Ukisema Jini tayari kuna majini miatatu karibu yako. Kila mtoto mchanga huguswa na jini dakika moja bada ya kuzaliwa. Vitabu vya dini vinasemaje?

hapo kuna vingine umeongea ni vya kweli na vingi umeongea si vya kweli. sijui ata reference zako umepata wapi? kama ni vitabu vya dini basi tupe quotations.. kama ni fikra zako binafsi pia utuambie.
 
Ukinilimit namna ya kukujibu sitaweza kukujibu,ila tambua ya kuwa majini waliishi hii dunia katika miaka mig nyuma kabla ya uwepo wa mwanadamu na alijengea himaya kubwa ya utawala katika enzi ya Jann na Jadda,
Kuumbwa kwa mwanadamu kwa udongo ni kama kureplace kuumbwa kwa mwanadamu kwa Moto ambapo mwanadamu wa udongo amekuja kuwa juu ya moto na nadhani waona moto hauwezi kuwaka juu ya udongo ila udongo huweza kukaa juu ya moto

Soma taratibu nilichokujibu utaelewa kwa sababu gani moto umekuwa wa kwanza kuwapo duniani kabla ya udongo
*alijengea himaya kubwa ya utawala katika enzi ya Jann na Jadda,*

tafadhali naomba kufahamu kuhusu Jann na Jadda
 
Mtoa mada, kudo.

Hebu malizia hii mada, inawezekana tunauliza maswali mengine kwakuwa tu mada hujaikamilisha bado.
Hebu idadavue hadi mwisho tujifunze kwanza kabla ya kuuliza neno lolote.
 
Hapana mimi sijasuta
Nilikuwa nauliza tu na kama ni siri yako basi.
Unajua vijana wasomi wa siku hizi hawataki kudanganywa jambo, wanataka unapoleta mada flani unaweka na chanzo cha hiyo habari.
Isije habari hiyo ikaonekana kama ni uzushi wa mtaani tu, kama Jini ni Zuri weka ushahidi wa maandiko yaliyoasisi huo uzuri wa Jini.
La sivyo wasomi hawatakuelewa kabisa.
Wew ni msomi?!
Unaamini katika kitabu kipi cha dini?!
Hadi sasa umesoma vitabu vingapi na aina ngapi ya vitabu vya dini yako?!

Mada ikikuzidi uwezo bora ukae kimya tu mana najua hakuna msomi yeyote aliekaa tu bila kujishugulisha kusoma na kujifunza labda siku akifa ndo ukomo wake wa kujifunza hufika mwisho
Hakuna kitu chochote duniani kisichokuwa na pande mbili yani mbaya na nzuri
Ndio mana ww unafurahia kuhonga kuliko kumpa ndugu...

Lakini pia sijataka Mada yangu ikufanye uachane na imani yako juu ya biumb hao
 
Asante kwa uchambuzi, ila kasoro ni moja tu kuwa uchambuzi huu umepungukiwa rejea yaani reference.
 
Wew ni msomi?!
Unaamini katika kitabu kipi cha dini?!
Hadi sasa umesoma vitabu vingapi na aina ngapi ya vitabu vya dini yako?!

Mada ikikuzidi uwezo bora ukae kimya tu mana najua hakuna msomi yeyote aliekaa tu bila kujishugulisha kusoma na kujifunza labda siku akifa ndo ukomo wake wa kujifunza hufika mwisho
Hakuna kitu chochote duniani kisichokuwa na pande mbili yani mbaya na nzuri
Ndio mana ww unafurahia kuhonga kuliko kumpa ndugu...

Lakini pia sijataka Mada yangu ikufanye uachane na imani yako juu ya biumb hao
Sawa, Lete hiyo elimu ya Majini tujifunze kwako mtaalamu wa hao viumbe.
 
WANAKULA NINI?

Majini wao wanakula mifupa na mavi ya farasi. Hivyo ni vyaluka vyao vikuu pamoja na kwamba wengine wanakula Moshi (Ubani) na wengine wanapenda kunywa damu.

Wanapokula au kunywa, wao hutumia mkono wa kushoto na Majini wazuri ndio ambao wanakula mifupa mizuri na kuwaachia mifupa mibaya na uchafu Majini wabaya au Mashetani.

JE MAJINI WANAZAA?

Majini wanaoa na kuongezeka kama tulivyo Binadamu na huzaana kwa wingi sana.
Katika wao kuna wale wanaokula na kuoana na kuna wale ambao hawafanyi hayo.

Binadamu Mwanamume ana uwezo wa kumuoa Jini Mwanamke na Jini wa Kiume ana uwezo wa kumuoa Binadamu Mwanamke pamoja na kwamba ndoa inayotambulika na Mwenyezi Mungu ni ya kiumbe kwa kiumbe yaani Binadamu kwa Binadamu na Jini kwa Jini.

JE UNAWEZA KUWAONA MAJINI?

Majini hawawezi kuonekana kwa macho ya kawaida ila kwa Utaalam Maalum, ingawa Mtu yeyote unaweza Kumuita, Kumuona na hata Kumtuma Jini akufanyie au akuletee kitu chochote kile Naye akafanya vivyo hivyo kama

ulivyomuagiza; katika njia Rahisi kabisa kama inavyoelezwa hapo chini. Wao wana uwezo wa kutuona sisi.
Viumbe ambao wana uwezo wa kuwaona Majini au Mashetani kwa macho yao ni Mbwa na Punda

Ukimsikia Mbwa anabweka bila sababu yeyote basi atakuwa amemuona Jini au Shetani yuko karibu au anapita. Maelezo haya yamethibitishwa na Wanazuoni kuhusu kuonekana vile vitu ambavyo sisi hatuvioni.

Mfano mwingine ni kwamba Sisimizi ana uwezo wa kuona miale ya mwangaza yenye rangi ya urujuani na kwa hiyo kuona Jua litokeapo kwenye mawingu na Popo nae ana uwezo wa kumuona Panya kwenye giza nene.

KUMUONA JINI:

Iwapo unataka kwa haraka kuona Majini na kuwatumia; tamka Majina haya MARA 1,000;

• 1. Salsal, Salsal ........................x 1,000.
• 2. Akmash, Akmash..................x 1,000.
• 3. Laash, Laash......................... .x 1,000.


Tamka majina hayo hapo juu, huku ukiwa unafukiza Ubani Maka, Kuzbara na Majani ya Mnazi wa Kipemba au majani ya Mtende au majani ya Mchikichi.
Ukiwa sawa (yaani uwe msafi, mahali safi na nguo safi); atakutokea Paka mweusi au Taa kuzimika au kutokea Moshi mweusi.

Ndio huyo – Muagize lolote lile ulitakalo; akuitie Mpenzi, Pesa, cheo au Ushindi.
Ni vizuri pia ujue ni wakati gani au ni Sayari gani inayotawala ili ujue ni Jini yupi atakaekuja.

Unashauriwa;
• Uwe na nia ya kweli na wala si mchezo au kufanya majaribio.
• Usiwe muoga, kwani iwapo utakuwa muoga anaweza kukudhuru.



Kuwatumia au Kujikinga na Majini

JE MAJINI WANAWEZA KUTUMIKA?

Majini wanaweza kutumika kwa kazi mbalimbali ambazo Binadamu anaweza kumtuma.
Mwenyezi Mungu aliwaamuru Majini wamtumikie Mfalme Suleimani na wakawa wanamfanyia Kazi kadri anavyotaka yeye.

Katika Biblia 1 Wafalme 5: (13-17).

Biblia inaeleza jinsi nyumba ya Suleimani ilivyokuwa ikijengwa kimya kimya. ... “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwishachongwa chimboni, wala nyundo wala shoka, wala chombo cha chuma chochote sauti yake haikusikika ilipokuwa ikijengwa Nyumba”.

Majini vilevile wanatumiwa na watu katika kupata habari za mambo mbalimbali kwa sababu wao wana uwezo wa kupata habari angani.

Majini vilevile wanatumika katika ulinzi wa kulinda majumba au kulinda watu au Mikutano au Shughuli yeyote na vilevile wanaweza kutumika katika vita.
Wao wanajigeuza katika maumbo aidha ya Binaadamu au Mnyama na kushiriki katika vita.

Mfano Shetani mmoja alijigeuza kwa mfano wa Binaadamu mmoja aitwae Saraqa Bin Malik na kushiriki vita vya Badri na kuwaahidi Makafiri ushindi mkubwa lakini alipoona Majeshi mawili ya Malaika wanateremka kutoka Mbinguni alitimka na kutoroka.

JE TUNAWEZA KUJIKINGA NA MASHETANI?

Zipo njia nyingi za kujikinga na Mashetani lakini kubwa zaidi ni kutumia Jina la Mwenyezi Mungu na kumtaka Mungu akuepushe na Shetani mbaya Naye atakusaidia.

Shetani ana Maudhi mengi sana kwa Binadamu kwa sababu anapenda kujishirikisha na Binadamu katika kila kitu kama vile katika kula, kunywa, kufanya Mapenzi, kutembea, Kuishi ndani ya Nyumba na hupenda kufanya hayo yote pale Mwanadamu anapopotea na kumsahau Mwenyezi Mungu.

Shetani vilevile anamgusa kila Mtoto anayezaliwa katika dunia hii. Mtoto ambaye hajaguswa na Shetani ni Yesu au Issa Bin Maryam hayo ni kwa mujibu wa maelezo ya Qurani na Mtume Muhammad (SAW).

Mashetani vilevile ndio wanasababisha Ugonjwa wa Tauni (Plague – Ugonjwa unaoambukiza). Mtume Muhammad (SAW) ameeleza “Hakika kuangamia kwa Umma wangu kunatokana na kushuka Hadhi yao na Ugonjwa wa Tauni na Adui yenu Mkubwa anatokana na Jini, na Hiyo kwenu ni Shahada”.

Hivyo basi ili kujiepusha na maovu ya Shetani unashauriwa kumweka mbele Mwenyeezi Mungu katika lolote unalolifanya ukiwa Nyumbani au popote pale.

Itaendelea
 
Ina maana wazungu wanatumia ujanja wa majini ndio maana wapo mbele kwa kila kitu ?? Hata kwa mwafrika anaejua haya maujanja yupo juu kimaendeleo
 
Sawa, Lete hiyo elimu ya Majini tujifunze kwako mtaalamu wa hao viumbe.
Ngoja nikwambie kitu ndugu
Msomi yeyote akiona kitu kinampa utata huingia mwenyew katika utafiti ili ajue na aje na challenge katika mada ama kuhusu kitu cha kwanza alichokina ama kukisoma ndo maana hadi leo Da vince licha ya kuwa hayupo duniani ila watu bado wanapambana na uwezo wk
Hivyo usisubiri kila kitu uoneshwe source wew ukiwa umekaa tu bila kujishugulisha huku ukijiita msomi

Sorry kama maneno yangu yamekukwaza ila nikutaka tu tuwe sawa na hata kama utaenda kutafuta elimu hii ya uongo au kweli basi uje na nondo ili wengine wajifunze.

Mfano ni kiranga haamini uwepo wa Mungu lakini anahoja na reference za msingi kiasi kwamba hata ww unaeamini uwepo wa mungu anakuacha mdomo wazi unaishia kulaani tu tabia yake hiyo
So unapobisha kitu njoo na mbadala wake ili sote tujifunze

Hope umenielewa na wengine watanielewa
 
Marafiki na Maadui wa Majini
MARAFIKI WA MAJINI:

Majini huwa wanafanya Urafiki na Binadamu lakini Marafiki wao wakubwa ni Ngamia.
Baadhi yao wanaishi katika nyumba tunazoishi na ukitaka kuwafukuza unasoma Quran au Biblia au kumtaja Mwenyezi Mungu.

Majini hukusanyika na kuongezeka giza linapoingia au unapopatwa Mwezi, na huwa wanakimbia wanaposikia Adhana au Kengele ya kamba.
Majini wengi wanapenda kukaa baina ya kivuli na jua na siyo vizuri kukaa eneo hilo.

SURA ZA MAJINI NA MASHETANI:

Majini sura zao ni za kutisha na mfano wake ni kama Matunda ya Mti wa Zaqum ambao unatoa matunda yenye sura mbaya na yanayofanana na mawe.

Majini wanakuwa na mkutano kila siku nyakati za kuchomoza na kuzama Jua na nyakati hizo ndizo ambazo wanafanya maasi yao.

Fitna na Maasi yao mengi wanafanyia upande wa Mashariki.
Majini vilevile wanaweza kujigeuza kama mbwa mweusi au paka mweusi kwa sababu Majini wanapenda Rangi Nyeusi kwa sababu ya kiza.

UADUI WA MAJINI NA BINADAMU:

Majini na Binadamu wana Uadui wa asili tangu pale Binadamu alipoumbwa na kabla Mwenyezi Mungu hajampulizia Roho; Shetani akawa anauzunguka mwili wa binaadam na kusema “Nikipewa Uongozi juu yako basi nitakufanya uwe Aaswi (Usimsikilize Mola wako) na ikiwa utapewa wewe Uongozi basi nitakuangamiza”.
Mungu alipompulizia Roho Adamu aliwaamrisha Ibilisi na Malaika wamsujudie lakini Ibilisi alikataa kwa kusema kwamba Yeye ni bora kuliko Binadamu.

JE MAJINI WANAKUFA?
Majini na Mashetani nao wanakufa isipokuwa wao wanaishi miaka mingi kuliko Binadamu kwa sababu hawana maumbo maalum.

TUNAWEZA KUWAUA MAJINI?

Majini tunaoishi nao nyumbani mwetu tunaweza kuwaua kwa kutumia utaalamu Maalum. Lakini kabla ya kufanya hivyo unatakiwa umuadhinie mara tatu Kidini yako au Umtaje Mwenyezi Mungu mara tatu; asipobadilika au

kuchukua mfano mwingine muache, lakini akibadilika muuwe huyo atakuwa Shetani.
Shetani anapohisi Binadamu anataka kumdhuru basi hukimbia kama vile damu inavyokimbia kwenye mishipa ya damu.
MAUMBO NA SURA ZA MAJINI KULINGANA NA SAYARI ZAO
1. Majini wa Saturn (Zohal) - Majini wa Jumamosi

Majini hawa huwa ni warefu, wembamba na wenye sura ya ukatili na kutisha, wana nyuso nne ambazo kila moja iko kila upande wa kichwa, yaani kwa mbele na nyuma sura inakua na midomo kama ya ndege.

• Pia wana sura nyeusi inayon’gaa katika kila goti. Mwendo wao ni kama mwendo wa upepo ambao huambatana na radi.
• Alama yao ni ardhi nyeupe kuliko theluji.
• Umbo lao maalum ni kama Mfalme mwenye ndevu anaemuendesha DRAGON.
• Umbo lingine ni la mtu mzee mwenye ndevu
• Umbo lingine ni la Bibi kizee ambae anaegemea kitu
• Umbo lingine ni la Mvulana
• Umbo lingine ni la Dragon
• Umbo lingine ni la Bundi (Owl)
• Umbo lingine ni la Nguo nyeusi isiyo na mwili
• Umbo lingine ni la Ndoano au Mundu
• Umbo lingine ni la mti wa Mreteni


2. Majini wa Jupiter (Mushtara) - Majini wa Alhamisi

Majini wa sayari hii wanakuwa na mwili mwekundu na umbo la kati siyo wakubwa wala siyo wadogo, mwendo wao na mwondoko wao ni wa kutisha na wa kuogopesha lakini na wapole na wanao ongea taratibu.

Wana rangi ya chuma ambayo inawaunganisha wao na Sayari ya Mars (Mariikh). Mwendo wao ni ule wa umeme ukiambatana na ngurumo za radi.

• Alama yao ni ya mizuka ya watu ambao miili yao ni kama iliyojeruhiwa na Simba.
• Umbo lao maalum ni la Mfalme mwenye Upanga akiwa mgongoni mwa Simba akimwendesha.
• Umbo lingine ni la Mtu aliyevalia rasmi Nguo za Chuma za Kivita.
• Umbo lingine ni la Kijakazi aliyevaa Taji lililopambwa kwa Maua.
• Umbo lingine ni la Ng’ombe Dume.
• Umbo lingine ni la Paa dume
• Umbo lingine ni la Tausi
• Umbo lingine ni la Nguo ya rangi ya bluu isiyokua na mwili.
• Umbo lingine ni la Upanga.
• Umbo lingine ni la Mti wa Mbuyu.

{mospagebreak}

3. Majini wa Mars (Mariikh) - Majini wa Jumanne

Majini wa Mars (Mariikh) wanakuwa na Umbo refu, Mwili Mwekundu, mchafu na hutoa harufu yenye kutia kinyaa. Huwa wanajitokeza pia katika mwili wenye rangi Nyekundu, Kahawia au Nyeusi. Wana mapembe kama ya mnyama aitwaye Ayala (Hart), kucha kama za Simba, Wanatoa sauti kama za Nyati (Mbogo).

• Mwendo wao ni kama mwendo wa moto unaowaka na Alama yao ni radi na umeme unaowaka kwa katikati.
• Umbo lao maalum ni la Mfalme aliyevalia kivita akiwa amempanda Mbweha (Mbwa mwitu).
• Umbo lao lingine ni la Mwanamme aliye na silaha.
• Umbo lao lingine ni la Mwanamke aliyeshikilia Ngao kwenye mapaja yake.
• Umbo lao lingine ni la Mbuzi Jike.
• Umbo lao lingine ni la Farasi.
• Umbo lao lingine ni la Paa.
• Umbo lao lingine ni la Nguo Nyekundu isiyokuwa na mwili.
• Umbo lao lingine ni la Sufi.


4. Majini wa Sayari ya Jua (Shams) - Majini wa Jumapili

Majini wa Sayari ya Jua (Shams) wana viungo na umbo la kati, wasiovutia na dhalimu, wana Sura nyekundu na rangi ya dhahabu iliyochanganyikana na Damu.

Mwendo wao ni mfano wa Umeme na Alama yao kubwa ni kusababisha mwenye kumuita kutokwa na jasho jingi (ambapo hii ni kawaida kwa Viumbe hivi ambavyo ni vigumu kuelezeka).

• Umbo lao maalum ni la Mfalme aliyebeba fimbo ya kifalme huku akiwa amempanda Simba.
• Umbo lao lingine ni la Mfalme aliyevikwa Taji.
• Umbo lao lingine ni la Malkia mwenye Fimbo ya Kifalme.
• Umbo lao lingine ni la Ndege wa aina yeyote isipokuwa wale ndege ambao wanawakilisha peponi.
• Umbo lao lingine ni la Simba.
• Umbo lao lingine ni la Jogoo.
• Umbo lao lingine ni la Nguo ya Dhahabu isiyokuwa na mwili.
• Umbo lao lingine ni la Fimbo ya Kifalme.
• Umbo lao lingine la mwisho ambalo kwa kweli ni la kutisha sana; ni lile la Kiumbe ambaye haeleweki eleweki vizuri na ni vigumu kumuelezea ila ana mkia.


5. Majini wa Sayari ya Venus (Zuhura) - Majini wa Ijumaa

Majini wa Sayari ya Venus wana Umbo la kati na ambalo ni zuri kwa kuliangalia ambapo sehemu yao ya juu ni ya dhahabu na sehemu yao ya chini katika mwili ni ya rangi nyeupe au kijani.

Mwendo wao ni kama wa mwendo wa Nyota inayong’aa. Alama yao ni ile inayofanana na Wanawake wanaocheza katikati ya Mduara, huku wakimshawishi na kumtamanisha Mwanamazingaombwe ajiunge nao.
{mospagebreak}

Umbo lao maalum ni:-

• Ni la Mfalme aliyebeba Fimbo ya Kifalme huku akiwa anamwendesha Ngamia.
• Umbo lao lingine ni la Mwanamke aliye Uchi.
• Umbo lao lingine ni la Mbuzi Mwanamke.
• Umbo lao lingine ni la Ngamia; ambaye huwakilisha Shetani mbaya aitwae Cazote.
• Umbo lao lingine ni la Njiwa.
• Umbo lao lingine ni la Nguo isiyokuwa na mwili ya rangi Nyeupe au Kijani.
• Umbo lao lingine ni la Mmea uitwao “Savine”.


6. Majini wa Sayari ya Mercury (Attwarid) - Majini wa Jumatano

Majini wa Sayari ya Mercury (Attwarid) mara nyingi hutokea na mwili wa Kati, Baridi, Majimaji, Unyevu nyevu. Kwa ujumla maana yake ni kusema kuwa Majini hawa wa Sayari ya Mercury wanafanana na maumbile ya Mercury (Zebaki).

Muonekano wa Majini hawa ni wa kuridhisha, ni Wachangamfu katika maongezi, wana Umbo la Kibinadamu, na wanaonekana kama Shujaa aliye na silaha.

• Mwendo wao ni kama wa Mawingu ya rangi ya Fedha. Alama yao ni kuwa wanasababisha Vitisho, Hofu na Woga kwa mwenye kuwaita.
• Umbo lao Maalum ni la Mfalme anaemuendesha Dubu.
• Umbo lao lingine ni la Kijana Mzuri wa Kuvutia.
• Umbo lao lingine ni la Mwanamke aliyebeba Kijiti cha kukunjia Uzi chenye bonge la uzi.
• Umbo lao lingine ni la Mbwa.
• Umbo lao lingine ni la Dubu Jike.
• Umbo lao lingine ni la Kunguru; Kunguru hawa hutumwa kwenda kusaidia katika Kazi za Kichawi na Kijini kwa Kuchukua Nguo za Ndani za Watu, Soksi, Vijiko, na vitu vingine vidogo dogo kama hivyo. Ndio maana katika aina nyingi za Ndege, Kunguru mara nyingi ndio huchukua vitu vya ajabu ajabu ambavyo ndege wengine hawawezi kuvichukua.
• Umbo lao lingine ni la Nguo isiyo na mwili yenye kubadilika badilika rangi.
• Umbo lao lingine ni la Fimbo, Rungu, Bakora au Gongo dogo.


7. Majini wa Sayari ya Moon (Qamar) - Majini wa Jumatatu

Majini wa Sayari ya Moon – Mwezi (Qamar) wana Maumbo makubwa, Laini, Tulivu na rangi yao ni kama wingu jeusi.
Muenekano wao ni umbo lililotuna, Vichwa vyao vina upara, Macho yao ni Mekundu na yanatoa Majimaji, Meno yao ni kama ya Nguruwe Mwitu.

• Mwendo wao ni kama Dhoruba kubwa Baharini. Alama yao ni ni Mvua kubwa inayonyesha katika Mduara.
• Umbo lao Maalum ni:-
• Ni la Mtu kama Mfalme anayerusha Mishale huku akiwa anamuendesha Swala Jike.
• Umbo lao lingine ni la Kijana Mdogo wa Kiume.
• Umbo lao lingine ni la Mwindaji wa Kike mwenye Upinde na Mishale.
• Umbo lao lingine ni la Ng’ombe.
• Umbo lao lingine ni la Swala Mdogo.
• Umbo lao lingine ni la Bata.
• Umbo lao lingine ni la Nguo isiyokuwa na Mwili yenye rangi ya Kijani au Fedha.
• Umbo lao lingine ni la Mshale.
• Umbo lao lingine ni la Kiumbe mwenye Miguu Mingi mfano wa Tandu.





SERIKALI YA MAJINI
Majini wana Utawala wao ambao ni Majini Wakuu na Majini wa Kawaida wanaopewa Kazi za kufanya na Wakuu wao, Katika Serikali yao kuna Wakuu wa Serikali, Wakuu wa Majeshi, Wakuu wa Mahakama na wengineo wengi.

Utawala katika Serikali yao umegawanyika katika sehemu Kuu mbili (2);

Itaendelea
 
Du umenifanya nijiulize maswali kadhaa hapa
Hivi hawa majini mbali na kuishi na sisi wana dunia yao ambapo wanakutana

Halafu nikajiuliza tena hivi mmoja wao akifa wanafanya matanga kama sisi?
Na mazishi yao yakoje
Ee Mwenyezi Mungu kweli katuficha mengi
 
Ngoja nikwambie kitu ndugu
Msomi yeyote akiona kitu kinampa utata huingia mwenyew katika utafiti ili ajue na aje na challenge katika mada ama kuhusu kitu cha kwanza alichokina ama kukisoma ndo maana hadi leo Da vince licha ya kuwa hayupo duniani ila watu bado wanapambana na uwezo wk
Hivyo usisubiri kila kitu uoneshwe source wew ukiwa umekaa tu bila kujishugulisha huku ukijiita msomi

Sorry kama maneno yangu yamekukwaza ila nikutaka tu tuwe sawa na hata kama utaenda kutafuta elimu hii ya uongo au kweli basi uje na nondo ili wengine wajifunze.

Mfano ni kiranga haamini uwepo wa Mungu lakini anahoja na reference za msingi kiasi kwamba hata ww unaeamini uwepo wa mungu anakuacha mdomo wazi unaishia kulaani tu tabia yake hiyo
So unapobisha kitu njoo na mbadala wake ili sote tujifunze

Hope umenielewa na wengine watanielewa
Sawa nimekuelewa
 
Sio kika unachojua wewe kiko sahihi ndo maana kuna elimu mbalimbali
Ndugu, hakuna Jini zuri au Jema hata moja.
Hebu nitajie wema wa Majini.
Jini likishirikiana na binadamu basi ni katika kufanya kazi mbaya tu za urozi, wizi uhalibifu, vifo, magonjwa nk.
Hao wanaopata pesa za majini zinaambatana na masharti mengi ya kuumiza, kama kutoa makafara ya watu au wanyama wa kula, kutumia hizo hela kwa kufanya uhalibifu, unakuta mtu tajiri lakini haruhusiwi kutumia hizo pesa kwa maendeleo yake, anakatazwa kulala kitandani, kula nyama, kuvaa vizuri nk.
Na mwisho wake anakuwa chizi au kufilisika kabisa.
Ni utajiri wa mauzauza tu ili yakuingize kingi kwenye himaya yao na yaishie kukutesa.
Huyo anayeyajua Majini utakuta hawezi kujinufaisha na hayo majini, na kama hana uwezo wa kutafuta pesa yeye mwenyewe basi anakuwa masikini wa kutupwa.
Ikisemekana Jini ni Jema tusisingizie huo wema yanamtendea Mungu kwani sisi hatuuoni.
Ili kujua wema wa Majini hebu tuweke hapa kama yanashirikiana na binadamu yanamnufaishaje huyo mwanadamu.
Siku moja kuna mtu alipandisha Majini eti yakawa yanadai yaletewe Ubani na Udi ili yafukiziwe moshi wake na pia yachinjiwe kuku ili yale damu yake,
Kuna jamaa mmoja akayaambia, "nyie majini kwanini msifuge hao kuku ili mkitaka damu mchinje na mnywe wenyewe "
Kwanini pia mnapenda kukaa kwa watu masikini ambao hawali sana kuku, badala ya kukaa kwa matajiri wanaokula kuku kila siku na nyinyi muambulie mchuzi " yakabaki nanachimba vimikwala tu
Jini ni kiumbe dhifu sana ukulinganisha na binadamu, Binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu na kupewa mamlaka ya kuitawala dunia. Jina hana mamlaka hayo ndio maana dunia inajengwa na binadamu na sio Majini.
Kuna siku moja jamaa alipandisha Majini eti yanadai yaletewe Bia ya Safari ili yanywe, tulicheka hadi nusu tuzimie, Jini hana uwezo hata wa kugema Ulansi au Pingu au Mnazi.
Binadamu anapoenda kuomba msaada kwa Jini, Jini mwenyewe huwa kwanza anamshangaa sana huyo binadamu.
Ni sawa na mtu mzima mwenye afya bora anaenda kumwomba msaada mtoto mdogo abebe mzigo mzito ambao huyo mtoto hawezi hata kuunyanyua.
Jini ni viumbe dhifu mno vinaishi kwenye mazingira magumu sana hayawezi hata kujenga makazi mazuri ya kuishi, yanaishi kwenye mapango, baharini kwenye baridi kali, jangwani joto lao mvua yao baridi lao, kwenye vichaka, kwenye mahame, chooni, nk
Binadamu usiogope Jini hata siku moja, haliwezi kukufanya chochote zaidi ya kukutishatisha ukiliendea linakimbia ukiogopa linakucheka.
Jini ni sawa na uchafu tu.
A Shit Hole.
 
Back
Top Bottom