Ukisafiri kula hivi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,657
698,408
Kuepuka usumbufu wa kwenda kujisaidia unaposafiri pata huu mlo...!

Mayai mawili tu ya kuchemsha na malta moja

Mlo huu utakusaidia pia kama bajeti inabana kwakuwa hutaumwa njaa wala hutasikia kiu kwa zaidi ya masaa kumi
 
Mayai ya kichemsha nasikia huwa yanaleta mvurugano kabisa

plus ushuzi kwenye basi unaweza kupitiwa na usingizi kumbe huku

unatoa mashuzi ya kufa mtu
 
Hahaha, kwa wenzangu na mii mayai ya kuchemsha epuka, tena pisha mbali! Kama tumbo lako hauliamini jaribu kula vyakula vikavu na visivyo na mafuta, kama biscuits, crisps zilizochomwa vizuri, karanga za kukaangwa, kunywa na energy drink nzuri upendayo, maji usinywe ya kuzidi...pia ni nzuri kubeba pipi mints mbili tatu. Jamaa yangu alinichekesha alipanda basi na dada mmoja "sister duu", kamsalimia amemwangalia kwanza kama sekunde 10 halafu akamjibu "salama" na kugeukia upande wa pili kama vile ana"mboa" flani hivi. Jamaa akachuna safari ikaanza, dada wa watu akaanza kufakamia vitu njiani, mara nyama ya kuku, chipsi, mayai, apple, malta, maziwa fresh, yoghurt....kila kitu kwake yeye pwani; kona na milima ilipoanza balaa ndiyo lilianzia hapo........!:evil:
 
Kuepuka usumbufu wa kwenda kujisaidia unaposafiri pata huu mlo...!
mayai mawili tu ya kuchemsha na malta moja
mlo huu utakusaidia pia kama bajeti inabana kwakuwa hutaumwa njaa wala hutasikia kiu kwa zaidi ya masaa kumi

sidhani kama hii ni njia nzuri.. specify aina za safari, modes of transport nk..

kwa jinsi wewe ulivyoweka hapa, umegusa tu barabara na carrier units ambazo ni mabasi tu..

njoo tena kiundani..
 
kuna siku nikula mtindi then nikafakamia mahindi ya kuchoma. I will never forget that day, nilipata mateso ya hatari baada ya tumbo kujaa gesi
 
Sio dhambi ila pata picha unachia kitu kwenye Marcopolo full Kiyoyozi ? Duh!

Kifupi mimi huwa sili nakunywa mAji tu!, Ila ikibidi ni Nyama ya Kuchoma au Kukaanga tu.
Ila angalia unaweza ukala Mbwa au Kibudu.

Mkuu si unapumua lakini humo kwenye kiyoyozi
 
Huwa napenda sana Karanga za kukaangwa,maji na Azm Malt, Zaid ya karanga nawza Chukua Kaukau,
 
Back
Top Bottom