UKIMWI bila Pesa ni hatari...

UKIMWI bila Pesa ni hatari...

Mariangonyani

Member
Joined
Mar 31, 2013
Posts
39
Reaction score
59
Siku nilipogundulika nina VVU nilishtuka ila nikaja kuzoea na nikasema sitakuwa kwenye mahusiano na ikawa hivyo; tatizo ni siku za karibuni familia yangu haijui tatizo langu na imeyumba kiuchumi.

Kiukweli naona nafika mwisho, sina hela! Muda mwingine hata ya kula; nahitaji kwenda hospital pia nashindwa.

Mungu anilinde na marafiki mniombee nina wakati mgumu sana!
 
Nimekugongea LIKE sio kwamba nimependa ulivyopata UKIMWI, ila ujasiri wako huo, Basi MUNGU wetu aonaye sirini na haja za mioyo yetu akakujibu siku ya shida yako, mtumaini yeye tu, usimwangalie mwanadamu awaye yeyote, kama yeye aliruhusu uwe hai hadi leo hii basi ataruhusu na MEMA yaje kwako.

Kuna wimbo wa Bukuku-Bahati naupenda sana una maneno yanasema hivi; wewe ni MUNGU tena ni MUNGU, hivi leo nimejua wewe ni MUNGU, kama ulivyoruhusu mabaya yaje kwangu, ndivyo uruhusu na mema yanipate, kama ulivyoruhusu MAGONJWA yaje kwangu ndivyo uruhusu UZIMA uje kwangu........Ni wimbo ambao una ujumbe mzito sana sana, MUNGU wangu wa Mbinguni ninayemtumaini na kumtegemea akakujibu haja ya MOYO wako leo, akasikie kilio chako, akasikie ombi lako leo, umuitapo akujibu upesi tena Martha Mwaipaja nae anasema hivi, Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi ila ni kikombe tu ambacho ni lazima apitie, usimwone mtu anapita kwenye jaribu........Muombe MUNGU aondoe kikombe hicho, hujatenda dhambi ndugu.
Abihudi Misholi kwenye latest CD aliyotoa ana wimbo pia unasema kuwa, hakuna kikombe kinachoponyesha UKIMWI, kikubwa ni TOBA na hii ndio itakuweka huru. Basi nakuombea toba ya kweli, uzidi kuwa huru katika Kristo YESU, sote tuseme AMen
 
Pole sana dada,,, japokuwa maelezo yako hayajanyooka vizuri lakini umeeleweka..

Itapendeza kama ukitueleza in details, uligunduliwa mwaka gani, na kazi uliacha lini?, na je una familia may be mme na watoto, etc

Mungu akuongoze na akuponye kabisa vvu,, kwa imani ninaamini VVU vitaondoka vyote mwilini mwako kwa uwezo wa Mungu wetu..Amina, ubarikiwe sana dada
 
Pole sana.

Usiwe mnyonge na kukosa raha. Mshukuru Mungu katika yote. Unatakiwa kupambana, maisha ni mapambano, tafuta chakula kwa njia halali usikubali kukaa tu na njaa huku ukiwaza na kujiumiza roho. Ikibidi ongea na watu wanaoweza kukusaidia hata kukupa chakula tu, kuna watu wanamwaga chakula kila siku hawajui wampe nani, unaelelwa wakati mwingine mtu yupo radhi akupe chakula na asikupe fedha, hivyo unaweza kuomba chakula usione aibu.

Nawashukuru sana jamani mmenitia moyo hadi machozi yamenitoka. Mungu ananipigania ila naanza kukata tamaa, niliupata 2008 na sijaanza kutumia dawa; bado Mungu ananiongoza.

Tatizo maisha yamekuwa magumu sana kwa sasa kiasi hadi nashindwa kula, yote ni woga wa kuwashirikisha marafiki na familia ila naamin Mungu atajibu maombi yangu
 
Kwa ushauri tu..shirikisha ht mama yako..ili upate mtu wa kukupa moyo na updates mbalimbali..ukikaa kimya hivyo unajiumiza..ss na unavyokaa na mawazo sana ss...Cd4 zitashuka utapata magonjwa nyemelezi..na magonjwa nyemelezi hayo ndg kuyatibu ni pesa..tena si ndgo...sasa shirikisha mtu...hasa mama na baba...watajua cha kukusaidia ukikwama
 
Nawashukuru sana jamani mmenitia moyo hadi machozi yamenitoka. Mungu ananipigania ila naanza kukata tamaa, niliupata 2008 na sijaanza kutumia dawa; bado Mungu ananiongoza.

Tatizo maisha yamekuwa magumu sana kwa sasa kiasi hadi nashindwa kula, yote ni woga wa kuwashirikisha marafiki na familia ila naamin Mungu atajibu maombi yangu
Pole sana....ila nachelewa kuamini kama ni kweli ama ni utapeli mpya wa mitandaoni,....samahani wakuu msinipige mawe ni katika hali ya kuwaza na kuwazua kwa kina.
 
Pole sana....ila nachelewa kuamini kama ni kweli ama ni utapeli mpya wa mitandaoni,....samahani wakuu msinipige mawe ni katika hali ya kuwaza na kuwazua kwa kina.
Siwezi kuwa tapeli maana sijaomba hela ya mtu.

Nimeongea hivi ili nishauriwe sababu sijawahi mshirikisha mtu, najua hapa sijulikani ndo maana nikaongea hivi wala sihitaji mia ya mtu, napenda kushauriwa tu
 
^^
Mungu mwenyezi ajuaye idadi kamili ya mifupa ikamilishayo mwili wako,,akutimizie mahitaji yako
^^
 
Vumilia....2015 tablets will come-up!! For curing
 
Kaunga nashukuru kwa kunishtua...

Kwa mtazamo wangu hapa tatizo ni kubwa zaidi ya pesa Dear.

Ikiwa tu frustrations zingine za Kimaisha ambazo zinaweza kuwa solved in the long run huhitaji sana watu wa karibu kukufariji na kukupa moyo - Upande wa kujitambua kuwa ni mwathirika bila kuwa na mtu wa ku share, kuongea, kujadili na kufarijiana ndio worse.

Naamini kuwa hata ikitokea akapewa msaada wa pesa, haitakuwa msaada sana kama vile yeye kupata support ya familia na watu wake wa karibu kwa kutambua hali yake Ki afya na kumkubali jinsi alivyo. Imagine kakiri kapata virusi hivyo toka 2008 na bado afya yake ni nzuri na hajaanza kupata vidonge. Hiyo ni sababu tosha kabisa ya kuendelea kuwa na matumaini na pia kigezo kikubwa kutumia kuwashirikisha ndugu na jamaa. Si wote but kwa kuanzia na wale ambao ni watu wazima na wanaweza play positive part katika hili.

Hata hivyo ikitokea ikaonekana ni muhimu kwa sie kuhamasisha nitahusika kwa asilimia 100.
 
Mariangonyani... Naomba nikupongeze kwa ujasiri na nguvu uliyo nayo. Kutitambua na kujikubali kuwa una virusi vya Ukimwi ni stage ambayo huwasumbua wengi. Na wavukao hapo huangukia kwa wema ama ubaya - Kwa kuchanganyikiwa na kuzidi hatarisha maisha ya wenzie ama kwa kutambua kuwa ni muhimu akajitazamia na kulinda afya yake.

Hii ni habari nzuri na wewe ni mfano tosha kua kuwa na Virusi vya Ukimwi si Ukimwi wenyewe. Una miaka mitano toka umejitambua, pengine una miaka mingi zaidi ya kuishi na virusi ila hapo 2008 ndipo ulipima na kutambua.

Sasa hivi miaka inavyozidi kwenda ndipo kunakuwa na unafuu katika jamii yetu ilojaa unafiki katika kulikabili suala la Ukimwi. Hii ambayo wewe umeweka siri rohoni kwako ni uthibitisho tosha kuwa yawezekana hata kuna ndugu, jamaa ama marafiki pia wameathirika ila nao wameweka siri na wanaumia kama wewe unavyoumia.

Najua hapa ni rahisi kwa wengi wetu kukupa ushauri, ni rahisi sana kutoa ushauri, ila jambo kama hili linapo kukuta ndipo unajua jinsi gani utakuwa.

Kuna mengi pia ni muhimu kujua ili kuwez kutoa ushauri ambao unaweza faa zaidi, kama vile Umeolewa na upo ndani ya ndoa? Unajitegemea ama unategemea? Una ndugu/jamaa/rafiki ambae ni mtu mzima wa kuweza kumfikishia hali yako kwa yeye kuweza kulipasua kwa urahisi kwa ndugu? Jamii ilokuzunguka ni wanyanyapaaji?

Kwa sasa zaidi mie naona the best option ni kufunguka na hasa zaidi kujiunga na makundi ya watu wanao ishi na virusi vya Ukimwi. Sababu huko wanabadilishana mawazo, wanapeana ushauri, wanasimuliana vikwazo wanavyokutana navyo. Na muhimu zaidi wana elewa from first hand kuwa mwenzie ni vipi hasa alivyo na wakati mgumu kila stage. Toka kupima mara ya kwanza, kutambua kuwa ni mwathirika, kwanza kwa hatua za maradhi nakadhalika.

I am so proud of you. With proper care ni wazi utaishi miaka mingi. Kikubwa utengeneze mazingira ya furaha na Amani.

Kila la kheri.
 
Last edited by a moderator:
Nimekugongea LIKE sio kwamba nimependa ulivyopata UKIMWI, ila ujasiri wako huo, Basi MUNGU wetu aonaye sirini na haja za mioyo yetu akakujibu siku ya shida yako, mtumaini yeye tu, usimwangalie mwanadamu awaye yeyote, kama yeye aliruhusu uwe hai hadi leo hii basi ataruhusu na MEMA yaje kwako.

Kuna wimbo wa Bukuku-Bahati naupenda sana una maneno yanasema hivi; wewe ni MUNIGU tena ni MUNGU, hivi leo nimejua wewe ni MUNGU, kama ulivyoruhusu mabaya yaje kwangu, ndivyo uruhusu na mema yanipate, kama ulivyoruhusu MAGONJWA yaje kwangu ndivyo uruhusu UZIMA uje kwangu........Ni wimbo ambao una ujumbe mzito sana sana, MUNGU wangu wa Mbinguni ninayemtumaini na kumtegemea akakujibu haja ya MOYO wako leo, akasikie kilio chako, akasikie ombi lako leo, umuitapo akujibu upesi tena Martha Mwaipaja nae anasema hivi, Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi ila ni kikombe tu ambacho ni lazima apitie, usimwone mtu anapita kwenye jaribu........Muombe MUNGU aondoe kikombe hicho, hujatenda dhambi ndugu.
Abihudi Misholi kwenye latest CD aliyotoa ana wimbo pia unasema kuwa, hakuna kikombe kinachoponyesha UKIMWI, kikubwa ni TOBA na hii ndio itakuweka huru. Basi nakuombea toba ya kweli, uzidi kuwa huru katika Kristo YESU, sote tuseme AMen
Amein amein
 
Kaunga nashukuru kwa kunishtua...

Kwa mtazamo wangu hapa tatizo ni kubwa zaidi ya pesa Dear.

Ikiwa tu frustrations zingine za Kimaisha ambazo zinaweza kuwa solved in the long run huhitaji sana watu wa karibu kukufariji na kukupa moyo - Upande wa kujitambua kuwa ni mwathirika bila kuwa na mtu wa ku share, kuongea, kujadili na kufarijiana ndio worse.

Naamini kuwa hata ikitokea akapewa msaada wa pesa, haitakuwa msaada sana kama vile yeye kupata support ya familia na watu wake wa karibu kwa kutambua hali yake Ki afya na kumkubali jinsi alivyo. Imagine kakiri kapata virusi hivyo toka 2008 na bado afya yake ni nzuri na hajaanza kupata vidonge. Hiyo ni sababu tosha kabisa ya kuendelea kuwa na matumaini na pia kigezo kikubwa kutumia kuwashirikisha ndugu na jamaa. Si wote but kwa kuanzia na wale ambao ni watu wazima na wanaweza play positive part katika hili.

Hata hivyo ikitokea ikaonekana ni muhimu kwa sie kuhamasisha nitahusika kwa asilimia 100.

Nakubaliana na wewe, nafikiri nimefikiria mbele zaidi far ahead of time. naona dada hafunguki sana, na kama anafikiri anahitaji sana msaada wa kujikwamua she needs to funguka hata kama si jamvini, na kwa mtazamo wangu wewe kwa reputation yako akifunguka zaidi kwako na ukija kwetu au kwa wadau baada ya kujiridhisha na taarifa zake ukisema anahitaji financial assistance basi tunaweza kujikuna mkono unapofika. la kuna wadau humu wana kampuni zao na wanaweza kumpa kibarua ambacho kitaweza kumsustain. Pamoja na counseling na whatever, financial stability ni muhimu kwa mtu yeyote na kwa mgonjwa wa Ukimwi ni zaidi IMO.
 
Back
Top Bottom