Ukipenda kweli ukatendwa au kuachwa utafanyaje?

Ukipenda kweli ukatendwa au kuachwa utafanyaje?

Ukiwa katika wakati kama huo huwezi fikiria utakujakupenda tena, kila jambo linaamuliwa na muda upe muda nafasi yake, baadaye utakuja kushangaa ilikuwaje ukapenda kiasi kile.
 
Mshukuru Mungu kila jambo linalotokea lina sababu ktk maisha yako, Mungu alipanga upitie hayo jipe mda utasahau.
 
nikiwa chuo nilikutana na mtoto mmoja mzuri kinoma nikashoboka akanielewa, tumeenda weee tukiwa mwaka wa tatu semester ya mwisho mwanzoni akadai eti amefanya uchungzi amegundua ninavuta bangi nichague moja kati ya bangi au yeye na kuanzia siku hiyo nisifike chimbo kwa washkaji, nikachagua bangi alichofanya ni kugeuka na kuondoka iliniuma ila na mimi nikaona usenge nikampotezea, nikaanzisha harakati kwa room mate wake yule demu alipogundua mwenyewe akajirudisha ila baadae tuliachana kwa amani na hadi sasa ameolewa ila akimiss show ananitafuta kama kawa!
 
Habari wakuu. Natumaini hamjambo.......


Hivi..
Ukipenda na ukazama kweli. Na siku ikatokea ukaachwa au ukatendwa na umpendae ambaye tumaini lako lote lilikuwa kwake.... Utafanya nini ili uzimudu hisia Kali za maumivu?..

Kama imewahi kukutokea tushirikishe ulifanyaje .....

Aiseh kimbilia kwa Mungu.faraja utakayoipata sio ya nchii hii huwezi amini.

Mimi imenisaidia sana ingawa ilichukua muda kufanya maamuz ya kumkimbilia Mungu
 
Cha kwanza itabidi ukubali matokeo,,, pili ujichunguze wapi ulikosea ufanye marekebisho ,,, tatu usikurupuke kuanzisha mahusiano mapya wakati yule bado unampenda ni kwa vile umeachwaaa

Hii ni kweli aise.ila sema sio wote tutajichunguza huwa tunaishia kulaumu tu
 
Nilicho mpa nilimpa ila kumkopesha kwa sababu kuna biashara alikuwa anataka kufanya ndio akaniomba nimkopeshe unajua mapenzi sio sio kujamiiana mkiwa wawili mnabadilishana mawazo nini mfanye ili msongeshe maisha mbele nilimkuta na ali mbaya ya kimaisha lakini nilivyo kaa nae nikamsikiliza alikuwa na mawazo ya kimaendeleo mwanzoni alifanya vizuri sana ila wamawake wandanganyika sana mimi nilijua kajazwa maneno yakamuingia ila hakufikilia mbele kawaza alipokuwa leo mumgu kasha mpiga bakora biashra kafunga katuma watu kuniomba msamaha nimemsamehe ila nimemwambia mapemzi kwake sitaki nikamuongopea nimeshapata mwingine siwezi kurudi kwenye mausiano nae kiukweli sina mtu ila nataka nimpunguze speed lakini hakomi

Aise pole mkuu..wakati mwingine sis wanawake tunashindwa kuchanganua mambo nafikir na hii ni kwa sababu tunaongozwa sana na hisia kuliko uhalisia.

Mungu akupe hitaji la moyo wako.ila usiwe na haraka jipe muda kwanza

Aiseh maumivu ya mapenzi huwa hayaelezeki kabisa
 
Kuachana kiroho safi kupoje mkuu?

mfano huyo X wako alianza ku flirt na wanaume wengine wakat bado mpo kwenye mahusiano, hatimaye ikabid muachane, Hapo utasema mmeachana kiroho safi au vip ?
Hapo ni mwendo wa buyu la milele, yani demu wangu aanzishe mtaa wa pili halafu iwe kiroho safi!?
 
yani nitakacho fanya ni kumpaa hela tu maana najuaa ndo ugonjwaaaa waooooo #we mpe hela hela yani mpe helaaa
 
Naona Maleta uzi umaniumiza sana nilimpenda mpnz wangu nilitamani nifanyie kila jambo atakaloniambia na mengine nilifanya nilimfungulia biashara nikampangishia nyumba mzazi wake akiumwa namtibia lakini alinigeuka mpaka sasa naumia sana aliingia mausiano na mtu tunae fahamiana na kuna ela. Nilimkopesha milioni tano ili aongeze kwenye biashara yake juzi nimeifata kwa sababu mda tulio aidiana umeshapita akaniambia hana mpaka atakapo pata nyumbani nilimtimua sijui na biashara niichukue maana kaniathili kisaikorojia
Mkuu una moyo wa chuma unahonga 5 mil? Sio siri atakua alikuroga
 
Umeonaee lawamaa zote unampa mwenzio

Unajua mara nyingi sana mtu ukishaumizwa,hata kama kosa lilikuwa lako ni lazima utajiona kuwa wewe ulikuwa malaika hukosei.ila ukija kukaa na kutafakari,,pengine yawezekana hata wewe unaenlaumu he/she kakuumiza kumbe hata wewe ulichangia kwa namna moja au nyingine kuvunjiaka
 
Back
Top Bottom