Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Ukimya wake unaniweka njia panda, naomba ushauri

Sasa unafiki na uchawi unatokea wapi? Kisa nimekwambia ni bora mwanaume akupende? Hayo ni mawazo yangu .......kama unayaona hayafai unayaacha tu.

Na hata ndiyo naweza kuwa na mwanaume anayenipenda mie nisimpende mana hata biblia inasema wanaume wapendeni wake zenu....na wanawake waheshimuni waume zenu........mie nitamweshimu ila jukumu la kunipenda ni lake yeye mwanaume.....

Ndiyo maana unalilia hapa mana unachukua jukumu la mwanaume ..... Wewe unatakiwa kumweshimu.

NB.
Umenikuta sijazimua.....
Heshima inakujaje bila mapenzi bibie? Love is above all, above everything.
 
Mkuu usimuombee mabaya cha msingi kumuombea mema Mungu atakulipa hayo mambo yapo nafikiri ata wewe unaweza kuwa ulimuumiza mtu ni mambo tu hayo kwenye mahusiano aiseee
Kweli sio vizuri kumuombea mtu mabaya ila kwa kunidhalilisha huku, Mungu anisamehe... Yamkute tu mabaya. Mbona yeye hana utu? Haoni kama anachonifanyia ni cha kinyama?
 
Sure dada. Wapo kibao wanaonitokea, nnachofanya ni kuwapa nafasi labda atatokea wa kunipenda nami nimpende japo kidogo. SIWEZI KUWA NA MTU NISIYEMPENDA kabisa. We unaweza? Kama ndio, basi we mnafki. Unaweza kuwa mchawi kabisaa!
 
Mkuu... Maybe it was a joke. To me it's OK to joke about anything, but not to extend such a joke to people around us. That doesn't appear as a joke to me. That's serious.
If he never meant it, he shouldn't have said it several times when people are always around us. Sasa kwa wanaonijua, si watasema huyu mchumba wa flani, atamuoa alituambia siku flani? Kama kuna mwenye interest, si ndio nimeshampoteza?! Angeninong'oneza peke yangu, hapo sawa. Kunitangazia kwa watu, kumbe ananichora sio poa. And on top of that, namuuliza still anakausha tuu. Nimemkosea nini mpaka anitende hivo? Kosa langu kumpenda na kumjulisha? Coz kwangu mimi sioni kosa kumvulia pichu, hakuwa wa kwanza, wala sio wa mwisho. Wote tulikuwa na genye na tulitumia wakati huo tuliopata kukata hamu. Haliniumi kabisaa.... Kinachoniuma ni kuniharibia. Inawezekana kabisa hao ma-x walisikia ndio maana wakabadilisha mawazo.
Yaan nakupenda tu jinsi unavyojua kupenda mpaka kuishia hapo.
tena matapeli wengi hufanya kama alivyokufanyia huyu kaka. eti ana kutel mbele za watu. Shame on him kwa kweli. nina rafiki yangu yeye mbinu yake huenda kijijin kwa mabibi/mababu kukuhakikishia atakuoa but anakuacha kweupeeee.

Please kukosea sio mbaya bali kurudia makosa. Just take note of what happened and take a lesson from there and move on. Don't allow any human being to still your happines. All will be well with you.
 
Habari wapendwa wa MMU,

Mimi ni msomaji mzuri sana wa JF majukwaa yote.

Nimeonelea nijisajili ili nami niweze kutoa yangu ya moyoni. Kwa kifupi tu mimi ni mwanamke, mwaka huu natimiza miaka 33, ni mfanyabiashara kwahiyo kwa kiasi kikubwa najitegemea kwa gharama ndogo ndogo. Nachoenda kuelezea ni hali halisi nnayopitia na ninaomba msinihukumu bali mnipe ushauri.

Tokea nivunje ungo, nimeshapitia mahusiano kadhaa, sitopenda kutaja idadi lakini nimewahi kupenda kwa dhati mara 2 tu. Mara ya kwanza ni kwa x wangu ambaye ndio alikuwa bf wangu wa kwanza kabisa. Baada ya kuumizwa sana na huyu x sikuwahi kupenda tena, niliingia kwenye mahusiano ili tu nisiwe mpweke ila sikuwapenda kwa dhati kabisa waliofuata. Huyo x mpenzi wangu wa dhati, ameoa mwaka jana na alinijulisha nami niliridhia kwa kuwa mapenzi yale ya dhati yalishaisha.

Sikuwahi kufikiria kuolewa kabisa baada ya kuumizwa na x mpenzi wangu huyo niliyempenda kwa dhati kwa hiyo niliamua kujisomea na kujipanga kutokuwa tegemezi hata kwa maboyfriend waliofuata. Nimekuja kupenda tena na kwa sasa nataka niolewe nianzishe familia.

Mwaka juzi nikiwa msibani nilikutana na kijana mmoja maarufu mjini akanitongoza na kutaka nikalale naye siku hio hio mi kwa kujiheshimu nikampotezea. Kusema kweli jamaa yuko vizuri, sio tu maarufu ila mpunga anao pia. Kwa upande mwingine huyu jamaa anafahamiana au niseme familia yake na familia ya ndugu zangu wameoleana kwa hiyo kuna kufahamiana zaidi ya kimjini mjini. Yeye alichukua namba yangu ya simu ila mimi sikuchukua.

Kesho yake alinipigia simu na sikupokea kwa kuwa siku hiyo niliuwa safarini na nikaamua kwamba sitopokea namba yeyote mpya. Ikapita kama miezi 3 hivi, nikiwa na dada na rafiki yangu katika story tukajikuta tunamzungumzia huyu mtu maarufu. Kwenye mazungumzo nikawaambia kuwa huyu jamaa aliwahi kunitokea ila mimi sikutilia maanani.

Basi ndugu zangu wale wakanisema kweli, "Oooh, unapoteza nafasi, wenzio wanaitafuta, mpigie simu na nini na nini". Kwa kuwa sikua na namba yake, dada yangu akanipa. Nikamwambia dada hata nikimpigia simu nitamuambia nini? Dada yangu akasema hilo niachie. Nitampigia na kuongea nae mimi. Basi nikamuachia hio ligi. Dada akapiga simu, akaongea na mshkaji wakapanga appointment.

Siku ya siku ikafika nikajiweka sawa nikaenda kukutana na jamaa kwa mara ya pili baada ya miezi 3. Kuanzia siku hio tukawa na mawasiliano mara kwa mara. Nilijikuta napata hisia za kumpenda kwa dhati huyu jamaa. Si kwa uzuri, umaarufu au pesa aliyo nayo, la hasha! Akaniomba nimpe nafasi ili anioe, nikamkubalia. Ila alinitahadharisha kwamba ana girlfriend.

Nampenda kweli na wala sikumficha, nilimuambia. Nimewahi kulala nae mara moja tu na kwa hakika alifurahia tendo. Sijawahi katika pita pita zangu kuona mwanaume amefurahia tendo kama huyo. Mwaka jana alikuwa busy sana na kampeni kwa kuwa alihusika kwa ukaribu sana na mgombea wa urais wa chama kimojawapo. Nilimpa nafasi amalizane na mikiki mikiki ya kampeni ila nikaanza kupata wasi wasi na uhusiano wetu kwa kuwa, kama nisipomtafuta mimi basi yeye hanitafuti ng'o! Nilijipa moyo kwamba labda yuko busy akitulia atanitafuta lakini wapi. Kwa kuwa nilipenda kweli sikuacha kumtafuta na kumjulia hali.

Katika kipindi hicho, nilitokewa pia na wanaume 3 waliotangaza nia ya kunioa. Kati yao, 2 nilishakuwa na mahusiano nao 1 ni mpya kabisa. Sikuwapa jibu kwa kuwa yupo nnayempenda kwa dhati na ndio nilikuwa namsikilizia. Mwaka huu ikabidi nianze kuuliza kwa uhakika kama nia ilikuwepo au la! Nikaanza na wale 2 niliokuwa na mahusiano nao.

Wote walinijibu kwamba niendelee tu na maisha yangu wao wamebadilisha mawazo. Nikashukuru, nikabaki na yule 1 ambae sijawahi kuhusiana nae mpaka sasa na anasubiri nimpe nafasi ila mi nimeogopa, huenda nae anataka anifunue tu chupi kisha asepe kwaiyo nimemuweka pending. Nikaja kumuuliza huyu mtu maarufu niliempenda kwa dhati msimamo wake majibu yake ni kwamba "ndio nilitaka kukuoa ila maisha yana changamoto na kwa sasa napitia wakati mgumu siwezi kukuelezea".

Nimejaribu kumsisitiza anipe msimamo wake kama pamoja na changamoto anazopitia kama amebadilisha mawazo au la, ili mi nifanye maamuzi, amekaa kimya. Nimemjulisha pia kwamba yupo anayetaka kuleta posa nyumbani kwaio anipe msimamo wake lakini jamaa bado hajibu, amekaa kimya tu. Nimemtafuta sana, jamaa response yake kwa kweli ni zero. Namuandikia msgs kwenye whatsapp, naona anasoma lakini hajibu. Nampigia simu hapokei.

Hitimisho!
Jamani, mimi nampenda sana huyu jamaa huyo mwengine sina kabisa hisia za kumpenda. Natongozwa kila ya leo lakini kila nikitongozwa namuwaza tu huyu mpenzi wangu maarufu. Nikipenda napenda kweli. Ningependa kuishi na mtu ninayempenda kwa dhati na sio tu kwasababu ya umri nikimbilie kuolewa na mtu nisiyempenda. Ndoa itanishinda. Kinachoniuma ni kwamba yeye hataki kuwa muwazi kwangu. Aniambie tu msimamo wake, mie nitaridhika na jibu lolote, hata ikiwa kumkosa kabisa mie nipo radhi. Nisaidieni nipo njia panda.

Asanteni na karibuni kwa michango.
aise una moyo ww mdau mpaka nimeshindwa kushangaa yani matendo yote hayo hauwezi kusoma alama za nyakati cheza na muda tu utakuta mwana sio wako aise
 
Oh I see! But Karma's a bitch... He will never find true love. He will always come across women with greed for money and will tear him apart. Just like the one he's dealing with right now. Until he's done with her, he's a bit broke.
Najua mtasema ana pesa atapata wengine.... Ila kwa kujitia nuksi na huyu mwizi aliye nae, atawavagaa mianawake mijizi forever.
Rafiki inaonekana umemupenda sana huyu jamaa aisee. Wapi nitapata mutu ya kunipenda kiasi hiki jaman???

hahahahahhaha kiding
 
Yaan nakupenda tu jinsi unavyojua kupenda mpaka kuishia hapo.
tena matapeli wengi hufanya kama alivyokufanyia huyu kaka. eti ana kutel mbele za watu. Shame on him kwa kweli. nina rafiki yangu yeye mbinu yake huenda kijijin kwa mabibi/mababu kukuhakikishia atakuoa but anakuacha kweupeeee.

Please kukosea sio mbaya bali kurudia makosa. Just take note of what happened and take a lesson from there and move on. Don't allow any human being to still your happines. All will be well with you.
Asante sana kwa uelewa wako mkuu. People like them do not deserve a person like me. I wonder how I got carried away with his lies. At some point I was warned, but moyo ukishapenda bhana... Ni majanga tuu! I take note & shall be careful!
 
Bibie una miaka 33 hujajua tu kuwa huna chako hapo??

Watu maarufu na wenye hela kama mimi profile zao huwa ni kumega tu na kuacha, unapomtamkia tu suala la ndoa kengele inagonga kichwani.

Yawezekana anao kama tisa hivi, na wote wanajisifia kama wewe kuwa walimpa mahaba mpaka akafurahia haswaa.

Kifupi umeshapigwa chini, jiongeze tafuta mahali serious, achana na watu maarufu, watu serious na ndoa huwa ni watu decent ambao nyie wakina dada huwa mnawaona " washamba fulani hivi"

Na huo ndio ukweli mchungu, hutaki unaacha
Haa haaa haaa yan km hajakubali hapo bdoooo!!! Bhas tenaaaaaa
 
Kweli sio vizuri kumuombea mtu mabaya ila kwa kunidhalilisha huku, Mungu anisamehe... Yamkute tu mabaya. Mbona yeye hana utu? Haoni kama anachonifanyia ni cha kinyama?



Pole sana mkuu kama muislam safi au mkristo safi nafikiri imani zetu zinatufunza kusamehe..unapomuombea kheri Mungu anafungua shani mbele yako..sisi binadamu ipo siku tutakutana tu..wengine wanamidomo mibaya sio vizuri kufungua kichwa kuomba mabaya kwa binadamu wenzako..piga moyo konde simama jipanguze halafu toka mbio kama usain bolt mdada
 
Pole sana mkuu kama muislam safi au mkristo safi nafikiri imani zetu zinatufunza kusamehe..unapomuombea kheri Mungu anafungua shani mbele yako..sisi binadamu ipo siku tutakutana tu..wengine wanamidomo mibaya sio vizuri kufungua kichwa kuomba mabaya kwa binadamu wenzako..piga moyo konde simama jipanguze halafu toka mbio kama usain bolt mdada
Siwezi kumuombea kheri baradhuli kama huyu. Kusamehe will take time... Not now.
 
Siwezi kumuombea kheri baradhuli kama huyu. Kusamehe will take time... Not now.





Poa mkuu maana hiyo ipo ndani ya uwezo wako sisi kama washereheshaji tu..inaonekana jamaa ulipenda kama zile za kwenye tamthilia za kifilipino....ngoja nitafute kama wewe labda anaweza kunishawishi kufunga ndoa[emoji12] [emoji12] [emoji12] just kiddin
 
Pole sana bt huo ndo msmamo wale kashakuchoka
Sawa... Nae ni binadamu hana lolote special. Yatamkuta tuu. Nna uhakika, kwa ubaradhuli wake huu hajaniumiza mimi tuu. Lazima kaumiza wengine kawaumiza same.
 
Sawa... Nae ni binadamu hana lolote special. Yatamkuta tuu. Nna uhakika, kwa ubaradhuli wake huu hajaniumiza mimi tuu. Lazima kaumiza wengine the same. Nayeye, ataisoma namba.
 
Poa mkuu maana hiyo ipo ndani ya uwezo wako sisi kama washereheshaji tu..inaonekana jamaa ulipenda kama zile za kwenye tamthilia za kifilipino....ngoja nitafute kama wewe labda anaweza kunishawishi kufunga ndoa[emoji12] [emoji12] [emoji12] just kiddin
Kweli nilimpenda, sio uongo. Sana tuu!
 
Back
Top Bottom