UKIMWI huchukua muda gani kuonesha dalili?

kiongozi naomba kukuuliza pia apa kwenye fangasi wa koo maana nina pacha wangu anasema koo linamsumbua now ni kama mwaka sasa.

na anasema anapata lympth node kweny shingo mara kwa mara na ata akikooa koo linakua kavu na kama kikoozi kikavu..kajaribu pima HIV mwaka sasa na kila baada ya miezi anapima ila yuko safi xo inaweza ikawa ndo iyo fungusi ya koo au..na kama n yenyewe matibabu yake n yapi au aende hospital gani wamfanyie check up
n.b ni mzee wa uvinza sana
 
...Nashukuru kwa post yako hapo juu. Unaweza kueleza kidogo kuhusu mahusiano ya HIV na fungus? Nimeshughulika na wagonjwa wa hili tatizo mara mbili, na mara zote tatizo la fungus limejitokeza, wa kwanza ilikuwa fungus kooni na mwingine alikuwa anapoteza kumbu kumbu kwa kipindi fulani, then madaktari wakasema tumpime CT-Scan ili kuona kama fungus imepanda kichwani.
kiongozi post chini ni yako.
 
Acha ngono! Ngono zote nje ya ndoa ni ngono zembe! Dalili kubwa kuliko zote za ukimwi ni kufanya ngono nje ya ndoa!
 
UKIMWI is no longer a death sentence. Bugia ARV maisha yasonge, kula mbogamboga, kunywa Juice za matunda, kunywa maji ya kutosha. Utajikuta unazika wazima, wewe unadunda.
Kuongea hivi rahisi sana ukishaambiwa eeh bwana umepigwa shoti jasho lazima likutoke unaona sasa nakufa
 
Watu wote wangekuwa kama Ragnar Loth humu JF mambo yangekuwa mazuri sana, siku hizi Jf imevamiwa na vijana wa fb comments nyingine zimekuwa za kitoto na kipuuzi hadi inakera.
 
Ukimwi una stage kuu tatu :

1) Acute HIV Infection / Primary stages.
Baada ya vijidudu kuingia mwili lazima utoe reaction ya mabadiliko.
Hii ni hatua ya kwanza kabisa kwa mtu aliyeambukizwa.
Inachukua week 2 hadi 6 kuonesha dalili kama, rushes, fever, headache, kuvimba tezi za shingo n.k
Dalili zinadumu kwa week 2 then zinapotea unakuwa kawaida.

2)Chronic HIV Infection.
Vijidudu vinaendelea kuzaliana ndani ya mwili kwa kiwango kidogo mno.
Mara nyingi hii hatua haina dalili za ugonjwa, wagonjwa huwa na afya njema kabisa, lkn anaambukiza kama kawaida.
Inachukua muda mrefu hata zaidi ya miaka 10 na kuendelea.

3)AIDS.
Vijidudu vinakuwa vimezaliana na kuongezeka kwa wingi mno,
Kinga ya mwili inakua imeshaharibika na kuelekea kumezwa na vijidudu kabisa.
CD4 zinashuka hadi chini ya 200cells/mm cubic.
Ndio hapa magonjwa nyemelezi yanakuandama, kama malaria, kuhara na mengine mengi.
Bila matibabu wala dawa ya aina yeyote mgonjwa anaweza survive kwa certainly miaka 3.

" WINDOW PERIOD ".

Window period ni muda kuanzia muda ulipopata infenctions hadi muda ambao vipimo vitaonesha umeathirika.
Ndani ya window period mgonjwa anaweza kuwa ameambukizwa lakini vipimo vikaonesha hajaathirika.
Muda huu huchukua zaidi ya week 4 hadi 12.

Kuhusu ipi ni dalili kubwa : Dalili zinatofautiana toka kwa mgonjwa mmoja hadi mwingine, unaweza kuwa na hii dalili mimi nisiwe nayo. Au ukawa na zote kwa pamoja.
Lakini mara nyingi dalili haiwi moja tu, zipo nyingi na sidhani kama ipo moja ambayo ni kubwa kuliko zingine.

Kwa maelezo zaidi nenda kituo cha afya.
Umeeleza vizuri
 
HIV hanauwezo wa kusababisha UKIMWI...

UKIMWI unatokana na life style ya mtu..kila mtu anaweza kupata UKIMWI na akapona kama atazingatia lishe bora.
 
Kuna dawa Uingereza walianza kuijaribu tangu 2014, inamaliza wadudu wote hatavwale waliojificha hivyo mgonjwa anaacha kutumia ARVs. Hata hivyo hawajathibitisha kuwa aliye acha kutumia dawa hawezi kumuambukiza mtu na pia kuna wagonjwa ambao immune system zao hazitakaa zirejee kama awali.
So hao ambao immune zao hazitarudi ,wanakuwa na deformed body?
 
Halafu tumepunguza awareness ya Ukimwi kwa kuchukulia kwamba kila mmoja ameshaufahamu.Tumejaza matangazo ya simu.Tuige mfano wa tangazo la Coca.Nani asiyeifahanu coca cola lakini kila siku inatangazwa.Swali lako kama walivyosema wengi hapo baada ya miezi mitatu dalili za kwanza zinaanza kujitokeza lakini nashauri watu wakapime hospital
 
Inategemea na immune system yako wengine wanakaa mpaka miaka 10 baada ya maambukizi ndiyo wanajulikana. Dalili pia hutofautiana, wengine hupata magonjwa nyemelezi kinga inavyozidi kushuka kama TB na pneumonia ndipo wanapojulikana wana HIV pia.
Miaka kumi mingi sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom