Ukiona picha hizi zinakukumbusha nini

Ukiona picha hizi zinakukumbusha nini

hii kitu madam nyamchele ilikuwa ni raw matreial ya kutengenezea Magari ya bati pia(watoto na vijana). Huwezi kukuta hili kopo jalalani kirahisi.
382b0a5ab325086884f5f89ed43357fe.jpg

la pili kushoto
bila shaka hao wenye ndala/yeboyebo ni watoto wa mwalimu au mwenyekiti wa kijiji
 
Umenikumbusha enzi za utoto nilikuwa na hoteli yangu kama za wagosi Dar,,,hasa chapati zangu za kuchoma visoda na kutoa ganda la kati !!!
Matonge yalikuwa visoda vya bar,,,kipind hicho tukiokota ganda la boksi ya condom tunaitana kuona wakubwa wakifanya mchezo ambazo ni picha za maelekezo,,,daaah utoto ni uchizi toshaa
 
redio kaseti inanikumbusha jirani yetu aliyekua nayo kijiji kizima pale Mombo
 
hallo,long time ago,wakati naanza life mafuta ya kupikia ni super ghee.hivi yapo jamani?
 
Mambo yamebadilika sana!! Ila hizo taa za chemli nimekuta huku usa wanazitumia wakiwa hunting!
 
1459299458272.jpg

Bolingo kavasha msondo ngoma zote zilihifadhiwa kwenye hizo CD !!
 
Mshana jr ...Umenikumbusha mbali sana enzi za upendo umetawala familia. Maji mtungini kikombe kimoja watu tunashea tu mambo ya extended family chakula kinapakuliwa kwenye sinia halafu mnaweka kwa makundi kulingana na umri mnakula pamoja. Maji ya kunywa yamejazwa kwa jagi ila kikombe ni kimoja hahahahaa hahhaa na wala hakuna alieona kinyaa wala kuambukiza kitu.
Kibatari/koroboi hahaha enzi hizo kulikua na watu wanapita mitaani wakusanya makopo ya dawa ya mtu au juisi za makopo, mna badilishana ww unapewa pipi kidonge moja kwa kopo moja au gulbiti hahaha haha daah
Cherehani ya singer maza alikua anatushonea saana nguo sare sare kutambaa kibaki anashona "pichu".
Kulikuwa na Tanbond pia. Haha hahaa those sweet memories
 
Yaani nilikuwa kwenye somo la infection control, wanashauri nyumbani kutumia mafuta ya maji au lotion ya tube kwakua ni mazuri kwa matumizi binafsi bila maambukizi. Nilikumbuka lile kopo la Vaseline liliachwa kwenye dressing table kila mtu kwa muda wake na watu walikuwa na afya njema bila magojwa ya ngozi.
 
Yani kijiradio chetu kilikuwa kinatafuna sana kanda, nikishaona imeharibika narudisha kwenye kasha lake nakaa kimyaaaaaa, lakini wakirudi wanajua tu kuwa ni Mimi... Utoto raha sanaaa
Uzi ukitoka tunaunganisha makasha mawili ya kibiriti huku na kule,
Inakuwa simu hata mita mia mnasikilizana.
Hapo ni mwendo Wa haloo,hellow, hapo hakuna cha smartphone wana cha kimobitel.
Akili zilikuwa zinacharge sana. Hakuna waste product kila kitu tulikuwa tunareinnovate.
Nakumbuka jamaa mmoja aliitwa Edwin aliokota redio jalalani mbovu kabisa, atatafuta ubao akanyofoa baadhi ya vitu, akatengeneza headphone local kaunganisha na vikorokocho vyake pale kwenye mbao. Ikashika radio Tanzania. Mitaani watoto wote tulimuona kama Mungu, tukawa tunamfuata nyuma kama mitume Wa yesu. Ukiamka asubuhi unaanzia kwao kushangaa redio. Thanks to street engineering
 
Back
Top Bottom