S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Moja ya sababu ambayo huwa inanipeleka Mlimani City ukiacha kwenda kununua baadhi ya vitu ambavyo madukani ni ghali zaidi kama Maji na vitu vidogo vidogo ni kwenda kupoteza mawazo kidogo kama kushangaa Watanzania wengi wanavyoigiza maisha yao. Lakini inafariji sana kwa muda mfupi. Pale Mlimani City, huwezi kumjua wa Temeke, Gongolamboto au Manzese Uswahilini kabisa. Wote utadhani wanakaa Masaki, Mikocheni au karibia wote kabisa ukiwatazama walivyovaa, wanavyotembea utadhani Taifa hili liko katika Uchumi wa Juu kabisa au kama si wa juu liko katika Uchumi wa Kati. Kumbe ni Usasa tu uliopo Mlimani City (Modernization) na si vinginevyo. Mnajua wale mliosoma nadharia ya Usasa (Modernization Theory). Mmmmmmh!!! Ahsante Mlimani City.
Ahsante sana kwa kuwa na Mlimani City, naomba watengeneze sehemu nyingi zaidi ili shida zetu tukazipoze hapo.
Globalization is a real discourse.
Ahsante sana kwa kuwa na Mlimani City, naomba watengeneze sehemu nyingi zaidi ili shida zetu tukazipoze hapo.
Globalization is a real discourse.