Ukimwi sasa kupimwa kwa mate

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
MAMLAKA ya Kudhibiti Chakula na Dawa Nchini Marekani (FDA), imethibitisha na kupitisha matumizi ya kifaa kipya cha kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa kutumia mate.

Kifaa hicho kilichotengenezwa na wanasayansi wa nchini humo, kimeelezwa kuwa na uwezo wa kutoa majibu sahihi kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kati ya dakika 20 na 40 baada ya kupima.
Imeeleza kuwa kifaa hicho kilichopewa jina la OraQuick, kimebuniwa sio tu kwa ajili ya matumizi ya hospitalini bali pia nyumbani na kitaanza kupatikana katika maduka ya dawa nchini Marekani kuanzia Oktoba mwaka huu kabla ya kusambazwa nchi mbalimbali duniani.

Serikali ya Marekani imesema inaamini kifaa hicho kitasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kubadili tabia ya watu wanaoishi na virusi hivyo bila kujua.
Wataalamu mbalimbali wa afya wamekielezea chombo hicho kuwa ni hatua nyingine kwa dunia katika jitihada zake za kudhibiti maambukizi ya VVU
.
Kinavyotumika
Kwa umbo OraQuick hakina tofauti na vipimo vingine vya kisasa ambavyo vimebuniwa kwa ajili ya kupima magonjwa kwa haraka kama vile malaria, Ukimwi na kisukari.
Lakini badala ya kuwa na sehemu ya kudondoshea tone la damu, kina sehemu laini iliyojitokeza, maalumu kwa ajili ya kunyonya mate.

Mtumiaji hapaswi kukitemea mate, bali kwa kutumia sehemu hiyo maalumu, atakiingiza kifaa hicho mdomoni na kuchukua mate katikati ya fizi na midomo chini au juu.

Sehemu hiyo laini italoa mate na kuyanyonya. Hapo mpimaji atapaswa kukiondoa kifaa hicho na kukiweka sehemu kavu kusubiri kimpatie majibu ndani ya muda huo wa kati ya dakika 20 na 40.

Gharama zake
Hakuna uhakika juu ya bei kamili ya kipimo hicho. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa kitauzwa kwa Dola za Marekani 17.50 sawa na Sh 27,300.
 
uwezo kwa watanzania itakuwa janga gharama tu ndio inagomba maana wengi wanahongwa/kuhonga 1000-5000 wanaridhika kwa hii more 27000 ni ngumu sijui
 
Kitakachofaa ni cha kupima kwa macho lakini hata walete cha kipima sijui hewa ni kazi bure maana kinachotakiwa ni namna ya kuzuia maambukizi yasienee kwa kasi.Sasa hata icho cha kupima mate kikija hapa bongo msaada wake nini hasa tofauti na hivi tulivonavo vinavopima damu
 
nimeona documentary moja ya south Africa...wao walishavipata hivyoo na wanavitumia kwa sasa..nasikia ni efficency kuliko vile vya kuweka damu.
 
nimeona documentary moja ya south Africa...wao walishavipata hivyoo na wanavitumia kwa sasa..nasikia ni efficency kuliko vile vya kuweka damu.
ila wanasayansi wetu si hua wanatuambia kua denda ni salama!! hasa kama kwenye mate kuna umeme huo usalama unatokeaga wapi?
 
Sasa wale wanasayansi walio tuambia kua ukimwi ukimwi haukai kwenye mate inamaana walitulisha matango pori

Daah kwaiyo hizi kiss za kisasa kama za kina wema hakuna hatari ya kuambukizana hapo?
 
Back
Top Bottom