Ukiona vyaelea ujue vimeundwa..................... .. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukiona vyaelea ujue vimeundwa..................... ..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Rutashubanyuma, Apr 30, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,599
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  Mwanadamu alivyoumbwa ni mwepesi kughafilika na kupagawa...
  Hupenda vya mvunguni lakini masharti yake hayawezi........
  Hupenda vya kunyonga lakini vya kuchinja huvikwepa.......
  Hupenda vya mteremko lakini vya kuhenya kuvigwaya.......
  Lakini ukiona vyaelea ujue fika vimeundwa.


  Nashangaa kumwona kijana mtanashati akimfukuzia binti hata hamjui......
  Kisa binti kapendeza, nguo zimemkaa huku akimeremeta.......
  Kijana damu humchemka na kujipiga moyo konde.......
  Bila hata ya kujiuliza hivi ni yeye tu mwenye macho ya kuangaza-angaza?
  Lakini ukiona vyaelea ujue fika vimeundwa.

  Kijana wa watu hupoteza hamu ya kula..........
  Shughuli zake zote kuziona ni nuksi.......
  Kisa ni kuwa bila ya kumpata yule binti yeye sasa mfu............
  Kijana kuhangaika usiku na mchana kumnasa mrembo.....
  Lakini ukiona vyaelea ujue fika vimeundwa.

  Siku ya siku kijana akutana na binti......
  Kiroho kikimdunda na kijasho kumdondoka amwaga sera.............
  Mrembo amwelewa lakini ampa pole.............
  Ukweli wafichuka kumbe mrembo ana mwenyewe.................
  Lakini ukiona vyaelea ujue fika vimeundwa.
   
 2. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hapa mkuu umegonga penyewe kabisa, na hii imeshatukuta vijana wengi sana, unamkuta binti unaanza kumbabakia kumbe hujui background yake na hujui kwanini umemkuta katika hali uliyomkuta nayo, na baadae ukija kugundua hali halisi tunaanza kulia lia tu, naikumbuka thread moja ilikuja last week inasema I will never trust any woman may be my Mom, mshikaji alifunguka vizuri na kweli alipenda mtoto wa chuo na alikutana nae katikati ya jiji...
  akatoa simu na pesa kumbe alikua hajui kuna msemo unasema Ukiona vyaelea ujue vimeundwa

   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,599
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  mara nyingi huwa tunajisahau.........tukifikiri ni sisi tu wenye meno kumbe wenye nayo tuko wengi na vingine vilikwishatafunwa na wengine..................kwa hiyo tunatakiwa twenda polepole...tukisoma khali ya upepo.....[MENTION]@Manyanza[/MENTION]
   
 4. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  hahha.....nyie si mnadhani vyote vinavyoelea ni vyepesi
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,599
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  Vaislay.................kwani hamtujui tulivyo mabwege tukikamatwa na vimbwanga vyenu....wakati mwingine mnapendeza mno na kutuchanganya.......[MENTION]@Vaislay[/MENTION]
   
 6. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,660
  Likes Received: 8,212
  Trophy Points: 280
  huenda kweli vimeundwa ila aliyeviunda labda hajui kuvitumia..au havitumii ipasavyo
  basi, huenda ikawa ndiyo bahati yako hapo kwamba wewe ndiye uliyekuwa ukingojewa to make a full utilization of kile kilichokuwa chaelea mtoni ilhali kilitakiwa kuwa chaelea baharini!
  never give up dat easily..
  ukiona vyaelea jua fika vimeundwa, ila je VYAELEA PANAPOSTAHILI!??
   
 7. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ishinde tamaa....tatizo wanaume wa sasa macho manne
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  na sijui kama nini wanaume tumekua dhaifu sana mbele ya wanawake? mkuu kwenda pole pole haiwezekani bana ukiona totozi lazima uanze kujipanga ili kuing'oa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,599
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  haya pia yaezekana kwani hata maandiko husema nayepnda siye atakayevuna.................lakini aliyepanda si ni mzazi na huyu aliyenaye si ndiye mvunaji au wataka kusema havuni vizuri?[MENTION]@Mentor[/MENTION]
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,599
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  angalia isije kukun'oa meno yako mwenyewe...............[MENTION]@manyanza[/MENTION]
   
 11. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Vipi kuhusu kina kaka? Unamuona kaka mtanashati.......... usafiri mzuri...... anapendeza, tunaanza kumrembulia macho na kutikisa makalio...... kumbe ana mkewe ambaye wamesota naye sana tu. Na pengine ungemuona kipindi anachapa lapa na bahasha ya kazi yenye CV na vyeti, kikwapa kwa mbali ......wala usingemuangalia mara mbili.....

  My point is ni pande zote!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  sijui bwana...
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,599
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  mnajipamba mno kwa malengo ya kututia tamaa............khalafu mwatuambia tuishinde tamaa....... Vaislay
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mkuu siku hizi nani anafanya hii kazi ya kukufundisha haya mambo
  Naomba unipe no ya huyo mtaalam uliyempata maana aise naona vtu vinashuka tuu bila hata mgogoro
  Asante sana mkuu kwa hii useful post
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,599
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  weye smile acha uongo..wadai hujawahi kutongozwa?....sasa hujui nini?[MENTION]@smile[/MENTION]
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,599
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  Mwenyezi Mungu kanijaza roho Mtakatifu.................na hizi busara zinatoka mbinguni
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,599
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  Kaunga uko juu sana.........sikupenda kuangalia upande wa pili wa shilingi kwa sababu zilizodhahiri..........msije mkalalama ya kuwa mwamba ngoma huvutia kwake..............[MENTION]@Kaunga[/MENTION]
   
 18. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahaa Smile hujui nini? ruta, Smile anatuzuga tu refer thread zake ambazo hua anawaponda wanaume...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ruta mambo ya Tanga hayooooooo! LOL.
   
 20. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  hahahaaa poleni sana..
   
Loading...