M45
JF-Expert Member
- Aug 20, 2015
- 1,461
- 2,320
Habari za muda huu wanadau wa JamiiAfrica? Juzi kati nilikutana na wazee wawili njiani,wakipeana ushauri wa jinsi ya kutumia hela anayoipata kwenye shughuli zake,kilichonishangaza ni pale mmoja wao alipoomba ushauri wa hela anazopata kila siku azifanyeje,Yule mzee wa pili alimjibu kwa kumwabia,ukipata hela yako kula,hakuna sababu ya kuweka hela wakati ukifariki tu, kikao cha kwanza wataanda kwanza bajeti ya chakula. Je hawa wazee walikuwa sahihi ama wana sababu zao nyingine?