Ukionewa ni sahihi kushika bunduki na kuingia mtaani kuua watu?

Nchi ilipofikia hakuna namna,tunalipo kodi halafu hatupewe huduma stahiki hakuna bunge,hakuna mahakama,hakuna serikali hivi hizo haki tukatoe wapi!!
Kodi zetu tunajichanga kuwalipa watesaji wetu ambao wamegawanywa maeneo mbali mbali kama mahakamani, bungeni na serikalini.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
To be honest dhuluma na uonevu wa pls ku tolerate inahitaji nguvu ya ziada.mana wanakera mpaka basii,hasa ukimkuta asie na elimu na anajifanya anajua unaweza ukachukua maamuzi magumu
 
Chifu,ukifika kwenye point of no return, huwezi ogopa chochote,liwalo na liwe, ogopa Sana hasira.
 
nothing you know about climax panic
 
Kujichukulia sheria mikononi wananchi wameiga kwa polisi kutofata sheria wafanyapo kazi zao.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Siku ya kwanza kufika shule nikiwa kidato Cha 1 mwalimu wangu mkuu alituita wanafunzi wa 2 mbele Mimi nilikuwa kiduchu halafu mwembambaaa na mwenzangu mrefu mnene akatutolea mfano .
Akamwambia Yule mnene mkubwa " KWA UKUBWA NA UNENE WAKO USIMUONEE HUYU KIMBAUMBAU"
Na "WEWE KWA UDOGO NA WEMBAMBA WAKO UWE MPOLE LAKINI USIKUBALI KUONEWA"
 
We umelizika wenzio hawakubali.
 
Ndani ya utawala wa ccm hakuna reform (japo rais kasema) itakayofanyika ktk jeshi la polisi. Mfumo uliopo unainufaisha ccm kisiasa. Ni kama ilivyo hoja ya katiba mpya.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hamza amepanda mbegu, mbegu hii itamea vizuri na mavuno yake yatawanufaisha wengi ni suala la muda, tutasheherekea tena, zaidi na zaidi tena kuliko jana.
 
Umeitaja mahakama, ni kati ya maeneo ambayo haki za raia zinakandamizwa vibaya. Polisi wanakubambika case, ukifika mahakamani bila kutoa hongo unaenda kufungwa. Magereza na mahabusu zimejaa wahanga wa uonevu wa polisi kwa baraka za mahakama wakisingizia sio wao, ni sheria imewaongoza.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Ayaaa mambo omba ya sikukute mtoa mada.... Yakikukuta wew mwenyewe automatic unayafanya.... Mwisho wa siku unabaki kumsingizia S H E T A N I....
 
Wacha nicheke tu
 
Fikra zangu zinanambia kuna kitu hamza alifanyiwa na ma askari....

Hamza alikua na chance ya kuua raia wengi wasio na hatia lakini hakufanya hivyo.....

Binadamu tunapishana level za uvumilivu......

Niku ulize ulishawai kukutana na tukio lolote maishani mwako ambalo lika kuumiza mpk unatoka kwenye state ya kibinadamu timamu?

Simply, alicho fanya hamza ni Revenge

Nani nchi hii asiye jua majority ya ma askari wetu wengi wanapenda rushwa na udhulumati....
 
Nani kaingia Mtaani akaua watu sababu ya kuonewa?

 
Unaonekana hukupita jkt, kwako SMG inaonekana ni silaha nzito. Kule kuna mafunzo ya kutumia mpaka LMG. Aliojifunza huko inaoneka unahisi tu, na hata jeshi la polisi halitaki kupata taarifa kutoka huko. Wako bussy kubumba wanayoona yana manufaa kwao.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Ila cha ajabu hatutakuja pata ukweli kama matukio mengi yaliyopita. Rejea Lisu, Akwiline, Mo nk

Hadithi za kuungaunga hadi zinafunikwa ma tukio jingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…