Ukipima DNA ukakuta mtoto si wako utafanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukipima DNA ukakuta mtoto si wako utafanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Magezi, Jul 10, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wakuu nimeona taarifa kwenye gazeti la Nipashe kuwa nusu ya watu waliokwenda kwa mkemia mkuu wa serikali kupima vinasaba (DNA) ili kujua uhalisia wa watoto wao wamekuta si wao.

  Sasa nikajiuliza kama ndo limenikuta/limekukuta utafanyaje?
   
 2. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mwanangu wala usiombe likukute. Hi hatari kuliko tufikiriavyo. Hatusemi vibaya dada zetu ila tumezidi kubambikiwa watoto. Kuna doctor mmoja alifariki majuzi huku Norhern Zone. alikuwa na secretary wake, akampa ujauzito, walipostukia wakamwozesha kijana wa watu fasta. Kasheshe ilikuja pale Dr alipokufa, dada akaanza kuhaha oooh mtoto wa Dr, alikuwa wake na mambo meeeeeeengi hakujali hata ameolewa. Mwisho kijana naye kasusa hataki tena mke. Hata ile sheria ya kikristu "ALICHOUNGANISHA MUNGU MWANADAMU ASITENGANISHE" hataki kusikia.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Unabwaga manyanga...au nimekosea??
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  IMO, Mungu haunganishi uongo, hivo hiyo ndoa is and was NULL. Kijana namuunga mkono.
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Ntafurahi kwa kupewa mtoto wa bure ila itabidi matunzo yawe kwamama yake na huyo mwenye kiumbe chake.....kwani huwa hujisikii raha kununua ng'ombe mwenye mimba???

  In fact, Nitamtimua au nitamzalisha wengi zaidi nikomkomoe
   
 6. doup

  doup JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  wote mama na mtoto warudishe kwa mwenyewe. huo ndio ubinadamu ukiokota cha mtu mrudishie
   
 7. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2010
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mkuu kipimo chochote hutakana na hisia. Na unapopima kuna majibu aina mbili tu. Aidha mtoto ni wako au Sio wako. Sasa kwa kulitambua hili mtu anaeamua kupima DNA anatakiwa awe tayari kwa amjibu yote mawili coz akiwa ni mtoto wako then utakuwa umefanya damage kubwa sana kwa mama incase ni mkeo na itachukua muda mrefu sana kulisuluhisha suala lenu na kama sio then utakuwa umepata pigo kubwa sana na huenda ukafanya maamuzi yasiyofikirika kwa hasira/kuchanganyikiwa.

  Ushauri wangu mimi ni kwamba pima tu pale ambapo wewe mwenyewe utakuwa tayari kwa kupokea majibu ya aina zote mbili!
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ati?? lol
   
 9. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,994
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Wengi wetu jibu ni kumwacha Mwanamke. Mtoto je?Ambaye naye victim wa udanganyifu kama wewe na labda umeshakuwa nae kwa zaidi ya miaka mitatu na mmebond,utajiangalia wewe mwenyewe (selfish) na utataka kumsikia?
   
 10. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hili ni Balaa ambalo yatupasa kumuomba mungu atuepushe nalo....ila mi sioni kwamba kuna haja ya kupima DNA kwa kumshirikisha mama wa mtoto....unaweza pima ukiwa tayari kwa majibu pasi na kumshirikisha mwenzio na ukiwa na majibu tayari ndo waweza muuliza mwenzio juu ya swala hili na mostly utamuuliza baada ya kuapata majibu hasi...otherwise keep living and achana kabisa na mamo ya hiki kipimo....
   
 11. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,994
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Hili swala lina pyschological effects kubwa sana kama depression,paranoid,substance and alcohol abuse...ukishamzalisha kuna uwezekano mkubwa kuanza kujirudia akilini au wakati akiwa na mimba kuanza kufikiria sio ya kwako tena... Akichelewa kurudi nyumbani au akiwa anaongea na mwanamme mwingine it will cause suspicious.
  Jibu ni kumwacha mwanamke na kukubali kumwangalia mtoto kama umeshakuwa nae kwa muda mrefu.
   
 12. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #12
  Jul 10, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kuna baadhi ya wakati watoto hubadilishwa hospitali, jee utamlaumu nani?

  Yupo mama mmoja namfahamu tukifanya kazi ofisi moja siku zote alikuwa akidai mtoto wake amebadilishiwa na hata alikwenda hospitali kulalamika lakini hakuna aliyemwelewa including her husband. Alikuwa tayari kuwapeleka mahakamani lakini familia haikumpa support na hivyo alishindwa kwa kukosa ushahidi. Ni miaka ile ya mwanzo wa tisini hakukuwa na vipimo vya DNA.

  Kwa bahati mbaya anaifahamu hiyo familia ambayo "walibadilishana" watoto maana walijifungua wakati mmoja na walikuwa wao wawili tu. Sasa alitaka kuchanganyikiwa maana hwenda mpaka karibu na kule kwa familia nyengine ili amuangalie yule mtoto anayesema wa kwake, lakini jamaa wakamstukia na walikuwa wanamficha kwa kuhofia atamuiba siku moja.

  Kwa vile nimehama ofisi ile sijui yule mama kama amepata guts za kwenda kupima DNA ya mtoto.
   
 13. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hii nayo ni mbaya sana, na inaumiza kwelikweli. Ule wakati wa kujifungua na muda baada ya kujifungua inatakiwa wahusika kuwa makini sana pamoja na manesi. Kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kubadilishiwa mtoto.
   
 14. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ni uamuzi mugumu sana kuukubali lakini inakubidi uamue kulingana mazingira yaliyopo kwa wakati husika..hapo ndo unaweza kutoa jibu muafaka.
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hakukuwahi kuwa na Ndoa hapo, so kijana yupo huru kabisa, na sisi Wakristo hatutumii Neno kuvunja ndoa kwa Sababu katika Mazingira kama hayo hapo hakujawahi kuwa na Ndoa, that the marriage was VOID, Kijana amtafute mtu Mwingine ampeleke kanisani ili Mungu awaunganishe
   
 16. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  A man is entitled to have his doubts if its outside the wedlock hell yeah DNA all the way. Lakini at one point a man is supposed to be a man and nothing else, sasa unataka DNA ya nini wakati hupo ndani ya wedlock? Kama unataka proof your wife betrayed the marriage and you wish to separate if you can get the evidence yeah go ahead. Lakini kama unania ya kubaki na mkeo na kuendeleza ndoa, mtoto wa kiume huna budi zaidi ya kukaa kimya na uweke doubt aside na ulee mtoto.

  Sometimes its not good to know too much, si ajabu matokeo yake wengi wamekuta watoto si wao. A man is supposed to live by his decision una nia na ndoa yako shut up na toa mashaka hata kama if the kid appears doubtful, if you feel betrayed and wish to end the marriage ukipata ushahidi, well then DNA should come into play.
   
 17. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Nani atawalea??
   
 18. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Unanyamaza.... Mnaendelea na maisha...

  Ukiamua kupima unatakiwa pia kuwa tayari kupokea majibu na kukubaliana nayo... kama huna kifua seek counselling au ahirisha zoezi... in jesus name!!..:amen:
   
 19. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Kitanda hakizai haramu Mkuu.
   
 20. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #20
  Jul 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mimi binafsi nitakubali matokeo, na nitalea mtoto kama halikutokea jambo lolote linalo uhusiana na DNA.
   
Loading...