Ukielewa mazuri ya Bima ya Afya kwa wote, huwezi kupinga tena Mpango huu wa Serikali

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
*UKIELEWA MAZURI YA BIMA YA AFYA KWA WOTE, HUWEZI TENA KUPINGA MPANGO HUU WA SERIKALI.

Leo kwenye Gazeti la Tanzania Leo nimeuchambua Mpango wa Serikali wa kuja na Bima ya Afya kwa wote ambao utawawezesha Wananchi wote kupata huduma za matibabu hata kama hawana fedha na kuokoa Watanzania wote na maskini wanaoshindwa kumudu gharama za matibabu. Muswada wa Bima ya Afya kwa wote utapelekwa Bungeni na Wizara ya Afya kesho Alhamisi, kujadiliwa kabla ya kupitishwa na kuanza kutekelezwa kwa kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa na Bima.

Matibabu bila Bima ni gharama sana na wengi wamekuwa wakishindwa hivyo kupitia Bima ya Afya kwa wote, Watanzania watapata huduma bora kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa. Soma Makala hii uone Mpango huu ulivyo na nia njema kwa Watanzania kwa kupata uhakika wa matibabu na kuondoa mambo ya kuuza mali na kufilisika kisa ugonjwa.
Screenshot_20230208-110211.png
IMG-20230208-WA0009.jpg

Bwanku M Bwanku.
bwanku55@gmail.com.
 
Wizi mtupu, hao wenye bima sasa hivi mbona hawana hizo huduma bora? Mmeshachota pesa kwenye mifuko ya bima za afya na kuifilisi ili kusaka sifa za kisiasa, sasa hivi mnarudi kwa gia nyingine ili kupora hela za wananchi.
 
Unaropoka sababu ni mzima, ila siku yakikukuta ndo utakumbuka huu uharo
 
Pumbavu kabisa, subiri ww kwenye huo utapeli. Mzee wangu aliugua na hiyo bima haikumpa matibabu yoyote ya maana.
Acha matusi bwana mdogo lete hoja uliona wapi huo utapeli? Mana sisi wengine tunahitaji kujifunza kutoka kwa ninyi mnaojua jambo hili sasa mnatuchanganya mwaga hoja zako ijulikane ulichoongea, sisi tuliielewa sasa tujuze hoja zako
 
Wizi mtupu, hao wenye bima sasa hivi mbona hawana hizo huduma bora? Mmeshachota pesa kwenye mifuko ya bima za afya na kuifilisi ili kusaka sifa za kisiasa, sasa hivi mnarudi kwa gia nyingine ili kupora hela za wananchi.
Umechemsha ndugu, huduma za bima ya afya nchini ni bora kuliko unapotibwa kwa sasa. Au unashambulia tu bila hoja.
 
Acha matusi bwana mdogo lete hoja uliona wapi huo utapeli? Mana sisi wengine tunahitaji kujifunza kutoka kwa ninyi mnaojua jambo hili sasa mnatuchanganya mwaga hoja zako ijulikane ulichoongea, sisi tuliielewa sasa tujuze hoja zako

Niache matusi au nimemjibu huyo mjinga kutokana na ujinga wake?
 
Huwezi sema ni Wizi mtupu, Jitihada za serikali ni kuhakikisha bima hii mpya iliyoboreshwa inampa nafuu mwananchi kupata huduma nyingi za afya katika vituo vya afya, bima ya mwanzo ilimbana sana mgonjwa kupata huduma baadhi ukilinganisha na hii mpya.

Vilevile bima hii inampa mtu uwezo wa kutibiwa hata nje ya mkoa au wilaya aliyojiandikishia.
 
*UKIELEWA MAZURI YA BIMA YA AFYA KWA WOTE, HUWEZI TENA KUPINGA MPANGO HUU WA SERIKALI.

Leo kwenye Gazeti la Tanzania Leo nimeuchambua Mpango wa Serikali wa kuja na Bima ya Afya kwa wote ambao utawawezesha Wananchi wote kupata huduma za matibabu hata kama hawana fedha na kuokoa Watanzania wote na maskini wanaoshindwa kumudu gharama za matibabu. Muswada wa Bima ya Afya kwa wote utapelekwa Bungeni na Wizara ya Afya kesho Alhamisi, kujadiliwa kabla ya kupitishwa na kuanza kutekelezwa kwa kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa na Bima.

Matibabu bila Bima ni gharama sana na wengi wamekuwa wakishindwa hivyo kupitia Bima ya Afya kwa wote, Watanzania watapata huduma bora kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa. Soma Makala hii uone Mpango huu ulivyo na nia njema kwa Watanzania kwa kupata uhakika wa matibabu na kuondoa mambo ya kuuza mali na kufilisika kisa ugonjwa.

Bwanku M Bwanku.
bwanku55@gmail.com.
Kama hiyo bima ni Bure , itawasaidia watu wengi, lakin kama ni ya kulipia kwa lazima, Ili nipate NIDA, passport, TIN ,lazima niwe na bima , naipinga bima ya kijambazi mpaka dk ya mwisho.

Ukweli usemwe, serikali rudisheni madeni mnayo daiwa na nhif na sio kuwatupia wananchi mzigo huo, kumbukenini tuna tozo tayar, alafu tena bima ya utake usitake
 
Sawa tuelekeze basi utapeli upo wapi ili tujue na sisi

Narudia tena, nilimtibu mzazi wangu aliyekuwa na bima ya afya, adha niliyokutana nayo nilijuta kwanini alijichanganya. Na sio yeye tu, wengi wa wagonjwa niliokutana nao wenye kupata matibabu kwa bima ilikuwa ni changamoto.

Hiki kinachoenda kufanyika sasa, ni kukusanya fedha za watu, huku wakiwa hawana uhakika wa huduma bora. Hizo fedha zitaishia kuchotwa na kuingizwa kwenye miradi ya kusaka sifa za kisiasa, huku wananchi wakiwa hawana uwezo wowote wa kuhoji fedha hizo.
 
*UKIELEWA MAZURI YA BIMA YA AFYA KWA WOTE, HUWEZI TENA KUPINGA MPANGO HUU WA SERIKALI.

Leo kwenye Gazeti la Tanzania Leo nimeuchambua Mpango wa Serikali wa kuja na Bima ya Afya kwa wote ambao utawawezesha Wananchi wote kupata huduma za matibabu hata kama hawana fedha na kuokoa Watanzania wote na maskini wanaoshindwa kumudu gharama za matibabu. Muswada wa Bima ya Afya kwa wote utapelekwa Bungeni na Wizara ya Afya kesho Alhamisi, kujadiliwa kabla ya kupitishwa na kuanza kutekelezwa kwa kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa na Bima.

Matibabu bila Bima ni gharama sana na wengi wamekuwa wakishindwa hivyo kupitia Bima ya Afya kwa wote, Watanzania watapata huduma bora kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa. Soma Makala hii uone Mpango huu ulivyo na nia njema kwa Watanzania kwa kupata uhakika wa matibabu na kuondoa mambo ya kuuza mali na kufilisika kisa ugonjwa.

Bwanku M Bwanku.
bwanku55@gmail.com.
Kabla hujafanya majumuisho kupitia mafanikio ya uendeshaji wenye tija wa mpango kama huo wa bima ya afya kwa wote, pengine labda ungetupa mfano mmoja tu wa mafanikio yake kwa mojawapo ya nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Tatizo kubwa la wasomi wa nchi yetu huwa hawaonyeshi sehemu sahihi, na namna bora ya kuanzisha uwekezaji mkubwa kama huo, bali wao hukimbilia kutoa sifa kedekede kwa kitu ambacho "pilot study" hata bado haijaanza kufanyika. Kabla ya kukimbilia kufanya kitu kikubwa kama hiki, ni vyema serikali ingeaanza kwa kutaka kutambua mafanikio na changamoto kwa maeneo machache teule, kabla ya kukimbilia kuanzisha mpango wake kwa nchi nzima.

Pengine tujaribu kudadisi juu ya changamoto za mpango wa "Obamacare Insurance" ambao ulikuwa ni mahususi kwa ajili ya waajiri na waajiliwa wenye vipato vya chini. Hapo tutang'amua kuwa ambao kuwa ni gharama kubwa sana kuuendesha, tena hii imetokea kwa nchi tajiri kama Marekani.

Sasa hapa tunazungumzia mpango wa bima ya afya wenye kuwahusu Watanzania wapatao milioni 62 waliopo mijini na vijijini. Hivi miundombinu yetu ya kiafya, usambazaji wa madawa, huduma za bima ni rafiki kiasi gani kufikia kiwango cha kutaka kukurupuka kufanya kitu kikubwa kama hicho!?
 
*UKIELEWA MAZURI YA BIMA YA AFYA KWA WOTE, HUWEZI TENA KUPINGA MPANGO HUU WA SERIKALI.

Leo kwenye Gazeti la Tanzania Leo nimeuchambua Mpango wa Serikali wa kuja na Bima ya Afya kwa wote ambao utawawezesha Wananchi wote kupata huduma za matibabu hata kama hawana fedha na kuokoa Watanzania wote na maskini wanaoshindwa kumudu gharama za matibabu. Muswada wa Bima ya Afya kwa wote utapelekwa Bungeni na Wizara ya Afya kesho Alhamisi, kujadiliwa kabla ya kupitishwa na kuanza kutekelezwa kwa kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa na Bima.

Matibabu bila Bima ni gharama sana na wengi wamekuwa wakishindwa hivyo kupitia Bima ya Afya kwa wote, Watanzania watapata huduma bora kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa. Soma Makala hii uone Mpango huu ulivyo na nia njema kwa Watanzania kwa kupata uhakika wa matibabu na kuondoa mambo ya kuuza mali na kufilisika kisa ugonjwa.

Bwanku M Bwanku.
bwanku55@gmail.com.
Weka hapa huo muswada tusome
 
Kama kipato chako si cha uhakika bora ujichange ukate bima inapunguza gharama za huduma hela utakayolipa kwa cash kupata huduma mara mbili au tatu ukiwa na bima una uhakika wa kupata huduma mwaka mzima
 
Back
Top Bottom