuamini hivyo mpaka watakavyo onyesha tofauti na kuni-prove wrong.
 

Tangu nianze kusoma post hii uliyoileta hapa nilipata maswali kadhaa na kisha kugundua yafuatayo:
1. Ninakufahamu na hukutegemea nijitokeze kukujibu hapa, nakufahamisha tu kuwa sina uoga katika kuzungumzia ukweli hata kama utakuchoma na hata kama utatoa tafsiri kama ambazo umeweka hapo
2.Umemuweka Seif Sharif katika mada hii kimtindo tu ili kurahisha kufikisha lengo lako ambalo kubwa ni kupinga Muungano, hoja ambayo ina mashiko katika vyama vinavyoshabikia serikali tatu.
3. Huna taarifa za kutosha juu ya mada hii kwa kuwa unatoa taarifa nyingi za kuhisia tu
4.Uwezo wako wa kuchambua hoja bila kuingiza mambo binafsi unaashiria kuwa hufai kupewa nafasi ya kuweka post hapa JF
5.Huna taarifa ya Katiba ya nchi hivyo hutambui hata majukumu ya viongozi wako wa kitaifa nafasi zao na kazi zao
6.Dk Bilal ni kiongozi wa Tanzania nzima ikiwemo Zanzibar kwa hiyo anafanya kazi kwa maslahi ya watu wa Rukwa, Kigoma, Singida Mjini Maghribiu, Kaskazini Pemba na kwa kiapo chake ni jukumu lake kufanya kazi kwa maslahi ya watanzania
7. Hoja ya uadilifu na mapenzi ya nchi yake sambamba na kutokuwa na tamaa ya mali ni sifa anuai alizonazo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo fanya tafiti kabla hujakimbilia kutoa hoja zinazoonyesha kuwa una chuki binafsi na viongozi wa nchi yetu ya Tanzania
 
Maneno yako kweli kabisa na una kila haki ya kutomwamini mtu yeyote kutokana na utamaduni wa Mtanzania (Unafiki) hilo halina shida kabisa isipokuwa nitayarudia maneno ya Lowassa ya kwamba ni bora kuchukua maamuzi magumu ukalaumiwa kuliko kutofanya kabisa! na pia ile ya JK kuhusu akili za mbayuwayu kwamba - Unapoambiwa kitu lazima usiamini moja kwa moja lazima uchanganye na za kwako!..

Haya yote ni mawazo yanayozingatia Uasilia wa watu na mazingira tuliyopo kwani sisi ni wavivu wa kufikiri, kutenda na kikubwa zaidi ni wanafiki. Tahadhali ni muhimu sana.

Mbowe na Zitto ni vijana wadogo sana ambao kiuhakika hawajafikia kujijenga kisiasa na kuwa na mtandao unaotisha. Hivyo, ni rahisi kuwaondfoa pindi watakapo vurunda kuliko kumwamini mtu yeyote anayetumikia cartel ya CCM. Na pengine niseme tu kwamba mimi nawaunga mkono Chadema kwa kutazama upeo wenye mwanga ktk kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini kwani kama Chadema watashinda na wakaharibu ni rahisi kuwaondoa wakasambaratika kama ilivyotokea Kenya ktk kumwondoa KANU.

Lakini sii kazi rahisi kabisa kumwondoa kiongozi yeyote aliyewekwa na CCM na wala sii rahisi kumpata kiongozi bora atakayetokana na CCM kwa sababu hii ni cartel ambayo inamweka mtu kwa maslahi ya chama kama walivyowekwa wote wale waliotangulia. Haiwezekani kiongozi bora atoke CCM ikiwa CC ya cartel ndiyo inamchagua mgombea - Haiwezekani atapigwa chini kwa hali na mali.

Dr.Bilal, Maalim Seif, Shein, Karume na hata Salim A. Salim wote hawa wamekulia CCM na labda watu wanashindwa kuelewa kwamba TANU na ASP zilikuwa na mahusiano makubwa kabla hata ya Mapinduzi. Mipango yote ya ASP ktk chaguzi za Zanzibar, TANU walikuwa nyuma yake na hata Mapinduzi yaliyofanywa na Umma Party yalidumu miezi miwili tu kabla TANU na ASP hawajayateka na kuwa yao, kisha leo hii watu tunashangaa na kujiuliza kuhusiana na Muungano while sote tunaamini Nyerere na Karume wakishirikiana na CIA kunyapua Mapinduzi!.kweli tuna akili timamu kama tunaijua historia ya mapinduzi vizuri?

Binafsi ndani ya CCM visiwani pengine naweza kumwamini Salim A. Salim pekee kwa sababu ya msimamo kama ule wa marehemu waliotangulia kina kina Dr Omar, Jaji Omar, Prof. Haroub Othman waliokuwa na msimamo dhidi ya system kwa maslahi ya wananchi..
 

Makene nini kimekuhudhi Mkuu?

Mbona unaanza kunishambulia mimi sasa badala ya maswali ya Msingi yaliopo hapa juu ya Dr. Bilal? Akiwa kiongozi wa Tanzania nzima na amini ndio anayonafasi nzuri sana ya kuisaidia Zanzibar hasa kwa yale ambayo aliwaaminisha Wazanzibari kwa muda mrefu kabla ya kupata nafasi! Kama alikuwa awadanganyi Wazanzibari sasa anafanya nini?

Nimesema hana touti na Maalimu Seif kama wewe unajuwa tofauti yao tuweke hapa.
 
Hapa Mkuu umechanganya madawa. Unazungumzia Wapemba gani waloweka matumaini kwa Dk. Bilal?
Ni Muungano gani waliofanya Seif na Bilal? Ni Wapemba gani waliopiga kura kumpinga Amani?

Ninavyoelewa mimi Seif na Wapemba walikuwa paka na moshi na Bilali, sijui sasa ambapo hawa wawili wamo ndani ya dau moja. Inawezekana wote wawili ni wasaliti (kwa maneno yako, sio yangu), kila mmoja na watu wake (Bilali na Waunguja na Seif na Wapemba) daima hawajawahi kupanga wala kufanya kazi pamoja.
 

Hata kupendana kwao hakukupaswa kutangazwa. Ukweli ni huo kwa mimi nnaeyajua.
 

Naweza kukuunga mkono asilimia 100%; maana hatuna jinsi bali kuishi kwa matumaini hasa pale tunapo yaona na kuhisi kuna matumaini kwasababu kitu ambacho kingeweza kutuepusha na aina hii ya wanasiasa ni Katiba Mpya ambayo pamoja na mambo mengine ingeunda Strong Institutions za kusimamia maslahi ya Umma, lakini CCM wanakwepa hilo na hawawezi kulifanya kwasababu wao ndio wanaofaidika na kuishi kwa uzembe huu ambao mtu anaweza kujitokeza kuwaadahaa wananchni ili mradi apate nafasi ya madaraka.

Mi binafsi imani yangu ipo kwa CDM kwa hali iliopo Tanzania na jinsi CCM walivyoinajisi hii nchni, ila lazima sisi kama wananchni tuelewe na kujuwa jinsi wanasiasa aina ya Dr. Bilal na Maalimu Seif wanavyoyuchezea kila mara na wanavyotumia kwa ajili ya maslahi yao binafsi na kuungana kutunyonya damu kila kukicha.

CDM inabidi 2015 waje na Mkataba wa kueleweka juu ya swala la Katiba mpya pamoja na kujenga strong institutions kuepuka siasa za kutegema tabia ya mtu ili tuwe na system imara, na hii lazima ndio kazi za awali kabisa, Wakenya wameweza 'why to us'.

Mfano ndani ya CCM hawa Wanafki ndio wenye nafasi kubwa zaidi na kila mara wamekuwa wakiwadangaya wananchni lakini hakuna system ya kuwachukulia hatua, hata ukiangalia aina ya Siasa ya Kikwete 1995 ilikuwa ni ya kuwa adahaa wananchni, watu wakaweka matumaini yao makubwa juu yake, huku akiwadanganya kuwa yeye ni Nyerere aliyefufuka, na kuwa Lowasa na Sokoine mwingine, Watanzania sijui kwanini wanakuwa wepesi wa kusahau leo hii Wakina Makene bila aibu wanajitokeza kuandika kutete hawa watu, alipo ingia madarakani basi kasahau kuwa alisema maisha bora kwa kila Mtanzania leo maisha bora kwa Ridhiwani mwanae aliyemaliza shule soon baada ya uchaguzi leo ni Billionea.


Mkandara; Mkataba na CDM lazima hasa juu ya nini wanatuahidi na nini tutafanya iwapo wao pia watakuwa kama hawa jamaa zetu waliozoea kutudanganya kila kukicha na sisi hatuamki tumeendelea kulala kila mara. Nafamu ukifanya analysis ni bora tudanganywe na Chadema sasa kuliko kuendelea kukalia uongo wa CCM na watu kama wakina Dr. Bilal, yes lazima analysis inaonyesha nafuu kuamini CDM kuliko CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…