Ukikutana na abiria anachungulia unachofanya kwenye simu yako bila ridhaa yako unafanyaje?

JF Toons

Digital Art by JF
Feb 19, 2024
32
66
abiria.jpg

Baadhi ya abiria wamekuwa na tabia hii ya kuchungulia kinachoendelea kwenye simu za majirani zao wanapokuwa kwenye usafiri wa umma bila kujali hawapaswi kufanya hivyo.

Ukikutana na abiria kama huyu akiwa anachungulia unachofanya kwenye simu yako bila ridhaa yako unafanyaje?
 
Kuna screen protecor za kisasa ambazo ni Private Screen Protector unaweka kwenye simu yako na wa pembeni hawezi kusoma wala kuona chochote.
Aina nzuri ni ya kampuni ya Belkin.Sijui Bongo kama zinapatikana.Ukipiga chabo kutoka pembeni screen unaiona nyeusi.Hakuna unachoona.
 
Kimsingi wewe ndio unatakiwa utunze privacy yako kwenye Public. Mi simfanyi chochote ila nahakikisha natunza usiri wangu. Tujitahidi kuepusha Keri na makwazo kwa wenzetu kwa kutunza privacy zetu.
Nchi zilizoendelea ni mara chache sana utakuta mtu anadokolea macho kwenye simu yako. Kwa Tanzania ni jambo la kawaida sana. Na kuna jingine: kudokolea mtu macho kama panya aliyedakwa shingo. Hili Bongo wanalo sana wanaume hasa Dar.
 
Imenikunbusha November mwaka jana tukiwa kwenye BM tunatoka Arusha kuja Dar, mama mmoja alimwachia mwanaye wa miaka kama 5 hivi simu acheze games, tukiwa mitaa ya Mbwewe kuitafuta Wami mama mtu akapitiwa usingizi, kitoto kikahama siti kikakaa siti ya nyuma yake na kuanza kutazama video, baadaye tunasikia clip zinatoa miguno ya porns, mama mmoja mtu mzima wa kama 40s+ akawa naye amekodoa macho anatazama baadaye akainuka bwana mmoja akapokonya ile simu akamfuata yule mama mwenye mtoto na kumwambia afute clip zote vinginevyo anamfungulia mashitaka.
 
Nchi zilizoendelea ni mara chache sana utakuta mtu anadokolea macho kwenye simu yako. Kwa Tanzania ni jambo la kawaida sana. Na kuna jingine: kudokolea mtu macho kama panya aliyedakwa shingo. Hili Bongo wanalo sana wanaume hasa Dar.
Kwanini nawe unashindwa kutunza usiri wako kwenye vyombo vya umma. Ficha simu yako na sio kuwasha au kuchati huku umeiweka wazi kwa umma.
 
Back
Top Bottom