Ukipima DNA ukakuta mtoto si wako utafanyaje?

Hivi mpaka mkeo anaamua kukuibia na kuzaa na mtu mwingine inakuwaje? maana tusing'anga'anie tu kujadili matokeo apa.....mpaka hilo linatokea unakuwa ulikuwa wapi? ina maana kuna sababu na nadhani ni vema ku deal na hizo sababu zinazopelekea tatizo hilo.....
Maanake tabia za ngono kwa wanaume haziwaumbui kwa sababu hawapati mimba...kama unaleta longolongo katika ndoaadhabu ni moja tu....ulee watoto wa jirani yako tehe tehe.....kuna watu wanatoa unyumba kwa wake zao kwa kipimo kwa sababu miguvu yote anaimalizia kwa hawara.....unategemea nini weewe mwanaume mwenye choyo?

mix with yours
mke ni
 
Wakuu nimeona taarifa kwenye gazeti la Nipashe kuwa nusu ya watu waliokwenda kwa mkemia mkuu wa serikali kupima vinasaba (DNA) ili kujua uhalisia wa watoto wao wamekuta si wao.

Sasa nikajiuliza kama ndo limenikuta/limekukuta utafanyaje?

..This is too hard..marekani naonaga kwenye shows watu wanajitolea kupima live.......matokeo wengi hushindwa kuyabeba....

kwa hali ya tanzania mkemia mkuu anakuambia kuwa asilimia 50% tangu wameanza kupima ...wamebambikiwa watoto.....so hili tatizo ni kubwa ....sana ..ni wazi kuwa inawezekana sample size yao ikawa kweli na ukakuta asilimia 50% ya kinababa labda tunalea wana si wetu!!!!!
Huu ni momonyoko mkubwa wa kijamii ...wote wanaume kwa wanawake wamekuwa malaya...lakini kinadada chonde chonde...msifanye usawa kwenye hili ..kwani matokeo ya mwanamke kuwa na mpenzi nje ni kumzalia mumewe mwana wa nje[sipendi kutumia jina mwanaharamu ,kwani hana kosa]......nadhani hata dini ya kiislamu inapotoa adhabu kubwa kwa mwanamke anayekamatwa na zinaa kuliko mwanamke ....pamoja na kuwa sikubaliani na aina ya adhabu ni wazi inatokana wao kuangalia mazilla ya mwanamke kuwa na wapenzi wengi....

sasa ufanye nini ukigunduA?.....inategemeana kama mtoto mwenyewe ndio huyo huyo ..huna budi kumuacha mkeo..huo ni ushahidi ambao hata kama ni ndoa ya kikatoliki iliyo ngumu kuvunja wanakubali...lakini mwanamme baada ya hapo lazima akubali mfadhaiko mkubwa na mwanamke anaweza jitetea kuwa alienda nje kwa kuwa wewe hukuweza kumzalisha....ambapo jamii ya sasa itamuamini na kukuacha wewe mwanamme na aibu zaidi....hapo ndio maana wengine huvumilia ...na kujitahidi kujitafutia mtoto wa halali ....na ikitokea amempata nje ya mkewe basi huwa na kifua cha kumtosa mkewe ......na ataungwa mkono...kwa kuwa tayari ana mtoto mkewe hatakuwa na utetezi....

ikiwa mkeo ameteleza na labda kati ya watoto wannne ametokea mmoja si wako.....wengi humalizana kiutu uzima...kwani mwanamume huangalia zaidi welfare ya wale watoto wake watatu na kuamua kuvumilia......lakini hii humnyima mwanamke haki ya kumuuliza mmewe lolote kuhusu ..mahusiano!!!

Tukiangalia historia miaka ya nyuma hapakuwa na utamaduni wa kuangalia mtoto au kumchambua....mtoto akishazaliwa wanasema ..kitanda hakizai haramu......,hakuna ambaye wala alidhubutu kutuhumu ..hilo..unless mwanamke hakuwa na mme au ni mjane na hakuolewa tena...hapo watajiuliza na alitakiwa kutoa jibu!!!....tena wazee wa zamani ....akisikia mtu amemzalisha mkewe wala hakuwa na hasira ..ukizingatia watu walikuwa na wake wengi....atasema tu kuwa umemsaidia kulima shamba ....yeye anavuna!....kimsingi watotot ulikuwa utajiri[mahari -wakike],nguvu kazi....[wakiume]....watu walitamani wake zao wazae kila mwaka sembuse kuanza kuchambua nasaba!!!

siku hizi pia maisha ni gharama so ukizalisha mke wa mtu mwanamume anaumia mengi ..ikiwemo mateso aliyoyapata kulea mimba ya mkewe,kumtibia wakati wewe umetulia tulii...gharama za malezi ,masomo na mengineyo...alafu ndio aje asikie kabambikiwa lazima apagawe!!.
 
hili la DNA limewagusa wababa eeeh,naona wanawake tunanyooshewa kidole....wakati we share equal rensposibilities!...hizo mimba hazikupatikana kny miti,men are involved!
 
Tatizo si kuwa tatizo wanaoenda kupima wote ni wenye mashaka yanayokaribia ukweli
sampo mbovu
mix with yours
 
Takwimu za DNA ziko biased mno! Mtoto kama anafanana na mimi ya nini kwenda kupima? Mtoto kama sio wako you just feel it! wanaoenda kupima ni wale enye mashaka! Mtoto eti anafanana na jirani yangu hapo mwana nitapima hata kama mara tatu! utafikiri napima ngoma!
 
sijui huwezi kutoa maamuzi nadhani itaegemea na factor mbali mbali.

  1. LOVE-Obvius kitendo cha kuchukua uamuzi wa kipma DNA ina maana penzi limelega lega . lakini Je ni yeye unahisi kabadilika hana mapenzi nawe tena ? au ni tetesi lakini bado anakupenda kiukweli ukiondoa hilo kosa
  2. Dini- Imani ya dini inaweza kuwa na ushawishi. Sijui kwa Muslim/ christian sheria zinasemaje
  3. Timing- unaenda kupima DNA mtoto akiwa na umri gani? Je kulikuwa na gap yakuwa mbali na mwenzako kwa muda mrefu kwa wakti fulani baada ya kupata mimba. Je unawatoto wengine na huyo mke au ni huyo 1ja tu ?
  4. Faithfulness na utu - Je wewe mwenyewe huna mtoto nje ambaye ulimficha mkeo? Hujawai kuwa na mahusiano nje na kulazmisha mtu atoe mimba wakati ukiwa kwenye ndoa?

Its complicated situation to be in lakini nadhani unatakiwa ku consider factor nyingi hata zaidi ya hizi nilizotaja
 
Kwanza kabisa unapoamua kupima DNA tayari unawasiwasi na jambo fulani. DNA ni kuthibitisha au kutothibitisha hoja yako. Kwa mantiki hiyo matokeo ni 50/50 na hili huhitaji counseling kwasababu kama mna aminiana hakuna haja ya DNA, ili kutoishi na walakini ndio maana ya kupima na uwe tayari kwa matokeo. Huna sababu ya kumpiga au kumdhuru mkeo. Prepare yourself psyachologically.
Pili, huyo mchangiaji anayeshauri kuwa mimba inatunga mkiwa mbali mbali si kweli. Unaweza kuwa na mkeo 24 hrs,laikini zile dakika 5 atakazo kuwa nje na mwizi zina umuhimu sana, kwasababu kama ni right time, right shot in right place, deal done! kwahiyo DNA haiitegemei mumekaa mbali kiasi gani bali mna aminiana kiasi gani.
Tatu, ukikuta DNA ni mushkeli basi huyo mtoto si wako. Kama una watatu wapeleke wote wakapime ili kutoishi na walakini kwasababu hatari iliyo mbeleni ni kutowatendea haki kwa hofu tu. Kwa matokeo yoyote inabidi uwapende watoto [unconditional love] kwasababu wakati mama yao anafanya mauza uza hawakuwepo na wewe ndiye baba yao wanayemjua. Ina haribu watoto kisaikolojia wanapoanza kutambua mambo kabla ya wakati. Endelea kuwapenda watoto na ukubwani waambie ukweli. Hii haina maana hawatakujali, hapana watakuthamini sana kwa uelewa wako. Kama mkeo atawaonyesha baba yao ni yupi basi umenawa mikono.
Mwisho,je mtaendelea na mapenzi? jibu hapa linategemea nyakati. Zamani ingewezekana, lakini zama hizi za magonjwa ni wazi kuwa si watotot tu bali mkeo anaweza kuwa amekuletea kasheshe kwasababu kuna ushahidi kuwa yeye na kibaka hawakutumia kinga[ ingawa hii si hoja kubwa kuliko uaminifu] na wala haihalalishi ujinga nje ya ndoa, lakini mantiki hapa ni kuwa huyu mwanamke atakuweka kwenye matatizo makubwa kuliko ya DNA, kwahiyo kwa ushauri muachane kwasababu hakuna love wala uaminifu.
Kuhusu dini zinasemaje, mimi ni mtaalamu wa mambo ya afya kwahiyo wataalam wa mambo ya dini wana majibu mazuri.
Ahsante
Nguruvi3 [ medical prof]
 
Wengi wa wale waliokutwa watoto siyo wa wanaume "husika" ni wale wenye mahusiano tata au wenye migogoro kuhusu mimba na watoto.Ukichunguza sana utaona kuna zaidi ya kinachojadiliwa hapa na mimi naongea kama mwanamke.Hali zifuatazo zinajitokeza zaidi:
1. Watoto wanaozaliwa na wazazi wasio na ndoa - Hawa ndio percent kubwa zaidi - kati ya asilimia 70 - 100 - baba amekuwa na mahusiano yasiyo rasmi mfano yuko kwenye ndoa na bado anatembea nje bila kinga.Sasa wewe baba una mke/familia bado unatembea ovyo tena bila kinga unatarajia nini? Si bora mtoto si ungeweza kuokota UKIMWI?
2. Wana ndoa wenye migogoro isiyoisha.Hawa ni asilimia isiyozidi 20 - 25 - Hapa napo kuna mambo mengi yanayochangia kuzaliwa watoto wenye utata. Sasa kwanini hamtatui migogoro yenu kabla ya kuendelea kuzaa?
3. Wenye ndoa wasio waaminifu hasa kwa mwanamke - hii ni per cent ndogo mno chini ya asilimia 5

Likikupata ndugu yangu utakachoweza kufanya itategemea uko katika kundi lipi hapo juu.
Kundi 1. Ni ushahidi tosha kuwa mtoto siyo wako hivyo hulazimiki wala huwajibiki kitu. Anza mbele
Kundi 2. Hapa itategemea mahusiano na mara nyingi mpaka mwende kwenye DNA basi ndoa ina migogoro inayoweza kuvunja ndoa
Kundi 3. Rejea 2 hapo juu.
 
Inategemea kuna watu wenye moyo mkuu wa hekima na ujasiri wanaweza kutoa maamuzi ya hekima.
Lakini kuna wengine kama yule baba aliyesubiri Binti akakua akaanza kumtafuna:A S confused:
 
Wakuu nimeona taarifa kwenye gazeti la Nipashe kuwa nusu ya watu waliokwenda kwa mkemia mkuu wa serikali kupima vinasaba (DNA) ili kujua uhalisia wa watoto wao wamekuta si wao.

Sasa nikajiuliza kama ndo limenikuta/limekukuta utafanyaje?

Magezi, kwa mkemia wanaenda watu wenye disputes. Kwa hiyo hizi takwimu haziwezi kutoa hali halisi ya kile kinachoendelea kwenye jamii. Hilo linaweza kujulikana endapo itafanyika population survey. Kwa hiyo watu washishangae kwa hizi takwimu.

Ila kama mtu aliamua kwenda kumpima mtoto anashangaa nini majibu? Ni kama vile inavyokuwa kwenye VVU!
 
Mimi ninaona kama ikitokea itabidi ujiulize je umeenda kupima kwa ajili gani maana uwezikwenda kupima bila sababu aidha ndani ya nyumba vuvuzela kaishalikoroga mwisho unasema ngoja nikapime DNA,kwakuwa ushaona mtoto kama mpemba simpemba msomari simsomari vyovyote vile!asikudanganye mtu mwanao utamjua na uwezikumtilia mashaka!!Kwahiyo ikitokea umeenda kupima maana yake unaji!!plan A na Plan B,Plan A nikwamba kama mtoto niwako nikwanda kumuomba msamaha mke!Japo hapo lazima kunakuwepo naugomvi mpaka mnafikia maamui kama hayo!!Plan B Nikikuta Mtoto siwangu Mama umeona??Mama ndiyo! je hapo tufanyeje??Mama mimi nakusikiliza wewe maana mim sijawahikutoka lelerile......blabla nyingi!!Unamwambia sawa lakini huyu mtoto hana makosa mimi namchukua nitamlea na wadogozake au kaka zake kama wangu ila ufahamu kuwa huyu simwanangu!!Mkirudi nyumbani na mkaka kama mwezi wee binafsi utajisikia vibaya namwisho utajiridhisha kwakusema hivi..Hivi vipimo vya wazungu saa yingine vinasema uongo mwisho unamuon kama wngine naunrudisha mapenzi kwa mkeo mnasahau nakama umesahau usij ukangombana naye ukakumbushia mtoto utakuwa ujamtendea haki mtoto!!Mpende mtoto!!Nawala usifikirie kumfukuza mke na mtoto!!!Mtizamo binafsi.
 
Yeyote anayekuita Baba toka moyoni ni mtoto hata kama si wewe uliyempa mama yake mimba. Tatizo la Waafrika mtoto mpaka atoke viunoni, kwani ni wangapi wana "adopt" watoto. Hivi mwanaume wa kiafrika aliyefikia cheo cha Uraisi kama Bill Cliton angekuwa na mtoto mmoja wa kike na bado uume wake unafanya kazi angevumilia kweli kubaki na huyo mtoto mmoja wa kike?
 
Hapo mzee utachemsha utabwaga majanga kwa wangapi?mbona hilo ni jambo la kawaida km wewe bado kua uyaone hayo ndio maisha,mbona hata mababa na mama zetu wanalijua hilo na walikukimezea kwa mengiii....maana hata wewe mwenyewe tafakari kuna familia zingine watoto wanne hawafanani hata kidogo...Hapo utaambiwa anafanana sana na Ba mdogo alifariki siku nyingi...au mjomba wa Sikonge...Kua uyaone Siri ya mtoto haijuae ni Mama...na wanasema wahenga usimchunguze bata hutashindwa kumla..na usilolijua halikusumbuiii.Kwa taarifa yako wengi walio kwenye ndoa wananyumba ndogo either mwanamke au mwanamme,tena unakuta relationship za siku nyingi kabla yakooo watu wanaziendeleza..
 
Mkuu unachosema ni kweli kabisa. Kuna ma-bastards wengi sana Tanzania (yaani wale waliozaliwa nje ya ndoa na watoto haramu) kwa hiyo ni lazima tukubali kuishi kwenye mazingira hayo. Kuna generation kubwa sana ya bastards na wenyewe nao wanaendelea ku-produce bastards
 
Jamani naomba kuuliza, hivi nyie hata siku za mimba hamjui? Wanaume mkajifunze siku za wenzenu othewise mtaletewa watoto wasio wenu. Mie najua siku, saa niliyodaka mimba na wanaume wengi wako makini na hilo iweje leo wewe uende kupima DNA.

Ikitokea ni ujinga wako, lea mtoto ili ukae na mama au fukuza mama aondoke akalee mwanae.
 
Wakuu nimeona taarifa kwenye gazeti la Nipashe kuwa nusu ya watu waliokwenda kwa mkemia mkuu wa serikali kupima vinasaba (DNA) ili kujua uhalisia wa watoto wao wamekuta si wao.

Sasa nikajiuliza kama ndo limenikuta/limekukuta utafanyaje?

C Utatafuta wa kwao.... The real kid from another mother....... garbage in......... garbage out
 
Back
Top Bottom