Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Ukimtazama mwanamke kwa kumtamani, tayari umefanya naye uzinzi moyoni.
Yesu Kristo alitoa onyo hilo zito kuhusu dhambi ya uzinzi usioonekana kwa macho ya kawaida lakini unaotekelezwa ndani ya moyo wa mtu. Katika Mathayo 5:28 anasema hivi:
"Lakini mimi nawaambia, Kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake." (Mathayo 5:28)
Maneno hayo yanabeba uzito mkubwa katika kizazi chetu, ambacho mitindo ya mavazi na maisha ya kisasa yanazidi kuamsha tamaa za mwili kupitia macho ya wanaume wengi.
Wanaume wengi hukumbwa na tamaa ya mwili wanapoona wanawake waliovaa mavazi yanayosisimua hisia zao kama vile:
Macho ni mlango wa moyo. Mwanaume huvutwa kwa kuona. Hivyo, mwanamke aliyevaa mavazi yanayoamsha tamaa ya mwili, humuweka mwanaume katika hatari ya dhambi ya uzinzi wa moyoni.
Mavazi yasiyo ya staha ni kichocheo cha dhambi ya uzinzi wa moyoni. Wanawake wanaovaa mavazi yasiyositiri mwili wanapaswa kujua kuwa wanawakwaza wanaume. Yesu alisema:
“Lakini mtu atakayemkwaza mmojawapo wa wadogo hawa waaminio, afadhali afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, azamishwe kilindini mwa bahari” (Mathayo 18:6)
Huu hapa ushauri wa kimaadili kwa Wanaume na Wanawake
1. Kwa Wanawake:
Vaa kwa heshima na kiasi. Sio kila fashion au mtindo maarufu mitandaoni ni halali mbele za Mungu. Elewa thamani yako haiko katika maumbile yanayoonekana, bali katika tabia ya utakatifu (1 Petro 3:3-4).
Uwe msaada kwa ndugu zako wanaume kwa kuepuka mavazi yanayowatia majaribuni.
2. Kwa Wanaume:
Linda macho yako. Ayubu alisema: "
“Nimefanya agano na macho yangu yasimtazame msichana kwa kumtamani." (Ayubu 31:1)
Omba neema ya kujizuia kutazama picha za utupu na uepuke mazingira ya majaribu. Kumbuka kuwa uzinzi wa moyoni ni dhambi kamili mbele za Mungu, hata kama haujafanyika kimwili.
Uzinzi wa moyoni ni hatari zaidi kwa sababu hauonekani kwa macho ya binadamu, lakini Mungu anaona kila wazo na nia ya moyo. Hebu tuamue kuwa watakatifu si kwa nje tu, bali kwa ndani pia.
Kina dada msivae hivyo mitaani, mnawakwaza kina kaka. Kumbukeni maneno haya ya Yesu:
"...Mambo yanayosababisha watu watende dhambi hayana budi kutukia. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha" (Luka 17:1-4)

- Suruali za kubana zinazochora wazi maumbile ya mwili
- Sketi fupi zinazoacha wazi mapaja
- Nguo za wazi zinazoonyesha kifua, tumbo, au mabega