Ukiona choo ndotoni usikitumie

Ukiona choo ndotoni usikitumie

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,446
Reaction score
829,809
Sikutaka kuileta mada hii mapema bali wakati huu.... Nina sababu maalum.... Baada ya muda mchache ujao tutaenda kulala, wala tusitambue yanayoendelea ulimwenguni... Mwili wa utashi utapumzika... Mwili wa roho uta take cover...!
Roho ni 'nafsi huru ' itafanya itakayo na kuenda itakako.. Taarifa utazipata kupitia ndotoni....
Ndoto taarifa
Ndoto maono
Ndoto mvurugano
Unapoona/ unapoota choo ndotoni kuna tafsiri kama tatu... Moja lazima iwe sahihi... Makinika... Usikitumie kwanza...

Choo ni uchafu... Hakuna anayependa uchafu.. Ukiona mtu anapenda uchafu ana walakini
Choo kinanuka... Hakuna anayependa harufu mbaya.. Ukiona mtu anapenda harufu mbaya ana walakini...!

Choo si kitu cha kuonekana hadharani... Kina sehemu yake ya kutunzwa... Ukikiona choo ndotoni si ishara njema(hapa ni kwa tafsiri ya kinyesi)

Choo ni mlango wa kuzimu ( hapa choo ni kile kibebeo cha uchafu wa kinyesi toka kwa mwanadamu)... Choo cha mnyama hakina kinyaa kama cha mwanadamu kwakuwa mnyama ni hayawani...

Epuka kutumia choo ndotoni kwakuwa kama hujajisaidia kitandani basi kuna jambo baya linakutafuta....
 
Hivi kumbe hiyo ndoto ya kuota choo ndo inavyomaanisha? Mimi nafikiriaga hapo tu kuwa usikitumie sababu utajikuta umejisaidia kitandani ila hiyo tafsiri nyingine nilikuwa siijui shukrani mkuu kwa ufafanuzi

Ila swali langu ni hili mtu atawezaje kujizuia ndotoni ikiwa wakati anaota anakuwa hajielewi ukiachilia mbali zile ndoto ambazo mtu anakuwa anajua kabisa kuwa anaota na anakuwa anajielewa naongelea zile ambazo anakuwa hajielewi anawezaje kujizuia kutumia choo?
 
Nipo nje ya mada ila katika ndoto,

Iliwahi kunikuta hali hii, Nililala katika hali ya uhalisia nikapata ndoto, nikaota katika ndoto ya kwanza ya kwamba nimelala huku naota ambapo ndoto ya pili nikaota tena nimelala naota.
Yani ndoto moja ikawa na mtoto na mjukuu.

Kila nikijaribu kuwaelezea watu wananiona kama mwehu, haya mambo husababishwa na nini?
 
Inawezekana kabisa ni kama zile ndoto za kuota unataka kufanyiwa jambo baya kisha unakemea kwa jina la Yesu aliye hai
 
Nipo nje ya mada ila katika ndoto,

Iliwahi kunikuta hali hii, Nililala katika hali ya uhalisia nikapata ndoto, nikaota katika ndoto ya kwanza ya kwamba nimelala huku naota ambapo ndoto ya pili nikaota tena nimelala naota.
Yani ndoto moja ikawa na mtoto na mjukuu.

Kila nikijaribu kuwaelezea watu wananiona kama mwehu, haya mambo husababishwa na nini?
IPO lakini kwa uchache unakuwa ndotoni kisha huko ndotoni unaota tena tena ndoto.. Hivi unatambua wewe ni nafsi zaidi ya moja? Pitia mada hizi utaelewa zaidi
 
Nipo nje ya mada ila katika ndoto,

Iliwahi kunikuta hali hii, Nililala katika hali ya uhalisia nikapata ndoto, nikaota katika ndoto ya kwanza ya kwamba nimelala huku naota ambapo ndoto ya pili nikaota tena nimelala naota.
Yani ndoto moja ikawa na mtoto na mjukuu.

Kila nikijaribu kuwaelezea watu wananiona kama mwehu, haya mambo husababishwa na nini?
 
Roho ni nafsi huru? Vipi wale wanaoamini binadamu ana mwili, roho na nafsi wakimaanisha ni vitu vitatu tofauti?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom