Ukisikia kiongozi anaitwa Dikteta ujue amewaminyia makanjania ulaji

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Ukisikia kiongozi anaitwa Dikteta ujue ameminyia makanjanja wa nchi ulaji.

Makanjanja wa nchi wanataka na wao wapate kula, wafaidi mema ya nchi hivyo humsema kiongozi dikteta kwa sababu amewaminyia ulaji.

Ukisikia makanjanja wanapiga kelele sio kwa niaba ya wananchi, ni kwa niaba yao. Mfano, Gadhafi alikua anaitwa dikteta na makanjanja wa nje na ndani huku akiwafanyia wananchi kila kitu na wananchi hawakua na shida na Ghadafi.

Rais Kikwete aliweza kuishi vizuri na makanjanja wa ndani na nje kwa sababu aliwaruhusu kula nchi, kufaidi nchi huku nchi ikijaa rushwa, utendaji mbovu, uzembe wa watumishi wa umma, wizi, mikataba mibovu, na kila aina ya ujinga. Yeye alifanikiwa kua anawaita makanjanja ikulu wanakunywa juice pamoja, wana 'rub shoulders '.

Magufuli aliwabania makanjanja wetu wa kisiasa, akaelekeza nguvu kwenye ujenzi wa miradi na miundombinu ya kimkakati ya nchi kwa miaka mingi ijayo, miaka zaidi ya 50 ijayo, SGR, JNHP, hospitali kila wilaya, hospitali za kanda kila kanda, maduka ya madawa ya serikali kila wilaya, kila hospitali, miundombinu ya maji, barabara, shule, vyuo, umeme wa elfu 25(hapa tanesco ilijikusanyia wateja 1.2M kwa miaka 5 wakati kwa miaka 60 ya uhuru ilikua na wateja 1.8m tu hivyo kufikisha wateja 3m), kuhamishia serikali Dodoma ku de- conjest mji wa Dar es salaam, umeme kupatikana muda wote, chakula bei rahisi watanzania walikua wanakula milo 3 kwa siku bila wasiwasi na mambo mengine mengi ya msingi.

Cha ajabu makanjanja wanakwambia alikua dikteta, aliminya uhuru wa habari. Sasa uhuru wa habari ungelea hayo maendeleo ama ungejrnga SGR? Watu wanataka maendeleo ama wanataka uhuru wa habari.

Rais Samia ameamua kula na makanjanja, anawaita ikulu wa rub shoulders, huwezi kusikia wanapiga kelele tena kuhusu maisha ya Watanzania. Leo Tanzania maharage kilo moja ni 4,500 hadi 5,000 sawa na kilo ya nyama. Lakini ajabu makanjanja wao wanaongelea udikiteta wa Magufuli.

Naomba kuwakumbusha makanjanja, mkisimama kusema udikiteta wa Magufuli pia semeni na mazuri aliyoyafanya ndani ya huo udikiteta wake, semeni alikua dikteta sana hadi kujenga SGR ama JNHP, sio tu kusema Dikteta.
 
😆 Sidhani kama Chadema watakuelewa
Chini ya Magufuli shirika kama TANESCO liliweza ku-break even na kutengeneza faida pamoja na kuvunja mikataba ya kitapeli kama ya IPTL, Symbioni nk. Miaka 60 tanesco ilikua ni hasara tu ila mdani ya miaka 5 shirika likatengeneza faida. Soma vitabu vya hesabu vya tanesco ana report ya CAG inasema yote.

Makanjanja hawasemi hayo mafanikio makubwa, wao kila siku alikua dikteta, watuambie huo udikteta umetuletea faida gani na hasara gani, wasitaje hasara tu.
 
Siku watanzania wakielewa siasa ni kazi km kazi nyingine, na kua wanasiasa wapo kwa ajili ya maslai yao na familia zao kwanza then huwezi pata shida na siasa za Tanzania...wanasiasa wanatafta ulaji wao na sisi wanaichi tunawashabikia...siku akitokea mtu akaweka maslai ya wanainchi kabla ya wanasiasa kitawaka, atapewa majina ya kila namna ilimradi kumchonganisha na wanainchi.
But sisi wanainchi wa kawaida tunaelewa zipi mbivu zipi mbichi..
 
Nani huyo aliuwawa na kutekwa, unaweza kunipa orodha ya waliouwawa na kutekwa?

Dr. Slaa alisema Chadema ilikua na kikosi maalum cha kuteka na kuua. Je hicho kikosi ndio kilikua inateka na kuua?
Ni rais mpumbavu tu anaweza kuona chama kinaua raia wake akakiacha. Mnapoteza muda tu. Magufuli hakufaa hata kuwa kiongozi wa kijiwe cha kahawa. Alikuwa mtu wa hovyo
 
Ni rais mpumbavu tu anaweza kuona chama kinaua raia wake akakiacha. Mnapoteza muda tu. Magufuli hakufaa hata kuwa kiongozi wa kijiwe cha kahawa. Alikuwa mtu wa hovyo
Mtu asiefaa kua kiongozi hata wa kijiwe cha kahawa aliwezaje kutengeneza ama kuanzisha miradi ya maendeleo ya nchi ambayo itaisaidia nchi kwa zaidi ya miaka 60 ijayo?

Huo uhovyo unaipimaje? Kwa kuanzisha SGR, JNHP, hospitali kila wilaya, hospitali za kanda kila kanda na mkoa? Hiyo ndio hovyo kwa mtazamo wako sio? Aisee.
 
Back
Top Bottom