Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,661
- 698,495
Leo ni kumbukumbu ya ni 911, fumbo la ghorofa pacha la world trade center ambalo halipo tena.
Mgawanyo wa madaraka na majukumu
TISS kufuatilia usalama wa nchi/taifa, viashiria, mipango, wahusika, wafadhili, na hata utekelezaji wa jambo lolote baya linalohusika na taifa katika ujumla wake bila kuwasahau viongozi.
JWTZ, Jeshi la wananchi wenye nchi - Jukumu kubwa ni kulinda mipaka ya nchi/Taifa isiingiliwe na maadui, pia kwenda vitani inapohitajika nk.
Jeshi la Polisi Tanzania - Kulinda usalama wa raia na mali zake pamoja na majukumu mengine yote yanayohusika na usalama wa wananchi na mali zao.
Majeshi mengine yote ni wasaidizi tu toka hayo hapo juu.
Tumekuwa na kipindi kama cha mpito tangu sakata la bandari lilipoanza zaidi ya miezi mitatu sasa. Mambo yamekuwa mengi mno kulihusu mema na mabaya.
Ni ngumu kuwalaumu TISS kwakuwa hawa huwa hawaendi front, na kwa mtazamo wa kawaida unaweza kudhani hawajafanya kitu, lakini pengine kwenye hili sakata wanapaswa kushukuriwa pakubwa sana!
Linapokuja suala la mipaka ya nchi, kwa maana ya anga, nchi kavu na majini, mhusika mkuu ni JWTZ kwa msaada wa TISS. Suala la bandari ni mojawapo ya maingilio ya nchi kutoka mipaka ya majini.
Utendaji wa JWTZ ni tofauti sana na Jeshi la polisi. JWTZ sio watu wa matamko wala press conferences kwakuwa hawadili na wananchi moja kwa moja na ndio maana unaposikia Jeshi linataka kutoa tamko ama linataka kuongea na waandishi wa habari, tashwishwi huwa kubwa.
Matamko ya kutaka wananchi wasivae nguo zinazofanana na za kwao, matamko ya kutaka kuingia mitaani kusaka nguo/sare zinazofanana na za kwao, matukio yanayosambazwa mitandaoni wanajeshi wakiwaadhibu wananchi wanaokutwa na nguo zinazofanana fanana na zao, naomba niseme sio level za Jeshi letu ni kukiuka katiba na kuingilia majukumu ya wengine!
Kama tunaweza kuipongeza TISS kwenye sakata hili la bandari, basi sasa macho na masikio ya wananchi yana tashwishwi ya kusikia neno toka kwa mhusika mkuu wa mipaka na malango ya taifa. Matamko ya sare sio case sensitive kama ishu ya mipaka.
Kama KITI kimeamua kukaa kimya. Inaweza kuwa ni hasara kubwa yenye faida kwa wengine kama nalo likisema. Funika kombe mwanaharamu apite.