mpiga era
JF-Expert Member
- Aug 7, 2016
- 2,079
- 2,255
Habari wana JF, naomba kufahamu upungufu Wa kinga mwilini unachukua muda gani kuonekana? Punde baada ya kuupata? Na ipi ni dalili kuu kuliko zote? Na kwenye kipimo huonekana baada ya muda gani?
Nawasilisha.
PIA SOMA:
=========
MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
Nawasilisha.
PIA SOMA:
Kwa wanaoogopa kupima, hizi zinaweza kuwa dalili za UKIMWI
By DK CHRIS Watu wengi wamekuwa waoga kupima virusi vya Ukimwi kutokana na madhara ya kisaikolojia yanayojitokeza baada ya mtu kujijua ana ugonjwa huu, hivyo wengi huamua kubaki na sintofahamu tu. Kwa ambao hawajawa tayari kupima Ukimwi, dalili zifuatazo zinaweza kuwa za ugonjwa wa Ukimwi...
www.jamiiforums.com
Siku ya UKIMWI Duniani: Watu Milioni 74.9 wameugua ugonjwa huo tangu ulipogundulika
Siku ya UKIMWI Duniani huadhimishwa kila tarehe 01 Desemba ikitoa mwanya kwa kusherekea na kuunga mkono jitihada zinazofanyika Ulimwenguni za kuzuia maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI, kuongeza uelewa kuhusu UKIMWI na kuwafariji wale waishio na Virusi hivyo Tangu Siku ya UKIMWI ilipoanza...
www.jamiiforums.com
MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
========Ukimwi una stage kuu tatu :
1) Acute HIV Infection / Primary stages.
Baada ya vijidudu kuingia mwili lazima utoe reaction ya mabadiliko.
Hii ni hatua ya kwanza kabisa kwa mtu aliyeambukizwa.
Inachukua week 2 hadi 6 kuonesha dalili kama, rushes, fever, headache, kuvimba tezi za shingo n.k
Dalili zinadumu kwa week 2 then zinapotea unakuwa kawaida.
2)Chronic HIV Infection.
Vijidudu vinaendelea kuzaliana ndani ya mwili kwa kiwango kidogo mno.
Mara nyingi hii hatua haina dalili za ugonjwa, wagonjwa huwa na afya njema kabisa, lakini anaambukiza kama kawaida.
Inachukua muda mrefu hata zaidi ya miaka 10 na kuendelea.
3)AIDS.
Vijidudu vinakuwa vimezaliana na kuongezeka kwa wingi mno,
Kinga ya mwili inakua imeshaharibika na kuelekea kumezwa na vijidudu kabisa.
CD4 zinashuka hadi chini ya 200cells/mm cubic.
Ndio hapa magonjwa nyemelezi yanakuandama, kama malaria, kuhara na mengine mengi.
Bila matibabu wala dawa ya aina yeyote mgonjwa anaweza survive kwa certainly miaka 3.
WINDOW PERIOD
Window period ni muda kuanzia muda ulipopata infenctions hadi muda ambao vipimo vitaonesha umeathirika.
Ndani ya window period mgonjwa anaweza kuwa ameambukizwa lakini vipimo vikaonesha hajaathirika.
Muda huu huchukua zaidi ya week 4 hadi 12.
Kuhusu ipi ni dalili kubwa : Dalili zinatofautiana toka kwa mgonjwa mmoja hadi mwingine, unaweza kuwa na hii dalili mimi nisiwe nayo. Au ukawa na zote kwa pamoja.
Lakini mara nyingi dalili haiwi moja tu, zipo nyingi na sidhani kama ipo moja ambayo ni kubwa kuliko zingine.
Kwa maelezo zaidi nenda kituo cha afya.
Hapa kuna ishu mbili kuu...kuna kuambukizwa na kugundua kama umeambukizwa.
Njia pekee ya kujua kama umeambukizwa ni kupima...kitaalamu inaaminika kuwa vipimo vinaweza kuonyesha umeambukizwa baada ya wiki mbili hadi sita na kuendelea.
Kitaalamu huwezi kuanzishwa dawa mpaka CD4 zako zishuke kufikia kiwango fulani. Hivyo, kama umeambukizwa na hujapima na mwili wako una uwezo wa kuhimili VVU (yaani CD4 hazishuki), basi utaishi tu kama kawaida, na siku zote utajiamini kuwa huna vvu.
Na bado Wataalamu wanashinda maabara kutafuta ni nini haswa kinatokea kwa hao wenye uwezo wa kuwahimili vvu na wakaishi bila kuathirika maisha yao yote.
Kwa hiyo mtihani hapa ni kwamba huwezi kujua kama mwili wako unao huo uwezo mpaka upime, sasa ndio ujue kumbe unaishi na vvu na hawana uwezo wa kukuangamiza...sasa ni wangapi wenye uwezo wa kuhimili matokeo ya kuwa wanaishi na vvu? kwani unaweza kupima ndio ukaathirika kisaikolojia, na mawazo ndio yakaangamiza CD4 zako badala ya VVU.
Kuwa na VVU kwenyewe sio ugonjwa, hivyo ni ngumu kutarajia kuwepo kwa dalili za moja kwa moja zitakazofanana kutoka Mtu mmoja hadi mwingine...kinachotokea ni kwa kuwa kinga inapungua mwilini basi ugonjwa wowote unaweza kukushambulia na kukupelekesha.
Kwahiyo, ukiweka mambo kwenye mizani ni kuwa faida ya kupima ni kubwa kuliko kuishi tu kutegemea zali la mentali.