"Ukikimbia wanakupiga risasi, ukijificha wanachoma nyumba"

"Ukikimbia wanakupiga risasi, ukijificha wanachoma nyumba"

Miss Halima

Senior Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
170
Reaction score
376
"Ukikimbia kuingia chumbani, wanakichoma moto," anasema Fatima, akielezea shambulio la hivi karibuni katika kijiji chake Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria. "Ukitoka nje na kuanza kukimbia, wanakupiga risasi."

Watu hao waliojihami kwa silaha, waliofanya shambulio hilo saa nane usiku (saa 02:00), waligawanyika katika makundi ili kuwazingira wakazi, kundi moja kwenye lango la kuingilia kijijini, jingine katikati na la tatu nyuma.
"Walianza kufyatua risasi bila kujali lolote, wakipiga risasi ovyo ovyo," mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 55 aliambia BBC World Service kwa sauti ya chini.

Ilikuwa ni mojawapo ya mashambulio mengi yaliyosababisha taharuki katika jamii hiyo ambayo wakazi wake wengi ni Waislamu na wanaishi kwa hofu ya kutekwa nyara ili kudaiwa fidia.

Fatima anaelezea jinsi mashambulio hayo yanavyofanyika, "Unaweza kuona pikipiki 100, na kila moja ikiwa imebeba watu watatu."
1787903497761.png
 
Ni washenzi tu hao kobazi, unaua mwafrika mwenzako kisa dini, dini lenyewe la kishenzi


Wewe mbwa bado huachi kubweka?!

Kufa kwa Chuki zako. Utaendelea kuuona Uislam ukikua mbele ya macho mpaka ndani ya familia yako kwa Idhini ya Allah.
 
wapi nimetaja uislam we mshenzi mfia dini?

Nilishakuambia wewe ni mbwa unayebwekea msafara unaosonga mbele.

Chuki hiyo itakuuwa.


Nigeria ni Nchi ambayo inakumbwa na tatizo kubwa la ujambazi na uporaji wa kutumia silaha, Allah Awafanyie Wepesi na Awaondolee mtihani huo.


Kuna makundi mengi ya majambazi wenye silaha wanaopora na kuteka watu Nigeria na kuua.

Wewe hata husomi taarifa wala hufuatilii, ukisoma taarifa kidogo hufuatilii kwa sababu chuki imekujaa moyoni dhidi ya Uislam na Waislam unakimbilia kuandika chuki zako zilizokujaa.


Maana hapo hawajatajwa hata wale Boko Haram ambao ni Makhawaarij mbwa wa motoni wale.

Ni magenge tu ya wahalifu ambayo yamekuwa yanasumbua sana Nigeria.

Wewe unakurupuka tu. Hivi unajua hata adhabu ya hao majambazi ambayo wamewekewa katika Shari'ah ya Kiislam? Katika Dola ya Kiislam watu kama hao wana adhabu kali sana wamewekewa.

Kuna sababu kwanini katika Dola ambazo zimekamata barabara Adhabu za Kishari'ah kama Saudi Arabia hakuna hayo mambo. Husikii sikii hao majambazi wanatamba katika Nchi kama Saudia.

Allah aikate mizizi ya hao majambazi wahalifu.
 
Hiyo Zamfara toka nimeanza kuisikia kuhusu hayo matukio ni kitambo sana,kumbe hadi leo bado hayo mambo yanaendelea. Duh pole yaoo. Na viongozi wa Nigeria wanatazama tu watu wanateketea maana ni miradi yao ya kibiashara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom