Mrembo Mchawi: Ukigundua mke wako ambaye hujafunga naye ndoa rasmi ya kidini ni mchawi au mshirikina utafanyaje?

Mashaurijr

JF-Expert Member
Oct 8, 2016
639
1,020
Wakuu nakuja tena kwenu nikiwa nimechoka sana. Ngoja ninywe hata juice nipate nguvu ya kuwasimulia yaliyonikuta na yanayoendelea kunikuta.

Ilikuwa mwaka jana mwezi wa 11 nilipokutana na mwanamke mmoja mrembo sana. Kwa hakika kila idara alijaliwa, makalio, hipsi, sura hakuna mwanaume ambaye asingetamani kuwa naye.

Alikuwa maeneo ya karibu na biashara zangu akiuza kiduka alichodai ni cha mama yake mkubwa. Kila siku nilijaribu kumweka karibu ila tatizo likawa sio mimi peke yangu niliyekuwa namfukuzia yule mrembo.

Ila mwisho wa siku nikaibuka mshindi mrembo akanasa, na siyo kidogo, akanasa kweli kweli kufikia hatua ya kuwa na wivu wa hali ya juu, hakutaka kabisa nikaribiwe na mwanamke mwingine yeyote.

Nilijiona mjanja sana na mwenye bahati hapo hata kumwonja mrembo ilikuwa bado. Ni kama kuna hisia zilikuwa zinanikatalia kumpeleka maskani nikajipongeze baada ya kuhangaika sana kumpata mrembo.

Nilifikiria sana kwanini naingia kibaridi na kiwoga cha ajabu kila ninapotaka kumpeleka mrembo maskani ila nikakosa jibu. Maana siyo mara yangu ya kwanza kutoka na mrembo mkali kama yeye useme ni kiwewe.

Zilikatika siku nyingi tukiwa wapenzi akionesha kabisa matamanio ya kupekwa maskani tukafanye yetu lakini mwamba bado nilizuiwa na hisia, nikikwepa kwepa kwa visingizio vidogo vidogo.

Siku ya mwaka mpya nilikunywa sana, sasa mrembo akafanya kunisindikiza akiwa na rafiki yake baada ya kukaribia maskani. Rafiki yake akamwambia anifikishe yeye anaongea na simu kidogo atamkuta, bila mimi kujua walikuwa wameshapanga tayari.

Basi mrembo akanifikisha mpaka maskani nikijua ataishia nje lakini wapi aliingia maskani, tukalala, nikampiga kimoko cha kilevi asubuhi game ndio ikachezwa haswaa. Licha ya kibaridi cha asubuhi wote tukawa tunatoka jasho mithili ya mtu anayelima kwenye jua kali.

Siku hiyo tulichelewa kufungua biashara mpaka tukazua minongono mtaani. Wakijiuliza na kujijibu wenyewe angali sisi wenye majibu kamili tukiwepo.

Sasa baada ya hapo ikatokea mtafaruku upande wake baada ya mume wa mama yake mkubwa kuanza kulazimisha mapenzi kwa mrembo bila yeye kutaka, vitendo hivyo vilimfikia mama mkubwa wake na kuamua mrembo arudi kijijini. Tena akimfukuza usiku na mrembo hakuwa na kwakwenda akaniomba aje alale kesho yake aondoke.

Kweli mrembo alikuja lakini hakuondoka tena, akakaa na mimi mwezi wa kwanza ukaisha salama japokuwa nilianza kumgundua ana mambo ya giza ndani yake, tuseme mapepo, ila sikuamini kama ni mchawi.

Mpaka juzi mdogo wangu alipougua nikashtuka sana, nikaanza kuwa mtu tofauti, nikaanza kumwomba Mungu. Hapo ndio nilipoanza kuoneshwa matendo ya ajabu ya mrembo niliyeishi naye kama mke.

Alikuwa na mizimu ya kichawi ndani yake, alikuwa akifanya mengi kwa kutumia uchawi wake bila mimi kujua. Hata usiku nikishalala yeye hubaki kama boshen tu ila nafsi yake huondoka kwenda kwenye vikao vya wachawi usiku.

Itaendelea sehemu ya pili...

Muendelezo sehemu ya pili soma hapa
 
Ushagundua mchawi unataka ushauriwe nini sasa?? Na wewe ingia kundini basi au subiri ufanywe msukule ukalimishwe mashamba ya mpunga.

Halafu hebu jipangeni na story zenu mkitaka kusimulia. Andika kisa chote, copy paste hapa watu wasome kama wanasoma maisha yaendelee.
Haya mambo ya itaendelea kama Isidingo hayanogi kwenye kusoma.
 
Ilikuwa mwaka jana mwezi wa 11 nilipokutana na mwanamke mmoja mrembo sana. Kwa hakika kila idara alijaliwa , makalio , hipsi sura hakuna mwanaume ambaye asingetamani kuwa nae, . Alikuwa maeneo ya karibu na biashara zangu akiuza kiduka alichodai nicha mama yake mkubwa .
Kila siku nilijaribu kumweka karibu ila tatizo likawa sio mimi peke yangu niliyekuwa namfukuzia yule mrembo .
Zigo lako kufa nalo begani
 
Mungu tusaidie Me tusihangaike na Michepuko iliyomfanya Nabii Suleiman akakuasi na kuabudu miungu baali.

Alipostuka akagundua yote ni ubatili mtupu pasipo kumcha BWANA.
 
Sehemu ya pili,

Zaidi niligundua kwenye begi lake kuna kikopo kama cha mafuta ya kupaka na kingine ni kama kigololi cha pool table ila nicha alminium ya zamani sana yenye kitundu kidogo kwa juu. Hivyo ndio vifaa vyake muhimu vya kazi zake haswa ile gololi kwani aliweza kuficha mizimu aliyobeba ndani yake ili yeye mwenyewe kutojulikana sehemu anazohofia kujulikana.

Na mafuta alitumia kidogo kujipaka utosini anapotaka kusafiri na kuacha mwili boshen kitandani. Kabla ya mimi kujua yote haya nilikuwa nikiishi kihuni hivyo kujua mengi ilikuwa ngumu, lakini kabla ya kuingia kwenye uhuni nimewahi kuwa mtu wa sala maombi na imani kali ambayo ilinipa kujua Mengi na kuona mengi yasiyoonekana kawaida.

Mpaka nilipolemewa na jaribu moja kubwa sana na kilema ambacho ni siri yangu kilicho ndani yangu baada ya kuanguka kidogo tu, tayari nilipoteza imani nikaamini Mungu ameniacha. Nikaamini Mungu hatanikubali tena. Na kweli kuna baadhi ya Mambo yalianza kuharibika kutokana na anguko nilikata tamaa sana ila tokea mdogo wangu kuugua ni kama nimefufuka upya kiimani.

Sasa baada ya kuzidi kumjua mrembo mchawi naye aligundua nimemfahamu na zaidi kabla ya yeye kujua wachawi wenzie akiwemo Mama yake walimtahadharisha kuwa huenda nimemjua tayari. Kwani walishashindwa kunidhibiti. Hii kauli ilinipa nguvu sana nilipokuwa naona maono haya nikiwa usingizini.

Zaidi kulipokucha, kumcheki mrembo pembeni yangu ambaye tokea nimemjua ni mchawi sikumgusa kabisa (sehemu ya kwanza nimeandika tokea juzi maana nimeiandika jumatano aliyopita).

Nilianza kushindwa kuvumilia niliyoyajua naye pia akajua rasmi nimemjua japo hakujua namjua kiundani sana. Siku zote mchawi aliyebeba uchawi ndani yake lazima ukimshtukia ajue.

Sasa tukawa kimya kwa muda wa siku nzima hakuna aliyemwongelesha mwingine zaidi ya hapo alianza kuhangaika nikimkaribia nikawa nakaa nae mbali. Hata usiku alipoondoka kwa sasa nikawa sio chochote lile bosheni silioni tena, anaondoka mzima mzima, ila baadae nilikuja kugundua ni imani yangu imerudi vyema hivyo naona uhalisia (angekuja binadamu wa kawaida basi angeona boshen la mrembo lililoachwa hata kuligusa).

Sasa siku hiyo aliporudi alirudi kimzimu kweli alifungua mlango na kuingia kisha akagusa mafuta kidogo akaweka kwenye paji la uso nikiwa nimejifanya nimelala, akajilaza kitandani na kuendeleza usingizi.

Siku hiyo akili yangu ilinituma nimrekodi nipate kujua anaongea nini na mama yake anapobaki mwenyewe. Kweli nilifanikiwa kupata rekodi ya siku nzima baada ya kumtegeshea simu yangu moja kwenye kona moja ikiwa inarekodi. Japo aliongea kilugha na mimi na yeye sio kabila moja nikaamua kutafuta mtu anitafsirie

Aisee nilichoka sana, kwa matendo maovu wanayofanya zaidi niongelee yale yanayonihusu mimi.

Walijaribu kwa njia nyingi sana ili nipumbazike, yaani nikiambiwa kitu niwe mtu wa ndio, wanidhibiti lakini walishindwa. Wakiamini mimi pia ni mchawi na nilichukua nyota kali za watu ndio zinanilinda.

Tuache waamini hivyo huenda hata huku wengine mtaamini nililindwa na nalindwa na uchawi lakini ukweli sio huo. Mimi namwomba Mungu wa mbinguni, ndio kimbilio langu na pia sio mlokole, najaribu kuwavuta kanisani kwetu tuvute sadaka, hapana mimi ni RC until I die.

Zaidi, nilijua mrembo mchawi ni mjamzito ila ujauzito wake umefungwa kichawi na mchawi mwenzao ambaye kuwa hataki kabisa huyu mrembo azae na mimi kwani anathamani sana kwao na kuna baadhi ya mambo yao yataharibika. lakini mama yake na mrembo mchawi na wengine walitaka wamwache mrembo mchawi na maisha yake hivyo walianza kupanga namna ya kumkabili huyo mwenzao kumtwanga mpaka ashike adabu na asiingilie tena uhuru wa mrembo mchawi.

Hapo nilipata jibu la kwanini anadalili za ujauzito ila vipimo havioneshi ana mimba au hana.

Lingine walipanga shambulio la mwisho la kujaribu kunishambulia kichawi, wafanye kuja mara ya sita sasa wajaribu tena kunipumbaza, sasa mama wa mrembo mchawi akasema wakishindwa kunipumbaza waniuwe kabisa.

Mrembo alikuja juu sana na kumbishia mama yake na kuahidi kunilinda na ameruhusu kupumbazwa tu. Pia alimwambia mama yake kwa sasa anapata shida akiwa karibu na mimi, anajisikia vibaya mno, mama yake akasema hata haelewi au uchawi wangu ni mkali una mdhuru. Mpaka hapo nikawa nimejua mengi sana kuwahusu.

Sasa usiku niliporudi nyumbani nikamkuta anapika alishtuka sana baada ya mimi kuingia ndani akaishiwa nguvu na kuanza kuniomba nitoke basi nikatoka. Kama nusu saa hivi nikarudi nikamkuta kawaida.

Nikajilaza kitandani yeye akiwa akiwa anakunja nguo na kuzipanga, nikajikuta nasukumwa kumwambia nasafiri hivyo aende kwa mama yake nikirudi nitakuja kumchukua rasmi kama mke nilipe na mahari. Ikawa kama nimejiwashia moto alikataa kata kata kuondoka.

Nikajikuta nakasirika sana alipokuwa analia akilalamika kuwa namfukuza na ndio namtelekeza, nikajaribu kumshawishi sana lakini wapi.

Sasa kesho yake nikatumia nguvu hata kutaka kutoa vitu vyake nje. Akaniomba nisimdhalilishe anatoka mwenyewe kweli baadae alitoka akakaa kwa rafiki yake jirani ili kesho yake arudi mkoani kwao. Baada yeye kutoka tu nikamtaarifu mama yake kuwa mwanae hayupo tena kwangu. Kisha nikampiga block baada ya kutaka kunipigia.

Kesho yake nikiwa kazini alifanya kitendo cha kushangaza, alifungua mlango wangu kwa nguvu zake za giza na kwenda kuchukua boxer zangu mbili ili aondoke nazo ila bahati nilikuwa na mashaka hayo nikawa nimechukua ki min kamera ninacho kitega sana kwenye biashara na kukitega chumbani kwangu, hivyo tukio hilo nililiona.

Nikamfuata kwa rafiki yake kwa jazba nikamuuliza akawa anabisha mpaka nilipomuonesha video

Itaendelea ......
 
Back
Top Bottom