Ukisafiri kula hivi

Kuepuka usumbufu wa kwenda kujisaidia unaposafiri pata huu mlo...!

Mayai mawili tu ya kuchemsha na malta moja

Mlo huu utakusaidia pia kama bajeti inabana kwakuwa hutaumwa njaa wala hutasikia kiu kwa zaidi ya masaa kumi
nikweli mayai mawili ya kuchemsha,karanga za kukangaa pakti mbili,mwindi wa kuchoma mmoja,na chungwa moja kisha maji ya kunywa hakika safari itakuwa nzuri
 
Hahaha, kwa wenzangu na mii mayai ya kuchemsha epuka, tena pisha mbali! Kama tumbo lako hauliamini jaribu kula vyakula vikavu na visivyo na mafuta, kama biscuits, crisps zilizochomwa vizuri, karanga za kukaangwa, kunywa na energy drink nzuri upendayo, maji usinywe ya kuzidi...pia ni nzuri kubeba pipi mints mbili tatu. Jamaa yangu alinichekesha alipanda basi na dada mmoja "sister duu", kamsalimia amemwangalia kwanza kama sekunde 10 halafu akamjibu "salama" na kugeukia upande wa pili kama vile ana"mboa" flani hivi. Jamaa akachuna safari ikaanza, dada wa watu akaanza kufakamia vitu njiani, mara nyama ya kuku, chipsi, mayai, apple, malta, maziwa fresh, yoghurt....kila kitu kwake yeye pwani; kona na milima ilipoanza balaa ndiyo lilianzia hapo........!:evil:

Malizia uhondo huo acha roho mbaya mkuu CYBERTEQ
 
Hapo ni bia zangu 3 za kopo na mbuz aliyekaushwa vizur na maji chupa mbili kubwa.
 
Kuepuka usumbufu wa kwenda kujisaidia unaposafiri pata huu mlo...!

Mayai mawili tu ya kuchemsha na malta moja

Mlo huu utakusaidia pia kama bajeti inabana kwakuwa hutaumwa njaa wala hutasikia kiu kwa zaidi ya masaa kumi

aisee mi nikila mayai ya kuchemsha safarini ndo natibua tumbo kabisaaa
 
Back
Top Bottom