Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Iringa

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Iringa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,163
Reaction score
11,230
Katika hali isiyo ya kawaida kuzoeleka ni baada ya wakazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa leo kushuhudia maajabu ya dunia baada ya kushuhudia tukio la aina yake kwa mbwa kuwachukua watoto wa nguruwe na kuwalea kwa kuwanyonyesha maziwa yake.

Tukio hilo limetrokea machi 15 mwaka huu majira ya asubuhi baada ya nguruwe wa mmoja kati ya watumishi wa mungu (mchungaji ) Daniel Kisonga kushuhudia mbwa huyo ambae alikuwa amezaa watoto watatu na kufariki wawili na kubakia na mtoto mmoja na hivyo kulazimika kuingia katika banda la nguruwe na kubeba watoto wanne wa nguruwe na kuamua kuwalea na kuwapa huduma zote ikiwemo ya kuwanyonyesha kwa upendo watoto hao wa Nguruwe bila kuwadhuru.

Akizunguza na mwandishi wa habari hizi leo mchangaji Kisonga amesema kuwa ni vigumu kuamini kuna mbwa akinyonyesha watoto wa nguruwe wakati kwa kawaida mbwa amekuwa ni mnyama hatari kwa nguruwe hao hasa pale wanapozaliwa .

Amesema kuwa mbwawa wamekuwa wakiingia katika mazizi ya nguruwe na kuwala nguruwe hao baada ya kuzaliwa ili imekuwa tofauti kwa mbwa baada ya kuamua kulea watoto wa nguruwe .

Hata hivyo amesema yawezekana ni maajabu ya dunia ila pia yawezekana ni dalili za siku ya mwisho kama ambavyo zimepatwa kutabiliwa katika maandiko matakatifu kuwa siku za mwisho yatajitokeza mambo mengi ya ajabu ambayo binadamu ni vigumu kuamini mambo hayo.

Japo upande wa wadau mbali mbali wamehoji nguruwe hao iwapo wataendelea kunyonya maziwa na mbwa wataliwa na binadamu ama lah ! kutokana na nyama ya mbwa kwa kawaida kutoliwa na binadamu sasa iweje kwa nguruwe hao kunyonya maziwa ya mbwa.

Credit: Francis Godwin

attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • ngr1.JPG
    ngr1.JPG
    35.7 KB · Views: 2,328
  • ngr2.JPG
    ngr2.JPG
    26.9 KB · Views: 2,310
Mi naona kawaida tu..watoto wa kuku wanalelewa na bata
 
hakuna maajabu bali mbwa na nguruwe wakae mbali na waislam walishagundua kuwa awa wanyama niharamu wanaendana tabia
 
Katika hali isiyo ya kawaida kuzoeleka ni baada ya wakazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa leo kushuhudia maajabu ya dunia baada ya kushuhudia tukio la aina yake kwa mbwa kuwachukua watoto wa nguruwe na kuwalea kwa kuwanyonyesha maziwa yake.

Tukio hilo limetrokea machi 15 mwaka huu majira ya asubuhi baada ya nguruwe wa mmoja kati ya watumishi wa mungu (mchungaji ) Daniel Kisonga kushuhudia mbwa huyo ambae alikuwa amezaa watoto watatu na kufariki wawili na kubakia na mtoto mmoja na hivyo kulazimika kuingia katika banda la nguruwe na kubeba watoto wanne wa nguruwe na kuamua kuwalea na kuwapa huduma zote ikiwemo ya kuwanyonyesha kwa upendo watoto hao wa Nguruwe bila kuwadhuru.

Akizunguza na mwandishi wa habari hizi leo mchangaji Kisonga amesema kuwa ni vigumu kuamini kuna mbwa akinyonyesha watoto wa nguruwe wakati kwa kawaida mbwa amekuwa ni mnyama hatari kwa nguruwe hao hasa pale wanapozaliwa .

Amesema kuwa mbwawa wamekuwa wakiingia katika mazizi ya nguruwe na kuwala nguruwe hao baada ya kuzaliwa ili imekuwa tofauti kwa mbwa baada ya kuamua kulea watoto wa nguruwe .

Hata hivyo amesema yawezekana ni maajabu ya dunia ila pia yawezekana ni dalili za siku ya mwisho kama ambavyo zimepatwa kutabiliwa katika maandiko matakatifu kuwa siku za mwisho yatajitokeza mambo mengi ya ajabu ambayo binadamu ni vigumu kuamini mambo hayo.

Japo upande wa wadau mbali mbali wamehoji nguruwe hao iwapo wataendelea kunyonya maziwa na mbwa wataliwa na binadamu ama lah ! kutokana na nyama ya mbwa kwa kawaida kutoliwa na binadamu sasa iweje kwa nguruwe hao kunyonya maziwa ya mbwa.

Credit: Francis Godwin

attachment.php

attachment.php

Bado natafakari hiyo ralation kati ya mbwa na waatoto wa nguruwe......
Ubongo hautaki kuelewa, ingawa nimewekewa na picha lakini bado,.. umeme umekatika!
 
Mi naona kawaida tu..watoto wa kuku wanalelewa na bata

utafiti;
Nilidhani utasema kuwa uliona kawaida tu watoto wa kuku kulelewa na mwewe kumbe ni bata. Walimnyonya bata au? Kweli wengine hata mtu akitembelea ulimi juu ya mbigili hawaona ni ajabu kwao.
Tangu lini mbwa anyonyeshe nguruwe? Je hao nguruwe wakikua wataambatana na mama yao mbwa? Mama ni yule alie kunyonyesha banaa
 
TAREHE 15 MARCH MBONA HATUJAFIKA? HALAFU HAO NGURUWE NDO WALIWE NA WATU? MUCH worse!!!
 
Kwa Wahehe siyo maajabu kabisa kwani Nguruwe na Mbwa wote ni KITOWEO....

Haya ndiyo maajabu ya Simba kumtunza Digidigi.......

Last edited by a moderator:
Watakula tu wenyewe huyu mdudu anakula mpaka mtoto wa binadamu na bado wanakula hayo maziwa ya mbwa hayawadhuru hata kidogo.
 
Bado natafakari hiyo ralation kati ya mbwa na waatoto wa nguruwe......
Ubongo hautaki kuelewa, ingawa nimewekewa na picha lakini bado,.. umeme umekatika!
. Hata mm siwezi amini mbona tah 15/3 haijafika au ya mwk gani?
 
Mbwa huyo ana akili sana, ameogopa akionekana hana maana yeyote hapa duniani ipo siku atajikuta chunguni akitokoswa
 
Picha hii mbona imenitia kichefu chefu gafla kah!
 
Back
Top Bottom