Ukijua Mnyama anavyoteseka, bado utakula nyama?

Ukijua Mnyama anavyoteseka, bado utakula nyama?

Nashukuru upande wa pili hawatumii huyu mdudu mana wangekua wanatumia naamini kiumbe anayeitwa nguruwe angekua ameshatoweka duniani na utamu wake
Nani kakwambia hawali?
Ungekuwa unafanya research before, during and after Ramadhan ndio ungejua kama huyu mdudu analiwa au haliwi huko upande wa 2.
Wanawake wengi wa kiislamu ndio huwa hawali kiviile....ila wanaume 75% tunagongana nao kwenye machimbo ya kitimoto.
Machimbo yanadorora sana wakati wa mfungo...asa jiulize walaji ni akina nani na nani!
 
Ina maana hao wanaume ni 5 kati ya 7 mnaogongana nao au kwa idadi ipi?
 
Labda ili la Uchungu tuliweke ivi, kwanini wanawake pamoja na uchungu wanaoupata wakati wa kujifungua(labor) mbona wakishatoka wengi wanatamani wapate mtoto mwingine japokuwa njia yenyewe ya upatikanaji wake anakua amekwisha ijua vizuri
Lilikuwa ni swali.
 
Kwani unakula mnyama au nyama? Kuchinja tu no mateso
 
Anae pigwa Shoka haumii, Just single hit anapoteza faham pengine kifo kabisa, hayo maumv anayapatia wapi
Nakukumbusha tu hata kwenye machinjio ya kisasa wanyama kama ng'ombe, mbuzi n. k huchinjwa baada ya kupigwa shock ya umeme. Kwani hayo siyo mateso? Ukatafakari na kuchunguuuza utakuwa unakula udongo tu. Na hata udongo wenyewe hukanyagwa sana tu. Chagua moja basi, usile chochote. Eee maana hamna namna.
 
Anae pigwa Shoka haumii, Just single hit anapoteza faham pengine kifo kabisa, hayo maumv anayapatia wapi

Ungetupa uzoefu jinsi ulivyoshiriki kuhisi hiyo hali
 
mi sjakuelewa point yako ni ipi labda? tusile sababu ya huruma au?
 
Vipi kama ukijua kwamba Mnyama kabla ya kupigwa shoka huwa anajua kwamba atapigwa shoka na kwamba anapitia mateso ya ajabu sana, kama vile wewe labda ujue kwamba baada ya dakika mbili utapigwa Panga la kichwa ufe, vipi bado utaendelea kula Nyama?
Wewe ona huruma, lakini mkongwe Simba na vijana wake chui, mbwa mwitu, Duma wenyewe huwa hawajiulizagi linapokuja suala la kutafuta kitowewo
 
Ukipata nafasi ya kujua mateso ambayo Mnyama anayapata au anapitia kabla hajachinjwa, Je, bado utaendelea kula nyama yake?
HIS IMPERIAL MAJESTY EMPEROR HAILE SELASSIE I THE FIRST
JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Samaki siyo mnyama, so kiimani hana sifa ya kuchinjwa
 
Wewe ona huruma, lakini mkongwe Simba na vijana wake chui, mbwa mwitu, Duma wenyewe huwa hawajiulizagi linapokuja suala la kutafuta kitowewo
Hivi unaamini kuna mwanadamu mwenye huruma kwenye suala zima la kutafuta mlo? hakuna hiyo kitu
 
Sintakubali kubwaga damu ya kiumbe chochote cha Mungu ISIPOKUWA MBU TU. Na hata nikishuhudia mnyama anachinjwa siwezi kumla. Sijui wale wachinjaji watamueleza nini Mungu siku ya mwisho maana Mungu katika kitabu cha KUTOKA 20:23 amesema usiue na hakufafanua usiue mnyama, au binadamu
 
Back
Top Bottom