Ukiona mwanamke anafika Miaka 30 hajaolewa, kuwa nae makini kama unataka kumuoa

Mi mwenyewe nawashangaa shogangu, we wasikupe presha kwa ambao hawajaolewa wataolewa kwa muda wao baada ya kujihakikisha ya kwamba wanaweza kumudu hizo ndoa, kama hawawez basi sio lazima katika amri 10 za Mungu hakuna mahali imeandikwa mwanamke asipoolewa atakataliwa mbinguni!
Comment imenikosha sana, wanasahau kuwa wao ndo wanaodanganya mabinti kwa uchumba hewa.
 
ina maana unamaanisha KE anavyozidi kuongeza miaka ndivyo thamani yake inazidi kushuka......tofauti na ME ambae thani inapanda kwenye kuhusiana...??....
 
Wewe nani hadi umpangie mtu muda wa kuolewa? Wataolewa rizki zao na machaguo yao tayapokuja hata wakiwa 50's sioni tatizo kwanza tuliowahi kuolewa tulijiingiza kitanzini tu kwa maana sasa hivi ndio tunaona machaguo yetu yakipita kwa nje na hatuna jinsi tumeshafungiwa
Noted, huu ndiyo ukweli kutoka moyoni mwako.
 
Kwa kifupi nina uzoefu wa kiasi fulani kuwa na urafiki wa kimapenzi au urafiki wa kawaida na wanawake waliozidi miaka 30.. Kuna vitu vingi sana najifunza kutoka kwao..

Wengi wao wanafika umri huo bila kuolewa kwa sababu zifuatazo..

Wengi toka wakiwa wadogo ni Viburi.. Wengine wana tabia ya Dharau.. Wengine wanajisikia sana.. Wengine wana mambo mengi, unakua na demu akili yake haitulii napenda mambo makubwa mno kuliko uwezo.. Wengine umalaya.

Kwa tabia hizo lazima mwanamke ufike miaka 30 bila kuolewa. Kama unatabia hizo mwanamke badilika mapema, wanaume tuko makini sana kwenye kuangalia mke wa kuoa. Badilika
Sababu kubwa na ya maana kati ya zote ulizozitoa hapo juu nimeiona moja tu nayo ni mambo mengi, kwani mwanamke mwenye malengo mazuri na maisha yake ni lazima aandae mambo yake mapema kuliko kumsubiria mwanamme ndiyo aje amlee na kuanza kupata manyanyaso ya hapa na pale. Lakini umejitahidi kufafanua mkuu.
 
Back
Top Bottom