^^
Nilialikwa kwenye tafrija fupi ya kuwapongeza wanandoa wawili.Wanandoa waliotimiza miaka 25 katika ndoa.Nilifika mapema sana,tafrijailikuwa inaanza saa 12,sitaki kutaja chakula,burudani na manjonjo yaliyokuwepo maana ntachokoza njaa za watu bure.
...
Kilichonipendeza ni namna wanandoa hawa walivyokuwa wamejawa tabasamu,faraja,na wakiwa wana matumaini mapya utadhani ndio kwanza wamefunga ndoa leo.
Lakini maneno yao machache juu ya simulizi zao yalijengwa juu ya neno moja 'haikuwa rahisi' Hilo halikunivutia kwani kila aliyekuwa ukumbini bila shaka alijua haikuwa rahisi.Kilichonivutia ni hichi
...
Namna walivyoingia katika ndoa.Mume alieleza namna alivyokutana na mkewe,alikuwa darasa la saba kamaliza,na mkewe alikuwa Mganga Mkuu wa wilaya.Binti ambae wakati huo anasema,alikwisha poteza tumaini la kuolewa.Alishazomewa akafika hatua akazoea,alishasimangwa akafika mahali akaona maneno ya watu hayaui.Walitueleza namna ndugu na jamaa walivyopinga uhusiano huu,walivyotengwa,na kwenda kuombewa kwa viongozi wa dini kuwa wamechanganyikiwa na walivyotishiwa radhi.Lakini kadri walivyopitia magumu ndivyo walivyopendana zaidi kiasi kuwa mke alimsomesha mume,hadi akawa Daktari kama yeye,wana watoto,majumba na kila ndugu akifika kwao hataki kurudi alikotoka
...
Nilijifunza mengi,lakini kubwa ni kuwa UKICHELEWESHWA MAHALI..UMEFIKISHWA MAHALI Mke alicheleweshwa ndoa lakini alifikishwa kwa mtu aliyemsitahili.Mume alicheleweshwa elimu lakini alifikishwa katika hekima na utaratibu
...
Kuna watu wamechelewa kupata wenza wao,lakini wamefikishwa katika darasa la subira,Kuna watu wamecheleweshwa kupata watoto lakini wamefikishwa katika somo la kuomba,Kuna watu wamecheleweshwa katika uchumba lakini wamefikishwa katika kujifunza ili wakimpata wajue thamani yake,Kuna watu wamecheleweshwa na mitazamo yao lakini wamefikishwa katika mitazamo.
...
Maisha yetu yote yana desturi ya kutuchelewesha Lakini tukikagua vizuri kuna mahali yametufikisha.
Hicho ndicho nilichojifunza.Waswahili wanasema Kizuri kula na umpendae.
Nimewaletea niwapendao MMU.
...
CC:
Queen Kan mimi49 Mentor Heaven on earth Mashaxizo Toria Lady doctor Munkari Nivea data lara 1 mwekundu Ablessed @FixedPoint
Kaunga kiwatengu Mtambuzi UNDENIABLE Shine Swts Blue G GRAffan1
Soo touchıng!!! Yaan Mungu hua hachelewı wala hawaı, He ıs always ontıme!