Uchaguzi 2020 Ukiondoa Wana - CHADEMA na wafuasi wake mwenyewe, Tundu Lissu atapata kura nyingine nyingi kutoka kwa hawa

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Tangu mh Tundu Lissu arejee nchini mwezi Agosti, amekuwa akitoa matamko mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa yameweza ku reshape approach ya serekali ya awamu ya 5 katika utekelezaji wa mambo yake kadhaa.

Hii imepelekea makundi mbalimbali katika jamii ya Watanzania kunufaika kwa namna moja ama nyingine. Tafsiri ya hili ni kwamba bila ya intervention ya Lissu serekali isingeweza kuchukua hatua stahiki kwa manufaa ya makundi haya.

Makundi haya lazima yatakuwa yameshatambua mchango wa Lissu katika ufanikishwaji wa yale waliyokuwa wanayahitaji kutoka serekalini bila mafanikio kwa miaka yote 5 iliyopita.

Nina uhakika akilini mwao watakuwa wanajiuliza "Kama Tundu Lissu amewezesha haya ilihali hayuko madarakani, je haitakuwa zaidi pale atakapokuwa madarakani? Kwa nini tusimpe nchi kabisa tunufaike pakubwa zaidi?"

1. Walimu 13'000 ambao serekali imetangaza kuwapa ajira mpya - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu

2. Wafanyabiashara waliopewa msaada wa sh milioni 100 - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu

3. Wananchi walioahidiwa kujengewa barabara ya km 46 (Sengerema - Nyehunge) - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu.

4. Wananchi wa Itigi walioahdiwa kujengewa barabara ya km 16 - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu

5. Wamachinga ambao Magufuli kawaambia si lazima tena kulipia elfu 20 kupata kitambulisho - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu.

6. Askofu Niwemugizi aliyerejeshewa passport yake baada ya Lissu kupiga spana - huyu pamoja na waumini wake na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu

7. Kuanzia mwezi huu mshahara kima cha chini serekalini umepanda kutoka 170,000 hadi 270,000 - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu

8. Kwa mara ya kwanza (baada ya kuwa anawafokea tu kwa miaka 5) Watanzania wamemwona mgombea urais wa CCM akiongea nao kwa kuwabembeleza - hawa na wategemezi wao wote watampigia kura Tundu Lissu.

9. Ni makundi hayo tu kwa uchache, lakini yapo mengi unaweza kuongeza mengine.
 
Kwa tafakur ya mbali Tundu Lissu mpaka sasa amefanya Chama tawala wajifunze utu, nguvu ya mabavu huenda hizi ndy nyakati zao kujifunza, nawaahidi katika nyakati za kujifunza ustaarabu hawa jamaa ni sasa. Lazma vikao vyao sasa ndani ya Chama ni kulaimiana tu maana Lissu anachoma penye ukweli na ukweli unauma. Mungu bariki Tanzania mpya itakayojali utu wetu na haki zetu!
 
8. Wakulima waliodhulumiwa korosho yao na Kahawa sasa wataweza kuuza mazao yao popote pale penye soko duniani na hii itasaidia kuondoa u- monopoly market ulioanzishwa na ccm nao watampigia kura Tundu Antipas Lissu
 
Kura kwa Mh Lissu, jiwe hafai kuwa Rais wa nchi yoyote achilia mbali kiongozi wa familia yoyote
 
Watz hawamtaki huyu dikteta mshamba na limbukeni....
Lakini anao wale aliowateua, aliowapa magari na mishahara minono ambao ndio wasemaji kwa niaba ya NEC na kauli yao haipingwi popote!! Hao je nani atawadhibiti watende haki? Ngoma nzito hii!
 
Back
Top Bottom