aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 776
- 1,121
Ukistaajabu ya Profesa Lipumba ambae ni Alhaji utakutana nayo ya Profesa Bana ambae pia ni Mhadhiri wa siasa wa Chuo Kikuu Dar es Salaam lakini kwa bahati mbaya zaidi hajui historia ya Zanzibar wala haijui vizuri Katiba ya Jamhuri ya Muungano wala Katiba ya Zanzibar.
Jana wakati anahojiwa na kituo cha redio ya Ujerumani DW mada miaka 54 ya Muungano wetu Demokrasia na Haki za Binadamu anasema muungano wetu huu ndio ulioleta mfumo wa vyama vingi kabla ya muungano hakukuwa na mfumo wa vyama vingi amesahau kama Zanzibar.
Siasa za vyama vingi zimeanza toka mwaka 1954 kabla ya Tanganyika haijapata uhuru kulikuwa na ZPP ASP ZNP sijui alikusudia wingi gani huyu Profesa wakati huo Zanzibar hata idadi ya watu laki mbili haijatimia hapo hapo Profesa huyo anasema ikiwa mtu hajaridhika na matokeo ya uchaguzi ya urais anaweza kwenda Mahakamani.
Amesahau kama Katiba zote mbili ya Zanzibar na Muungano zinasema kwamba matokeo yote ya urais hayatohojiwa na Mahakama yeyote ile ya rufaa sijui katiba ipi aliyoisoma Profesa huyu Bana.