Ukicheleweshwa mahali...umewahishwa mahali

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,193
^^
Nilialikwa kwenye tafrija fupi ya kuwapongeza wanandoa wawili.Wanandoa waliotimiza miaka 25 katika ndoa.Nilifika mapema sana,tafrija ilikuwa inaanza saa 12,sitaki kutaja chakula,burudani na manjonjo yaliyokuwepo maana ntachokoza njaa za watu bure.
...
Kilichonipendeza ni namna wanandoa hawa walivyokuwa wamejawa tabasamu,faraja,na wakiwa wana matumaini mapya utadhani ndio kwanza wamefunga ndoa leo.
Lakini maneno yao machache juu ya simulizi zao yalijengwa juu ya neno moja 'haikuwa rahisi' Hilo halikunivutia kwani kila aliyekuwa ukumbini bila shaka alijua haikuwa rahisi.Kilichonivutia ni hichi
...
Namna walivyoingia katika ndoa.Mume alieleza namna alivyokutana na mkewe,alikuwa darasa la saba kamaliza,na mkewe alikuwa Mganga Mkuu wa wilaya.Binti ambae wakati huo anasema,alikwisha poteza tumaini la kuolewa.Alishazomewa akafika hatua akazoea,alishasimangwa akafika mahali akaona maneno ya watu hayaui.Walitueleza namna ndugu na jamaa walivyopinga uhusiano huu,walivyotengwa,na kwenda kuombewa kwa viongozi wa dini kuwa wamechanganyikiwa na walivyotishiwa radhi.Lakini kadri walivyopitia magumu ndivyo walivyopendana zaidi kiasi kuwa mke alimsomesha mume,hadi akawa Daktari kama yeye,wana watoto,majumba na kila ndugu akifika kwao hataki kurudi alikotoka
...
Nilijifunza mengi,lakini kubwa ni kuwa UKICHELEWESHWA MAHALI..UMEFIKISHWA MAHALI Mke alicheleweshwa ndoa lakini alifikishwa kwa mtu aliyemsitahili.Mume alicheleweshwa elimu lakini alifikishwa katika hekima na utaratibu
...
Kuna watu wamechelewa kupata wenza wao,lakini wamefikishwa katika darasa la subira,Kuna watu wamecheleweshwa kupata watoto lakini wamefikishwa katika somo la kuomba,Kuna watu wamecheleweshwa katika uchumba lakini wamefikishwa katika kujifunza ili wakimpata wajue thamani yake,Kuna watu wamecheleweshwa na mitazamo yao lakini wamefikishwa katika mitazamo.
...
Maisha yetu yote yana desturi ya kutuchelewesha Lakini tukikagua vizuri kuna mahali yametufikisha.
Hicho ndicho nilichojifunza.Waswahili wanasema Kizuri kula na umpendae.
Nimewaletea niwapendao MMU.
...
CC:
Queen Kan mimi49 Mentor Heaven on earth Mashaxizo Toria Lady doctor Munkari Nivea data lara 1 mwekundu Ablessed @FixedPoint Kaunga kiwatengu Mtambuzi UNDENIABLE Shine Swts Blue G GRAffan1 Mshinga christine ibrahim awp na kila mmoja
^^
 
Last edited by a moderator:
^^

Nilijifunza mengi,lakini kubwa ni kuwa UKICHELEWESHWA MAHALI..UMEFIKISHWA MAHALI Mke alicheleweshwa ndoa lakini alifikishwa kwa mtu aliyemsitahili.Mume alicheleweshwa elimu lakini alifikishwa katika hekima na utaratibu

^^

Nimeipenda hii .....
"... Maneno haya, yawe faraja kwa wadada wote ambao hawajaoelewa na wamefikia hatua ya kukata tamaa".
Saa nyingine si jambo jema kulazimisha mambo hususani ndoa. Ni vyema kumuomba Mungu ili akupe mtu ambaye hata geuka kuwa sehemu ya maumivu yako ya moyo kwa kukutenda mabaya na kukusaliti.
 
nice stuff kwakweli uvumilivu mpenzi Heaven on Earth unatakiwa sana usione kama nakupotezea kuja kwenu kujitambulisha lahasha subira huvuta heri,ni matarajio yangu tutaishi kwenye uchumba miaka kumi pete likiwa limekuganda hapo kidoleni kama Madame B anavyosubiria ndoa huu mwaka wa kumi na tano kwa Mshinga
 
kitu pekee ambacho huwa nasema kinatushinda sana waafrika ni RISK TAKING.
mdada alichukua risk kubwa ambayo hata mimi ingekuwa ngumu kwangu kama ningekuwa mwanmke kuifanya mana imezoeleka kuwa wanaume tu ndio wanastahili kutoa pesa kusomesha wenzi wao.
ETI HAPA NAWEZA KUPATA DEMU MWENYE DEGREE ANISOMESHE TOKA FORM YANGU MPAKA NIWE KAMA YEYE?ngumu sana.
risk ya kwanza ni alipoamua kutumia pesa kwa mwanaume ambaye angeweza kumsaliti baada ya mambo kumnyokea kama wafanyavyo wengi.
Risk nyingine ni kumpeleka mtu shule huku hujui kama za darasani zinachaji.
HII NI NGUMU SANA AISE.
 
Nice Ujumbe....,Ujumbe mzuri

sasa hawa wanaokazania kuwa eti tukifikisha miaka 25 hatuolewi tena

sijui wanatokaga wap!!!!!!!!!!!!!!
ha ha ha ha lols ,jipe moyo utashinda.kumbee.....!!nimeamini miaka ikikata na inavyozidi kukata mwanamke anakua desperate
 
haki iwe sawa kwa waume na wanawake hata kama kuna risk moja ya falsafa za thread
 
Somo zuri sana yatupasa kuwa wavumilivu na hatutakiwi kukata tamaa mapema. Risiki kama ipo, ipo tu hamna "kucheleweshwa wala kuchelewa"
 
Hapa kuna mambo mawili ya kujifunza

1:Kuna haja kabisa wakati mwingine wa kutoisikiliza jamii
Unakuta mtu unajua unachokifanya lakini jamii inakujia juu kwa vitisho viingi sana,wanashindwa kujua kuwa masuala ya ndoa ni suala la mtu binafsi la halimuhusu mtu mwingine yoyote

2:Wakati mwingine maumbile yanapotusubirisha tunatakiwa tujue kuwa yupo alie sahihi kwaajili yetu,ni suala la uvumilivu tu,kwanza maumbile hayana kuchelewa,kuchelewa tunako sisi hasa pale tunapokuwa na tamaa ya kukamilisha yale tunayodhani ni mema kwetu

Kuna jamaa mmoja alikuwa analaumu kila siku kuwa hapati hela na akawa anamlaumu sana Mungu kwa hayo,muda ulifika alipata kazi nzuri sana na akawa analipwa kwa wiki,alikuwa analipwa sh 250,000!

Baada ya muda alianza ulevi akawa anabadilisha wanawake kila uchao,ilipita miezi 8 tangu apate ile kazi akatalikiana na mkewe,aliendelea na visa hadi siku moja akiwa amelewa aligongwa na gari na kufariki hapo hapo!!!!!!

Ndivyo ilivyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu Himidini hili ni somo zuri sana kwetu sote na hasa wenye mitazamo hasi kuhusu ndoa.
Kupitia ujumbe huu inaonyesha kwamba upendo huzidi fahamu zote, yaani watu hawa walipendana kiasi kwamba maneno ya ndugu na jamaa kwao hayakua pingamizi la kutimiza azma yao.

"UKICHELEWESHWA MAHALI..UMEFIKISHWA MAHALI ", huu msemo una mambo mengi ndani yake.So kwa yule aliyekata tamaa azingatie hili na kulifanyia kazi. Pia ikumbukwe kua upendo sio feeling ni kazi , kama huyo dada alivyofanya sehemu yake alihakikisha anamtengeneza mwanaume mwenye elimu anayopenda na hii imenivutia mno. Kwa kweli kama ukiweza kupata partner unaempenda na yeye akakupenda na kukuheshimu miaka 25 inakua kama siku 25, na ndoa inakua ina raha kupita kiasi.
 
kitu pekee ambacho huwa nasema kinatushinda sana waafrika ni RISK TAKING.
mdada alichukua risk kubwa ambayo hata mimi ingekuwa ngumu kwangu kama ningekuwa mwanmke kuifanya mana imezoeleka kuwa wanaume tu ndio wanastahili kutoa pesa kusomesha wenzi wao.
ETI HAPA NAWEZA KUPATA DEMU MWENYE DEGREE ANISOMESHE TOKA FORM YANGU MPAKA NIWE KAMA YEYE?ngumu sana.
risk ya kwanza ni alipoamua kutumia pesa kwa mwanaume ambaye angeweza kumsaliti baada ya mambo kumnyokea kama wafanyavyo wengi.
Risk nyingine ni kumpeleka mtu shule huku hujui kama za darasani zinachaji.
HII NI NGUMU SANA AISE.
Ni kweli mkuu huyu mdada anastahili pongezi na hata mkaka anaonekana mwaminifu na walipendana kwa dhati. Jambo lingine linaloshangaza ni jinsi huyo mkaka alivyoamua kumtokea mdada msomi wakati yeye alikua std 7 tu . Kweli aliamua liwalo na liwe. Pia hii inasaidia kutukumbusha kwamba usione vinaelea vimeundwa.
 
Hapa kuna mambo mawili ya kujifunza

1:Kuna haja kabisa wakati mwingine wa kutoisikiliza jamii
Unakuta mtu unajua unachokifanya lakini jamii inakujia juu kwa vitisho viingi sana,wanashindwa kujua kuwa masuala ya ndoa ni suala la mtu binafsi la halimuhusu mtu mwingine yoyote

2:Wakati mwingine maumbile yanapotusubirisha tunatakiwa tujue kuwa yupo alie sahihi kwaajili yetu,ni suala la uvumilivu tu,kwanza maumbile hayana kuchelewa,kuchelewa tunako sisi hasa pale tunapokuwa na tamaa ya kukamilisha yale tunayodhani ni mema kwetu

Kuna jamaa mmoja alikuwa analaumu kila siku kuwa hapati hela na akawa anamlaumu sana Mungu kwa hayo,muda ulifika alipata kazi nzuri sana na akawa analipwa kwa wiki,alikuwa analipwa sh 250,000!

Baada ya muda alianza ulevi akawa anabadilisha wanawake kila uchao,ilipita miezi 8 tangu apate ile kazi akatalikiana na mkewe,aliendelea na visa hadi siku moja akiwa amelewa aligongwa na gari na kufariki hapo hapo!!!!!!

Ndivyo ilivyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Maskini inasikitisha sana, wapo wasiothamini baraka za Mungu hudhani ni kismati tu kumbe kuna aliyesikia kilio chao. Wakati mwingine sijui ubinadamu hutusumbua yaani wakati unahitaji unaomba sana na baada ya kukipata basi hata hukumbuki ulikotoka .
 
Hapa kuna mambo mawili ya kujifunza

1:Kuna haja kabisa wakati mwingine wa kutoisikiliza jamii
Unakuta mtu unajua unachokifanya lakini jamii inakujia juu kwa vitisho viingi sana,wanashindwa kujua kuwa masuala ya ndoa ni suala la mtu binafsi la halimuhusu mtu mwingine yoyote

2:Wakati mwingine maumbile yanapotusubirisha tunatakiwa tujue kuwa yupo alie sahihi kwaajili yetu,ni suala la uvumilivu tu,kwanza maumbile hayana kuchelewa,kuchelewa tunako sisi hasa pale tunapokuwa na tamaa ya kukamilisha yale tunayodhani ni mema kwetu

Kuna jamaa mmoja alikuwa analaumu kila siku kuwa hapati hela na akawa anamlaumu sana Mungu kwa hayo,muda ulifika alipata kazi nzuri sana na akawa analipwa kwa wiki,alikuwa analipwa sh 250,000!

Baada ya muda alianza ulevi akawa anabadilisha wanawake kila uchao,ilipita miezi 8 tangu apate ile kazi akatalikiana na mkewe,aliendelea na visa hadi siku moja akiwa amelewa aligongwa na gari na kufariki hapo hapo!!!!!!

Ndivyo ilivyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

^^
Inaumiza lakini ndio ukweli,,Kuna wakati wa Mwanadamu na wakati wa Mungu.
Subira ni dawa katika maisha
^^
 
Mkuu Himidini hili ni somo zuri sana kwetu sote na hasa wenye mitazamo hasi kuhusu ndoa.
Kupitia ujumbe huu inaonyesha kwamba upendo huzidi fahamu zote, yaani watu hawa walipendana kiasi kwamba maneno ya ndugu na jamaa kwao hayakua pingamizi la kutimiza azma yao.

"UKICHELEWESHWA MAHALI..UMEFIKISHWA MAHALI ", huu msemo una mambo mengi ndani yake.So kwa yule aliyekata tamaa azingatie hili na kulifanyia kazi. Pia ikumbukwe kua upendo sio feeling ni kazi , kama huyo dada alivyofanya sehemu yake alihakikisha anamtengeneza mwanaume mwenye elimu anayopenda na hii imenivutia mno. Kwa kweli kama ukiweza kupata partner unaempenda na yeye akakupenda na kukuheshimu miaka 25 inakua kama siku 25, na ndoa inakua ina raha kupita kiasi.

^^
Shukrani Ablessed nilijifunza mengi..kukubaliana na kuumana mioyo ni silaha njema katika maisha.
^^
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom