Ukiona choo ndotoni usikitumie



Ndoto ndani ya ndoto-- huo ni ulimwengu wa "kifo", ambao ni ngumu kwa roho iliyomo mwilini kwenda hadi iwe imeachana na mwili (imekufa).
 
Ndoto taarifa
Ndoto maono


Mkuu Mshana jr, Elimu yako ni kubwa.

Ila angalizo ulilotoa kuhusu kutotumia choo ndotoni ni jambo gumu sana katika aina ya hizo njozi mbili. Sababu kipindi hicho mtu unakuwa huna tena controll ya nafsi yako (subconscious or unconscious).
 
Ndoto ndani ya ndoto-- huo ni ulimwengu wa "kifo", ambao ni ngumu kwa roho iliyomo mwilini kwenda hadi iwe imeachana na mwili (imekufa).
Hivyo unataka kuniambia kwamba nini kilitokea juu yangu?
 
Hivyo unataka kuniambia kwamba nini kilitokea juu yangu?


Maisha ya ndoto yapo kati ya duniani na Barzakh, maana yake ni kwamba roho inakuwa nusu ndani ya mwili na nusu imo Barzakh, unapoamka kutoka usingizini maana yake roho yako imo "full" katika mwili na mtu akifa maana yake roho yake "full" imeingia Barzakh ambamo roho inakuwa na maisha mapya ya kiroho.

Ndoto tunazoota wakati huo roho zetu huwa katikati ya maisha ya duniani na maisha ya Barzakh sasa inapotokea kwamba ukiwa mahali hapo ukaota ndoto ndani ya ndoto ndiyo nikasema hiyo ndoto ya pili si ya katikati ya duniani na Barakh bali ipo katika ullimwengu mwingine (another realm) na huo ulimwengu uliokaribu na sisi ni Barzakh na baada ya Barzakh unakuja ulimwengu wa akhera ambamo kuna kiyama (hukumu).

Ndiyo maana ninashangaa au labda lipo nje ya elimu na ufahamu wangu kwamba mtu aote ndoto ndani ya ndoto nje ya Barzakh?!!, yaani hiyo ndoto ya pili ni ya ulimwengu wa Barzakh ambamo zinaingia roho zilizotengana na miili yetu baada ya kufa.
 
Asante mkuu, kweli maisha ni fumbo, kwa lugha nyepesi naweza kufahamu maana ya Barzakh? Je kwa hali hii kujitokeza kwangu huwenda nilikufa usingizini na kufufuka bila kujijua?
 
Epuka kutumia choo ndotoni kwakuwa kama hujajisaidia kitandani basi kuna jambo baya linakutafuta....

Jambo kama lipi/yapi?
Na mtu akiwa katumia choo anafanyaje kuondoa aliyotenda la kujiwekea balaa na kujirudisha mwanzo?
 
Duh.! Umenikumbusha juzi Kati niko usingizini nimechoka na kazi za kutwa nzima sasa nikaota niko napiga kazi ngumu kwenye jengo flani la wahindi,
Sasa ile jioni nimemaliza kazi tuko na washkaji kwenye foleni ya kulipwa hela ili niondoke nirudi home mara ghafla simu yangu ikaita nikazinduka usingizini kupokea ni jamaa flani ananidai pesa nkamwambia sina hela maana amepiga ndo nlikuwa kwenye foleni ya malipo!
 
Asante mkuu, kweli maisha ni fumbo, kwa lugha nyepesi naweza kufahamu maana ya Barzakh? Je kwa hali hii kujitokeza kwangu huwenda nilikufa usingizini na kufufuka bila kujijua?


Barzakh ni mahali ambapo roho huingia baada ya mtu kufariki, unaweza kusema ni kaburi la roho au ni hatua ya kati ya maisha ya roho baina ya maisha ya duniani na maisha ya akhera, Barzakh ni mahali ambapo roho husubirishwa kwa ajili ya ufufuo wa siku ya akhera.

Mtu roho yake ikiingia Barzakh maana yake mtu huyo kishakufa na kamwe hawezi kufufuka.

Ndoto ndani ya ndoto haiwezekani, kama inawezekana basi hata mtoto angejizaa mwenyewe.

Basi tufafanulie hiyo ndoto yako ndani ya ndoto ilikuaje, kumbuka ndoto ya kwanza lazima mtu ulale usingizi na ndoto ya pili lazima ulale tena ndani ya usingizi wa kwanza, kwa hiyo utaona ndoto ni moja tu ambayo ni hiyo ya pili, ambayo ni ndoto ya kawaida tu.

Practically ,huwezi kuota ndoto ndani ya ndoto.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…