Nimekugongea LIKE sio kwamba nimependa ulivyopata UKIMWI, ila ujasiri wako huo, Basi MUNGU wetu aonaye sirini na haja za mioyo yetu akakujibu siku ya shida yako, mtumaini yeye tu, usimwangalie mwanadamu awaye yeyote, kama yeye aliruhusu uwe hai hadi leo hii basi ataruhusu na MEMA yaje kwako.
Kuna wimbo wa Bukuku-Bahati naupenda sana una maneno yanasema hivi; wewe ni MUNIGU tena ni MUNGU, hivi leo nimejua wewe ni MUNGU, kama ulivyoruhusu mabaya yaje kwangu, ndivyo uruhusu na mema yanipate, kama ulivyoruhusu MAGONJWA yaje kwangu ndivyo uruhusu UZIMA uje kwangu........Ni wimbo ambao una ujumbe mzito sana sana, MUNGU wangu wa Mbinguni ninayemtumaini na kumtegemea akakujibu haja ya MOYO wako leo, akasikie kilio chako, akasikie ombi lako leo, umuitapo akujibu upesi tena Martha Mwaipaja nae anasema hivi, Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi ila ni kikombe tu ambacho ni lazima apitie, usimwone mtu anapita kwenye jaribu........Muombe MUNGU aondoe kikombe hicho, hujatenda dhambi ndugu.
Abihudi Misholi kwenye latest CD aliyotoa ana wimbo pia unasema kuwa, hakuna kikombe kinachoponyesha UKIMWI, kikubwa ni TOBA na hii ndio itakuweka huru. Basi nakuombea toba ya kweli, uzidi kuwa huru katika Kristo YESU, sote tuseme AMen