Ukimfumania mwenzi wako nyamaza

na hilo ni wazo linahitaji kufanyiwa kazi asante kwa ushauri wako mkuu..
 
Swala ni kutokwenda kichwa kichwa kama mbuzi aliyekatwa shingo,uwe umejipanga na maamuzi unayo tayari
nikiitwa leo nikamfumanie Mr siendi ili iweje baada ya hapo?
Halafu Chauro nilimuona leo Mr wako kama anaingia maeneo ya Coral Beach Hotel vipi ana mkutano kule ??? Lol!!!
 
Anahangaikia mlo wa watoto Finest.
Ukianza kuwa negative na mwenzi wako hata akiweka kijiko upande utakuwa na wasiwasi mwisho wa siku mwenyewe ndo utajikuta unaumia.

Halafu Chauro nilimuona leo Mr wako kama anaingia maeneo ya Coral Beach Hotel vipi ana mkutano kule ??? Lol!!!
 
lizzy, kwa hiyo wewe utapiga kelele watu waje waone? eeh? mbaya zaidi ni pale ambapo hamtaachana!
 
Fumanizi halipangwi unaweza ukapoteza fahamu, au ukatoa ile bastola yako ukamaliza mtu so hakuna fomula hapa
 
Ndio maana waswahili wakauliza "aibu yao aibu yangu? Aibu yao wenyewe" Mimi nikifumania ni varangati tu! Kwa nini aibu iwe yangu na isiwe ya hao wanaofungulia kofuli kila mtu. Kha yani mtu anidhalilishe kwa kucheat afu bado unambie aibu yangu. Sioni aibu wala nini as long as sina tabia za kizinzi kama wao. Aibu nione ya nini kwani mimi ndo cheater. Hata majirani woote wajae aibu atabaki nayo yeye mwenyewe, na in most cases nikuambie watu wanamtoa thamani cheater na si anaekuwa cheated!! Kwa hiyo mliofumania na kujaza umati muwe na amani tu anayechekwa na jamii ni huyo mzinzi wala si wewe kwani ulimtuma.
 
kuna jamaa mwingine magomeni alimfumania mke wake wakawatoa nje uchi wa nyama na jamaa yake (miaka ya 1995) baadae watu wazima wakawashauri ndio wakawavisha khanga na kuwapeleka polisi. Cha ajabu jamaa baada ya mwezi akamrudia mkewe wakahama mtaa kwa aibu wote wawili
 
Cha kufanya ni kumpa kisago kwanza huyo hawala kama una ubavu lakini angalia situations, mke utamkuta home maana pale atakimbia ukifika nawe home mpe kisago hakuna kumuuliza, hata kidogo upo mzee
 
Inashauriwa kuwa ukimfumania mwenzi wako-mke/mume, usipige kelele ili watu wasijue,maana watakucheka kuwa mpaka mwenzi wako kafika hatua hiyo wewe una dosari mahali au huwajibiki ipasavyo ndio maana kaamua kutoka.Kaa kimya kama kuachana iwe kimya kimya kulinda heshima yako.

Dhana potofu nyingine hii!! Mwenza wako akikuchiti haina maana kuwa wewe una dosari na huwajibiki ipasavyo (ingawa yawezekana pia). Kuna watu tu hawana maadili, mapepe, washobokaji, vichwa juu, na kadhalika. Yaani hata ufanyeje mwenzako anatamani vingine tu. Sasa ukiwa na mtu wa aina hiyo ama kubali tu kuwa mnyonge au sepa.
 
Mh! hii mada noma!! Napita tu wakuu maana bibi yangu alikuwa na kamsemo ukitaja nyoka shika fimbo mkononi......... naogopa kuchangia kwasababu sijui nitafanya nini na nitaacha nini lakini chochote kutikea.
 
Ushauri mwingine kama nguvu za giza
Kwanza niambie kama wewe una mwenza na kama unaye kweli hapa tunaweza kuongea[/QUO
Nimo kwenye taasisi kwa muda mrefu.

Kama uko kwenye taasisi muda mrefu huu ushauri wako hapa nautilia mashaka maana uchungu wa mke au mume anaujua mke au mume muhusika na unapokuta mkeo yuko kitandani na mwanaume mwingine huo uchungu wake sijui kama unaelezeka
Ndo maana kweney issue za murder provocation as defence inakubalika kwenye issue za kumfumania mke na mtu akachukua reaction hapo hapo defence ya provocation inakubalika
Sasa unapotuambia eti unyamaze na uuchune ili kulinda heshima, heshima mbona ishapotea toka hapo. Kitendo cha kutembea nje ya ndoa ni cha kukushushia heshima muhusika bila kujali kuwa umemkamata au hajakamatwa
 
Hakuna kitu kinachoniudhi kama tabia ya watu kuwalaumu watu waliokuwa cheated. Utasikia eti jichunguze mapungufu ulonayo mpaka mwenzio akatoka nje ya ndoa. Kha. This is a language used to justify cheating. Kwa hiyo mume/mke aki cheat kosa ni la mwenza kwa kuwa hakutimiza wajibu? Afu macheater wanaipenda hiyo theory. Na wenye vimada au vidumu zaidi ya kimoja vyote vijichunguze kipi hawatimizi kwa huyo mfalme! Cheating ni ugonjwa hakuna justification ya aina yoyote. Kama upate kitu roho inataka toka kwa mwenza wako achana nae kabla ya kuanza kukitembeza kwa wengine mtaja uana kwa magonjwa bure.
 
Dhana potofu nyingine hii!! Mwenza wako akikuchiti haina maana kuwa wewe una dosari na huwajibiki ipasavyo (ingawa yawezekana pia). Kuna watu tu hawana maadili, mapepe, washobokaji, vichwa juu, na kadhalika. Yaani hata ufanyeje mwenzako anatamani vingine tu. Sasa ukiwa na mtu wa aina hiyo ama kubali tu kuwa mnyonge au sepa.
Leo umeongea point kweli.....
 
Hakuna kitu kinachoniudhi kama tabia ya watu kuwalaumu watu waliokuwa cheated. Utasikia eti jichunguze mapungufu ulonayo mpaka mwenzio akatoka nje ya ndoa. Kha. This is a language used to justify cheating. Kwa hiyo mume/mke aki cheat kosa ni la mwenza kwa kuwa hakutimiza wajibu? Afu macheater wanaipenda hiyo theory. Na wenye vimada au vidumu zaidi ya kimoja vyote vijichunguze kipi hawatimizi kwa huyo mfalme! Cheating ni ugonjwa hakuna justification ya aina yoyote. Kama upate kitu roho inataka toka kwa mwenza wako achana nae kabla ya kuanza kukitembeza kwa wengine mtaja uana kwa magonjwa bure.

Hapo umenena
Madhaifu ya ndoa yamekuwa ndio wimbo wa cheaters wengi
kama kuna madhaifu kwa nini kama wanandoa msikae chini kuyamaliza na kuzungumza mpaka kwenda nje ya ndoa.
Haina maana kama kuna madhaifu ndo mtu utoke nje ya ndoa
 
Inashauriwa kuwa ukimfumania mwenzi wako-mke/mume, usipige kelele ili watu wasijue,maana watakucheka kuwa mpaka mwenzi wako kafika hatua hiyo wewe una dosari mahali au huwajibiki ipasavyo ndio maana kaamua kutoka.Kaa kimya kama kuachana iwe kimya kimya kulinda heshima yako.

daaahhh, ungeweka warning kabla mtu hajaanza kusoma hii, nimepaliwa vibaya sana na nilichokuwa nakunywa hapa sababu ya kicheko, LOL...hivi kumbe kuna watu hupiga yowe wakifumania eeh?...ha ha ha ahaaa

haya bana, vigezo na masharti yatazingatiwa...lol!
 
Hiyo nguvu ya yowe utakuwa nayo Mbu
hapo ukifumania waweza pata heart attack ukafa eti ile kitu inauma wacha habari yake
 
Kwa uzoefu wangu wa dunia mambo ya kucheat watakuwa wanayajua tu majirani ila hawakwambii.Kibaya zaidi hata ndugu au marafiki wa karibu wanajuaga lakini wanaminya.Ukimuacha tu utasikia stori kibao.KWA HIYO SIKUBALIANA NA MUANZISHA THREAD KWA WATAJUA.WANAJUA TAYARI ILA TU SEMA MAMBO YA KUPIGA MAKELELE NA KUPIGANA SI YA KISTARABU
 
Hakuna kupiga kelele za nini, kwanza unampa kisago huyo bwana wake lakini unaangalia situations kama unamuweza, Bibi utamkuta home unampa kisago na yeye, kujaza watu ndio ishara kwamba mke/mme sio waamnifu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom