Ukiijua hii Saikolojia na tabia ya Askari Polisi, hawatakusumbua sana

The Initiator huru

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
1,345
2,000
Maisha haya bhana!

Nilipokuwaga mdogo nilikuwa na akili finyu sana nadhani kuliko watoto wote wa mtaani kwetu.. Niliamini kirahisi sana mambo bila hata kufikiri kwa kina yaani zile akili teketeke za kitoto..yaani nikitaka kuamini jambo basi naamini mwenyewe tu bila hata kuuliza mtu wala kujisumbua kulichambua na kuingia ndani zaidi kifikra, mfano niliamini polisi wote wanajua kufanya kila kitu kuanzia kuendesha gari, pikipiki, ndege, kupiga risasi, hadi kuwa na akili kubwa kuliko wote...maana niliwahi kuwa na rafiki yangu mmoja baba yake alikuwa anaendesha lile pikipiki a kuongozea misafara ya viongozi wa serikali,

Sasa Mimi kwa akili yangu ya kitoto baada ya kuona hata Rais wa nchi anaongozwa njia na traffic nikaamini watakuwa super human hawa yaani hata Rais wa nchi haijui njia vizuri hadi hawa wamwongoze? Watakuwa na akili kubwa sana hawa mapolisi. Ahahaha!! Utoto una mengi sana ya kustaajabisha na kufurahisha.

Sikuishia hapo kuna siku niliona ajali imetokea na umati mkubwa sana uliwasubiri polisi waje wapime pale ile ajali ilipotokea..ilizidi kuchochea Mimi kuhisi polisi Wenda ndio binadamu wenye akili na ujasiri sana Duniani maana wamesubiriwa waje waamue hatma ya ile ajali. Sikujua, I was kid and Naïve.

Mattet of fact, Kuishi na mjomba aliekuwa Kamanda wa Polisi na Kukulia pia kuishi karibu na kambi ya polisi kwa zaidi ya miaka 20 kulinifanya niwe karibu na askari wengi sana kuanzia utoto wangu hadi ukubwani nina marafiki wengi tu mapolisi, hii ilinisogeza na kunifanya niwe karibu na maisha yao ya kila siku, ambao baadhi wamekuwa ni rafiki zangu wa kutupwa hadi kesho maana kuna walio wema na wazuri sana tofauti na wengi tulivyowakariri kwa picha mbaya ya umoja wao kama watu makatili, wanyang'anyi, waonevu e.t.c but trust me! wapo ambao ni wema, waungwana, waelewa na wenye huruma zaidi yetu sisi Raia wa kawaida.

Anyways, Baada ya kwenda chuoni na kusoma masomo yangu ambayo yalijumuisha na pure psychology kama minor discipline ambamo humo nilikuja kugundua Polisi almost wote wana kitu kitaalamu kinaitwa "Superiority complex" hii ni ile hali ya kuona wao wako juu yako wewe Raia kimamlaka na kimabavu hivyo wengi wanategemea kukuona ukikubali na kutekeleza maagizo, maelekezo na amri kutoka kwao bila majadiliano yeyote, afande yeyote Duniani anachukia sana kukuona ukijadili kichwani mwako kutekeleza amri aliyotoa. Hii ndio iliwafanya wakaja na msemo wao "Utii wa Sheria bila shuruti" msemo huu huko wazi kabisa wanataka wewe uwape nafasi yao ya "superiority" sababu hicho ndicho wanachofeel na kutaka kukiona kutoka kwako na ndicho kinachowaplease na kuwapa raha rohoni.

Ufanyeje sasa ili umuwin vizuri huyu kaka Polisi na aione hii superiority yake? Wewe hakikisha una adjust wewe mwenye psychologically hadi uhakikishe Afande anapata nafasi yake ya kuiona ile superiority complex, akikupa amri halali hakikisha unaitii kwa heshima na unyenyekevu huku ukimuonesha kwamba wewe huna shida wala maneno nae na mara zote epuka majibizano nae yasiyo na tija kwako hayakusaidii zaidi unamprovoke tu kaka Polisi, jitahidi kukaa kimya panapotakiwa lakini si saana maana sometimes wanatafsiri ukimya kama dharau na ngebe lakini dhumuni lako ni kuiwin trust yake zaidi ili akuamini na akupe hata mwanya wa wewe kumuachia manyoya na kumtoroka ikibidi kwa yeye kukuover trust.

Maana tayari kakuamini na kukuona wewe sio combatant zaidi kwake. Kamwe usibishane nae na kutaka kumnyang'anya superiority yake atakumwaga mavi hadharani na kwa mara ya kwanza utajua ni kwanini IDD Amini Dada aliitwa Dada wakati alikuwa wa kiume ....

Kuwa mwelevu, makini na mtulivu wakati wote ukiwa unampanga kimkakati Mwela hata kama kakukalisha chini ya sakafu ukipanic na kujifanya unazijua haki zako zaidi ya mwenyekiti wa wanasheria Tanganyika utapigwa vibao, virungu vya kila rangi ili akili ikukae sawa utambue kwamba bado huko Umatumbini kwa akina Nyani Shambuku na sio majuu kwa waliostaharabika kitambo tangu mwaka 1058 B.C ambapo tangu zamani wana askari wa doria maalumu ya magari na helicopter kila siku kwa ajili ya kuokota walevi wanaomangamanga usiku kila mtaa ili wasifunikwe na barafu na kufa kwa kuwalaza kituoni hadi kunapopambazuka wanawaachia huru bila mashtaka yeyote then ikifika tena usiku njemba zinarudi tena Bar kupiga vyombo zinaokotwa na kupelekwa kituoni kwenye mablanketi na vitanda special vya kupumzika walevi kwenye kituo cha Polisi kwa usalama wao.

Hii ni Africa ambayo ni hatari zaidi Raia kuwa sahihi huku serikali ikiwa imekosea ni hatari sana..... Ukiwa mbele ya kaka polisi kama kuna kitu kinamchefua na kumpandisha hasira ni kujua wewe unajua haki zako na unataka kuzidefend hata aggressively ikibidi...its very risk..!

Na nakusisitiza utafia mikononi mwa polisi ukiendekeza tabia ya kusisititizia haki zako ukiwa mikononi mwao labda kama huko na Barrister/ lawyer wako on spot. Wewe zijue haki zako ila unatakiwa ujue namna ya kuzipresent humbly and smoothly kwa kaka polisi ili aendelee kukafeel kale ka superiority kake unless ukikabutua ka superiority unamfanya apate inferiority complex na Daima huwa hawana uvumilivu wa kukumbatia inferiority complex mbele ya Raia huwa hawana namna nyingine zaidi watakuchakata sana mkuu hadi ujiadjust kulingana na uhalisia wao wenyewe.

Jitahidi uijue hii psychological mind battle kati yako na bwana Afande wa kiafrika once ukiimaster hata yule RPC wa Dodoma hawezi kukuadhiri kwenye Press conference zake maana ukikutana nae kwenye preliminary interrogation nae wewe Fanya kazi ndogo ya yeye kuiona superiority yake once akiikosa ataenda kuisaka mbele ya waandishi wa habari akiwa anakushika bega na kukuadhiri bongo nzima kama Nabii Tito vile .... Uzembe kama huu ulimgharimu hata marehemu Mwangosi, alichukua superiority yao akina Afande then wakaitafuta kwa nguvu at last ikagharimu maisha ya huyu innocent journalist, Mwandishi wa habari aliefirigiswa na mamwela majuzi kati kwenye simba Day nae alishindwa kuendana na hii rhythm ya superiority e.t.c

Ukijifanya kuzijua zaidi haki zako utasikia Afande hili linajifanya ni "Libush lawyer" means wewe unajifanya mwanasheria wa kijijini anaejifanya anajua Sheria kumbe hujui... Hapo ndio kwa wale mamwela wa zamani... Linafuata swali kwa sauti ya ukali huku akiwa kashika kitambulisho chako utasikia wewe unaitwa nani? Unajibu naitwa Maiko, unamsikia Afande anang'aka kwa ukali kwa wenzake mnaona maafande limetudanganya linaitwa maiko wakati kitambulisho chake kimeandikwa "Michaeli".... Anakunawa zinga la Kofi usoni pwaaaaaaaaaa... Yaani ni visa tu na mikasa ili aipate superiority yake ilhali ni makosa yake ya kiusomaji tu lakini yeye lengo lake kubwa ni kuisaka superiority yake hata kwa mlango wa nyuma anasahau wakati wewe unasoma yeye alikuwa Muheza - Tanga anauza machungwa then Anko wake akampa kimemo akawa Mwela unfortunately sasa yupo kazini kusoma tu jina anascratch kama CD iliyochubuka vile afu anakuangushia wewe Raia kama ndio kosa lako vile kutaja Maiko.

Then wana kitu kingine kitaalamu kinaitwa "conspiracy of silence" yaani wana mambo yao ambayo wanafeel pleasant sana kuongea wao wenyewe Kama wenyewe nilikuwa na washkaji zangu Mamwela kipindi nikiwa wadogo unasikia redio zao zinaongea mara November... Mara India mara Lima... Yaani upo karibu lakini ung'amui hata moja wakiamua kuongea kwa yale malugha yao ya kipolisi ndio unatoka kapa zaidi. Ila hata mkoloni alilijua hili akawatengenezea Barracks zao au kotazi huko wao wana maisha tao wenyewe na lifestyle yao wenyewe tofauti na wengine.

Hivyo hata wakikaa mtaani watalazimisha waipate hii haki yao ya faragha na kuwa wao sasa kama Raia ni vyema ukiwa nao kama washkaji au mtuhumiwa uwape hii space ya wao kuwa na muda wao wa kuongea lugha yao wanayaoelewana wao tu. Hata wakikukamata give them space ya wao kuishi hii Dunia yao adhimu kidogo. Ukiwa mtumhumiwa pia wape hii nafasi sio unaona kaka polisi anataka kuongea na polisi mwenzie lugha yao unaleta pua yako. Watakupukusa na rungu ushindwe kutembea ili uwape hii nafasi ya kufanya their own conspiracy of silence, Mimi huwa naiita Police to police heart to heart talks.

Wana triple "W" woman, war and whisky, askari kamili alieiva anazunguka katika hivi vitu vitatu, askari alieiva anapenda sana mademu kwa maana ya woman, then anapenda sana ubabe usio na msingi ili adominate na kuwa superior na pia anapenda mtungi ndio maana wamewekewa na canteen zao za kulewa kwa bei chee kabisa ili watimize cycle yao ya W... Askari alieiva ni yule anaemiliki hizo "W" kikamilifu.

Kimsimgi sikumbuki ni lini nimeingia kwenye 18 za askari nikashindwa kumuwin psychologically maana physically simuwezi naanzia deep down his mental processing then mwilini najua patafuata tu yale niliyopandikiza akilini mwake during my first impression kwake. Make sure you Don't cross his line, ukimprovokes negatively utageuka nzi atakutega kwa mavi na sio Mchele kama ukiwa mpole, makini na mwelevu mwenye Pendo fake kama njiwa manga.

Nina mengi zaidi ya kushare na kudiscuss na nyie wakuu ila kwa leo tutembee na haya ya fasta fasta niliyoandika hapo juu, nikisettle vizuri nitaandika deeply and precisely kuhusu police psychology.

Lastly, tuwaheshimu na kuwasamehe ndugu zetu polisi kwa mengi mabaya wanayotufanyia inaweza kuwa sababu ya stress na solid depression wanayopitia kulingana na nature ya kazi yao pia niwape heko kwa kuwa miongoni mwa champion wa kuhandle stress wanazokutana nazo kila siku kazini na niwaase wanasiasa kutowatumia polisi vibaya kwa interest zao ili social harmony and peace itawale milele taifa la Bongo. Amen!

Imekaa vibaya kama Kally P. View attachment 841866 View attachment 841867 View attachment 841868 View attachment 841869 View attachment 841870 View attachment 841871
mkuu tuwekee na audio mm nimejitahidi but nimeshindwa kabisa kumalizia kusoma, hakuna vituo kabisa
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,715
2,000
Naomba unijibu.

Unaweza jua wanawake anaotembea nao baba yako?
Unaweza ukaelewa kutokana na kashifa za kifamilia.

Mfano kinamama mahawara zake kuleta malalamiko ya matunzo ya watoto na wengine kuja kutelekezea wadogo zako mlangoni kwenu ajili ya kutopata matunzo ya baba yao.

Ama ugomvi wa baba na mama nyumbani kwenu unaotokana na mzee kubobea kwenye nyumba ndogo zake na kutelekeza familia yenu na mambo kama hayo nk nk.

Kwa mtu mzima hauwezi kushindwa kuelewa tabia halisi za wazazi wako kwa kuwa unaishi nao.

Katika 'komenti' yako ilitakiwa umsafishe pia kwa hilo ili tukuunge mkono kuondoa dhana dhaifu za wadau kuwa wanajeshi ama polisi ni wakorofi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
24,521
2,000
Unaweza ukaelewa kutokana na kashifa za kifamilia.

Mfano kinamama mahawara zake kuleta malalamiko ya matunzo ya watoto na wengine kuja kutelekezea wadogo zako mlangoni kwenu ajili ya kutopata matunzo ya baba yao.

Ama ugomvi wa baba na mama nyumbani kwenu unaotokana na mzee kubobea kwenye nyumba ndogo zake na kutelekeza familia yenu na mambo kama hayo nk nk.

Kwa mtu mzima hauwezi kushindwa kuelewa tabia halisi za wazazi wako kwa kuwa unaishi nao.

Katika 'komenti' yako ilitakiwa umsafishe pia kwa hilo ili tukuunge mkono kuondoa dhana dhaifu za wadau kuwa wanajeshi ama polisi ni wakorofi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakutokea mtu nje kudai matunzo.

Sikushuhudia ugomvi wa ugoni.

Ningefanyaje ili nijue kua ana kazi za nje?
 

Bi Khadija

Member
Aug 20, 2018
79
150
WEWE NI ASKARI. ASKARI HAWANA SUPERIORITY COMPLEX. WANA INFERIORITY COMPLEX ndo Maana wanakuwa WAOGA NA WENYE HASIRA SABABU WENGI NI WALIO FAIL. HAT SAIKOLOJIA HUIFAHAM. KILAZA TU. MTU MWENYE SUPERIORITY COMPLEX ANAPUUZA MAMBO MENGINE. Askari sababu anaji feel inferior ndo anataka aogopwe au anakuwa mbabe. Ukimwelimisha anaona ni sababu unamwona hana elimu au ni mtu wa chini anaishia kuwa mkali na mbabe
 

Mkomavu

JF-Expert Member
Jan 25, 2016
11,609
2,000
WEWE NI ASKARI. ASKARI HAWANA SUPERIORITY COMPLEX. WANA INFERIORITY COMPLEX ndo Maana wanakuwa WAOGA NA WENYE HASIRA SABABU WENGI NI WALIO FAIL. HAT SAIKOLOJIA HUIFAHAM. KILAZA TU. MTU MWENYE SUPERIORITY COMPLEX ANAPUUZA MAMBO MENGINE. Askari sababu anaji feel inferior ndo anataka aogopwe au anakuwa mbabe. Ukimwelimisha anaona ni sababu unamwona hana elimu au ni mtu wa chini anaishia kuwa mkali na mbabe
Umetumia maneno makali sana dhidi ya askari
 

NEVADA

JF-Expert Member
Oct 15, 2017
464
1,000
Polisi wasenge tu , mimi hawanitishi kwa lolote hao mbwa , wakini zingua tunatwangana ngumi tu . Nilishawahi mfumua pongo
 

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,504
2,000
1. police wa bongo dawa yao ndogo! kuwa mkimya tii amri lakini with authority. mfano muanze wewe kumsalimia tena mwambie 'POT kWEMA?' Hapo nakwambia 50% ya comfo linamuisha. muongeleshe halari za kikazi za kipolisi kama kuna tukio ama operation unayoijua inaendelea wewe ndio umwambie na umsifu na kulisifu jeshio la polisi na makamda wake na kama uko wilaya au mkoa huyo mwaga sifa kwa kiongozi wao ukimtaja jina na ukionesha mna mahusiano. i.e nitamwambia Mambosasa tukiktana hili......... halafu mwambie enhee kulikoni pot ? hapo atakwambia sababui za kukusimamisha wakati mwingine atakwambie nenda au atatunga sababu isiyo na maana na hapo utaambiwa ondoka.

2. kama ni mpitaji wa barabara hiyo (hasa traffic) basi uqwe na kawaida huna kosa unasimama unawasalimia na kuwasifia kama una maji ya 1/2 katikia gari wape hasa kama kuna jua kali! usiwape hela, sasa hapo ushweka bima!! anytime ukisimamishwa basi wanaambiana achana na huyo!! mpo?
 

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,504
2,000
Lakini silaha ya mwisho tuwe watii wa sheria ili wakija kichwa kichwa hasa wale hardliners bassi wanakwama!
 

Thesis

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
1,417
2,000
Maelezo marefu kweli kweli safi sana.

Askari shupavu anakamilisha cycle ya W? Siyo kweli. Hii iko kwenye muvi zaidi na maandiko ya mitandaoni.

Kwamba Mabeyo na Siro wanapiga ulabu kushinda Jibapa?

Sababu pekee sinywi pombe ni kwasababu katika familia nilikosa wa kuchagiza hata kuionja pombe.
Baba ni mwanajeshi mstaafu, hajawahi kunywa pombe wala kuvuta sigara tangu napata akili mpaka leo. Wanawake siwezi kumsemea, ubabe najua hana ni civil sana.

Psychologically askari anaact shit siyo kwasababu ya superiority ila ni kwa sababu ubongo wa binadamu uko programmed hivyo. Yaani hata leo Humble African ukikabidhiwa mamlaka ya kuamua hatma ya mustakabali wa mtu una chance nzuri ya kua sadist soon.

Hiyo iko proved na experiment hii
Stanford prison experiment - Wikipedia

Au kwenye muvi ya Forest Whitaker inaitwa The Experiment.
Hii theory naweza kuikubali pia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom